UKURASA WA 758; Ushindi Wa Wengine Ni Muhimu Kwetu…

By | January 27, 2017

Duniani tunategemeana, inaweza kuwa moja kwa moja au isiwe moja kwa moja. Kikubwa ni kwamba huwezi kuishi kwenye dunia yako peke yako. Na kwenye dunia unayoishi, pale kila mtu anaposhinda, ndivyo maisha yanavyokuwa bora, na ndivyo na wewe unashinda pia.

 

Hata wale ambao ni washindani wako wa moja kwa moja, ushindi wao ni muhimu sana kwenye ushindi wako. Uwepo wao ni muhimu sana kwenye mafanikio yako.

Japo ni rahisi kufurahia pale wanaposhindwa, na wakati mwingine kutamani washindwe kabisa, lakini wakishindwa kabisa hata na wewe pia utashindwa.

Hebu fikiria kwenye michezo, timu za mpira kama simba na yanga, mafanikio ya simba yanategemea sana mafanikio ya yanga, na kinyume chake pia. Huwezi kuwa na yanga nzuri kama haina simba ya kuipa changamoto.

SOMA; Maneno Mazuri Ya Ushindi Kutoka Kwa Rafiki Yetu.

Hivyo pia kwenye kazi na biashara zetu,

Mfano kwenye biashara, kadiri wafanyabiashara wanapokuwa wengi, ndivyo watu wengi wanavyozidi kuona uwepo wa biashara zenu, wataenda kwa yeyote kupata huduma au bidhaa, baada ya kujua vizuri wataanza kutafuta kile kilicho bora zaidi. Hivyo wewe unachohitaji siyo kutaka wengine washindwe, bali wafanikiwe, na waweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Unachohitaji wewe ni kuwa bora zaidi kila siku, ili wale wateja wanaosaka ubora, wafike kwako na kuwa wateja wako pia.

Ushindi wa wengine ni muhimu mno kwenye ushindi wetu, hivyo kadiri tunavyopata nafasi, tuhakikishe tunawasaidia wengine kufanikiwa zaidi. Hivi ndivyo tunavyotengeneza mafanikio yetu pia.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.