UKURASA WA 835; Kudanganya Na Kutosema Ukweli Wote…

By | April 14, 2017

Kudanganya au kusema uongo ni tabia ambayo haiendani na mafanikio. Hii ni kwa sababu unapodanganya, watu wanakosa uaminifu na wewe na hivyo kushindwa kushirikiana na wewe. Mafanikio yanahitaji sana uaminifu na uadilifu, hivyo kuonekana tofauti na hivyo ni kujiondoa kwenye njia ya mafanikio.

IMG-20170316-WA0010

Lakini pia huwezi kusema ukweli mara zote, na kwa kila jambo. Kuna mambo ambayo hupaswi kuyasema au kuyaeleza yote kama yalivyo. Lakini pia huwezi kuyadanganya kwa sababu siku itafika na watu wataujua ukweli na wewe utaonekana mwongo.

Kwa mambo kama hayo, ambayo kusema ukweli wote kama ulivyo kwa wakati huo unaweza kuumiza zaidi ya kusaidia, husemi ukweli wote. Hapa unaeleza ukweli kwa kiasi ambacho utasaidia kwenye swala husika, halafu unaishia hapo. Husemi uongo kwa namna yoyote ile, ila kuna maelezo huyatoi kwa wakati husika kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kuharibu zaidi.

SOMA; Ni Nani Huyo Alikudanganya?

Kuna mstari mwembamba sana kati ya kusema uongo na kutokutoa ukweli wote, hivyo unahitaji umakini sana usivuke mstari huo. Unahitaji uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kuweza kuchuja kipi cha kusema na kipi cha kuacha kwa sasa. Kama tayari unayo tabia ya uongo, unaweza kusema uongo huku ukijidanganya kwamba hudanganyi ila husemi ukweli wote.

Nakushirikisha hili ila litumie kwa makini sana, na isiwe kwa maslahi yako binafsi ila kwa maslahi ya wengi. Katika nyakati kama hizo ambapo ukweli wote unaweza kuumiza kuliko kusaidia, toa ukweli kwa kiasi, na kadiri inavyoruhusu endelea kutoa ukweli.

Kama kweli kwa kufanya hivyo kutawasaidia watu, watu watakuelewa na kukushukuru. Lakini kama kufanya hivyo husaidii watu bali unajinufaisha wewe, watu watachukia na kukuona wewe ni mtu usiyefaa.

Mstari ni mwembamba sana, hata hauonekani, hivyo kuwa makini.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.