UKURASA WA 844; Hakuna Hali Ya Kudumu….

By | April 23, 2017

Tunapopita katika matatizo na changamoto, ni rahisi sana kusahau kwamba hakuna hali inayodumu kwenye maisha yetu, ni rahisi kuamini kwamba mambo yatakuwa hivyo na yatazidi kuwa mabaya zaidi kadiri siku zinavyokwenda. Lakini huo siyo uhalisia, sheria za asili haziruhusu jambo lolote kudumu milele.

IMG-20170314-WA0002

Ndiyo maana hata jua liwe kali kiasi gani, halitawaka masaa 24, kuna muda litaondoka na tutaweza kufanya mambo mengine. Hata mvua ziwe nyingi kiasi gani, masika hayatauwepo mwaka mzima, itakuja misimu mingine katika mwaka. Na hata ukame uwe mkubwa kiasi gani, hautadumu milele, itapita hata mvua kidogo kuotesha hata nyasi kidogo.

Hivyo pia kwa maisha yako binafsi, tukianza na uhai wako, hutaishi milele, ipo siku utakufa. Kadhalika kwenye matatizo na changamoto zako, hazitadumu milele, kuna wakati zinapita. Hivyo unapokuwa kwenye changamoto, usikate tamaa, endelea kuweka juhudi ambazo unapaswa kuweka ili kupata kile ambacho unataka kupata. Kwa juhudi zako utaweza kuzishinda changamoto zako, na kama hutaweza basi muda utakusaidia kumaliza changamoto hizo.

SOMA; Haijalishi Hali Ya Uchumi Ikoje, Fursa Za Kutengeneza Fedha Bado Ni Nyingi…

Hakuna hali yoyote ya kudumu kwenye maisha yako, labda wewe mwenyewe uamue iwe hivyo, na ukiamua maana yake umechagua kudumu na hali ya chini. Kama umasikini, hofu na vingine ambavyo unaweza kujijengea wewe binafsi.

Haijalishi mambo ni magumu kiasi gani, kumbuka hayatadumu milele, na hata kama yakichelewa sana, basi wewe binafsi hutadumu milele. Hivyo endelea kuweka juhudi, na endelea kuifanyia kazi ndoto kubwa ya maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.