UKURASA WA 715; Kuhusu Kazi Na Mapumziko…

By | December 15, 2016

Watu wengi wa kawaida utawakuta wakizungumzia kuhusu kazi na mapumziko, kwamba ni muda gani ambao wanafanya kazi na muda gani wa kupumzika. Wengi wamekuwa wakikazana kupata usawa wa kazi na mapumziko, wasifanye kazi sana ili pia wapate muda wa kutosha wa kupumzika.

Wanaofanikiwa sana hawana kitu kama hiki, huwezi kumkuta mtu aliyefanikiwa anajaribu kutengeneza usawa wa muda gani afanye kazi na muda gani apumzike. Na hii ni kwa sababu waliofanikiwa hawafanyi kazi, bali wanafanya kitu ambacho wanakijali sana. Wanafanya kitu ambacho wapo tayari kukifanya muda wote. Na kama mtu upo tayari kufanya muda wote kile ambacho umechagua kufanya, hutakumbuka hata kuuliza ni muda gani w akupumzika.

SOMA; Kazi Ya Maisha Yako Yote…

Dhana hapa ni kwamba chagua kufanya kitu ambacho unataka kweli kukifanya, kitu ambacho upo tayari kukifanya muda wote. Na pia chagua kufanya hivyo na watu ambao unavutiwa kufanya nao, watu ambao mnaendana. Ukiweza kufika kwenye hali hii, hutakuja kujiona kama unafanya kazi hata siku moja. Badala yake utaona unayaishi maisha yako na wala hutakuwa unatafuta ni muda gani sahihi kwako kupumzika.

SOMA; Mitandao Ya Kijamii, Kazi na Mapumziko.

Wengi wanapata msongo wa mawazo kwa sababu ya kufanya kazi au biashara ambazo hawazipendi. Wengi wanachoka kwa sababu wanafanya mambo ambayo hayatoki ndani yao. Na wengi wanaanza kukata tamaa wanapoamka asubuhi wakikumbuka kwamba wana siku nyingine ya kazi, ya kwenda kukutana na watu ambao hawaendani nao, iwe ni kwenye kazi au biashara.

Acha kufanya kazi na anza kufanya maisha, na utaifurahia kila hatua ya maisha yako. Dhana ya kazi na kupumzika waachie wanaoendesha maisha ya kawaida.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.