UKURASA WA 828; Hakuna Mkono Wa Mtu….

By | April 7, 2017

Mara nyingi kuna vitu ambavyo tunavitaka, tunakazana sana kuweka juhudi ili kuvipata, na tunaona kila dalili kwamba tunakwenda kuvipata, ila ghafla mambo yanabadilika na tunakosa tulichotaka. Pamoja na juhudi zote tulizoweka, pamoja na kufanya kila tulichopaswa kufanya, lakini tunashindwa kupata tulichotaka.

IMG-20170218-WA0000

Ni rahisi kwenye nyakati kama hizi kufikiri kwamba kuna mkono wa mtu. Kwamba yupo mtu ambaye amefanya jambo lililopelekea sisi kukosa tulichokuwa tunafanyia kazi kwa juhudi zote. Kwa asilimia kubwa hizi ni hisia zetu wenyewe kwa sababu tunapenda kupata sababu ya kila kitu, na tukikosa sababu tunatengeneza za kwetu wenyewe.

Ndiyo utakuja na sababu, “…ona hata alivyokuwa ananiangalia…”, na sababu nyingine za aina hiyo.

Ukweli ni kwamba, mara nyingi hakuna mkono wowote wa mtu, hata wale tunaowadhania sana kama wamechangia sisi kukosa, wala hata hawahusiki. Labda ni kweli walikuwa na wivu kuhusu sisi kupata, labda kweli hawakufurahia, lakini hayo hayamaanishi wao ndiyo wamesababisha sisi kukosa kile tulichotaka.

SOMA; Hakuna Siri…

Kuna mahali sisi wenyewe tunakuwa tumekosea na kutoa fursa ya kushindwa. Kuna kitu tunakuwa tumefanya au hatukufanya ambacho kimepelekea tukose kile tunachotaka. Na hata kama wengine ndiyo walioonesha hilo, bado haiondoi ukweli kwamba sisi tumechangia kwenye kushindwa kwetu.

Hivyo ninachotaka wewe rafiki yangu utoke nacho hapa leo hii ni hiki, kwa chochote utakachoshindwa au utakachokosa, usiwe kama wengi ambao wanakimbilia kuangalia kuna mkono wa nani. Bali angalia mkono wako mwenyewe umeingiaje pale. Ni kipi ambacho hukuzingatia na kimepelekea pawepo na nafasi ya wewe kushindwa au kukosa.

Kwa njia hii utajipanga vizuri zaidi na utaweza kufanya vizuri wakati mwingine. Lakini ukikimbilia kuangalia mkono wa nani umehusika, utaishia kugombana na watu na mwishowe hutapata ulichotaka. Wewe fanyia kazi kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako, hayo mengine achana nayo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.