UKURASA WA 811; Upo Muda Wa Kutoa, Lakini Haupo Wa Kurudisha…

By | March 21, 2017

Upo muda wa kutoa neno, wa kuongea kwa namna unavyotaka na unavyojisikia wewe mwenyewe. Lakini unachopaswa kujua kabla ya kufanya hivyo ni kwamba, ukishaongea huwezi kurudisha maneno yako, huwezi kuyafuta. Hata wale wanaoambiwa fura kauli, ni neno tu la kuridhisha lakini kila mtu atakumbuka ulisema nini.

IMG-20170314-WA0016

Hivyo basi, usiwe mtu wa kukumbilia kuongea, hasa pale unapokuwa umejawa na hisia za furaha, hofu au hasira. Huu ni wakati ambao hufikiri sawasawa na hivyo inawezekana ukaongea kitu ambacho utakuja kujijutia baadaye. Wengi wanaoshindwa kujizuia wakati wakiwa na hisia, wamekuwa wakiishia kuongea maneno ambayo baadaye wanayajutia.

Unapoongea, jua kwamba unarekodiwa, jua kwamba kile unachoongea hakitosahaulika kamwe, na hivyo usiwe na haraka, utaongea muda wowote utakao, ukikimbilia kuongea utaongea yasiyo sahihi na huwezi kukimbilia kuyafuta au kuyarudisha.

Unapoongea, kuwa kama unaandika agano, au wosia au sheria, kwamba kadiri maneno yanavyokuwa machache, ndivyo inavyopunguza mkanganyiko. Sema machache na sema yale muhimu tu.

Wakati mwingine kukaa kimya ni jambo muhimu zaidi kwako, siyo lazima uchangie kila kitu, siyo lazima ujibu kila kitu. Kadiri unavyoongea sana ndivyo inavyokuwa rahisi kuongea kitu cha kijinga. Na pia unapoongea sana unazoeleka na watu wanaacha kuyapa uzito maneno yako, hasa pale unapoongelea kila kitu, mpaka vitu vya hovyo.

SOMA; Kama Huna Muda Sasa, Hutakuwa Na Muda Baadaye…

Mdomo ni wako, akili ni yako na maneno ni yako, lakini huwezi kuyatoa unavyojisikia wewe mwenyewe. Jua maneno hayo yanawaendea watu na watu ni viumbe wa hisia. Kuwa makini sana na maneno unayoyatoa, huwezi kuyarudisha tena na pia huwezi kuyafuta.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.