UKURASA WA 764; Samaki Huanza Kuozea Kichwani…

By | February 2, 2017

Popote tunapokutana na changamoto, huwa tunaanza kuangalia nani wa kumlaumu. Na tukishaanza kutafuta wa kulaumu, huwa hatumkosi, kwa sababu ni rahisi kupata watu wa kuwalaumu. Lakini mara nyingi, chanzo cha changamoto kipo wazi.

Kama changamoto ni kwenye maisha yako binafsi, basi wewe ndiye unayezisababisha, na siyo mtu mwingine yeyote. Wewe pekee ndiye unayechagua kufanya au kutokufanya mambo fulani na hivyo kupelekea changamoto kutokea kwenye maisha yako.

Kama una changamoto kwenye biashara yako, jua kabisa wewe ndiye msababishi mkuu, wewe mwenyewe kuna mambo umefanya au hujafanya ambayo yanapelekea biashara yako kuyumba.

Na popote pale ambapo wewe ni kiongozi, yaani wewe ndiye unayefuatwa kwa namna mambo yanavyofanyika, iwe ni kwenye kazi, umeajiri au hata kwenye familia, wale walio chini yako, changamoto zao zinaanzia kwako. Yaani unapofika mahali na kukuta kuna matatizo fulani, jua kabisa matatizo hayo yanaanzia juu kabisa.

SOMA; Hakuna Kitakachotokea Kwenye Biashara Yako Mpaka Ufanye Vitu Hivi Viwili…

Kwa mfano ukifikia kwenye biashara ambayo wafanyakazi hawajali wateja, au hawajitumi na kuweka umakini kwenye kazi zao, basi jua kabisa hata mwenye biashara hajali wateja na wala haoneshi umakini kwenye biashara hiyo. Kwa sababu watu wa chini yake, wanafanya kile ambacho wanaona yeye anafanya.

Hivyo, popote ulipo, jitahidi sana kutengeneza utamaduni bora, kile ambacho unataka kiwe kinafanyika, anza kukifanya wewe. Namna unavyotaka watu wawe, anza kuwa wewe. Wale wote ambao wako chini yako wataiga na kufanya kama unavyofanya wewe.

Usijidanganye kwamba watu wanakuangusha, ukweli ni kwamba wewe ndiye unayewaangusha watu, hasa wale waliopo chini yako.

Samaki anaanza kuozea kichwani, hivyo changamoto zozote zilizopo chini yako, kwa hakika kabisa, zimeanza na wewe mwenyewe. Chukua hatua wewe ili kuweza kubadili mambo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.