UKURASA WA 889; Siyo Mara Moja….

By | June 7, 2017

Tone la maji linaweza kutoboa mwamba mgumu au hata chuma.

Lakini siyo tone moja pekee, bali matone yanayojirudia rudia bila ya kukoma. Kama kuna mwamba, na kila wakati kuna tone moja la maji linaudondokea, baada ya muda mwamba ule utavunjika kabisa. Kilichouvunja siyo nguvu ya tone la maji, bali kujirudia rudia kwa tone lile la maji.

Wapo watu wamekuwa wanafikiri kipo kitu kimoja tu ambacho wakiweza kukifanya basi mafanikio yao ni uhakika. Hivyo wanapoteza muda wao kuruka ruka na vitu vya kufanya. Wanajaribu hichi wanaona hakiwapi wanachotaka, wanatoka na kujaribu kingine. Wanafanya hivyo kwa muda mrefu mpaka wanapokuja kugundua wanachotafuta hakipo.

Mafanikio ya kweli yanapatikana kwenye kitu kimoja ambacho mtu amekifanya kwa kurudia rudia muda mrefu. Amefanya kila siku, amefanya kila mara na muda wote, mawazo yake yapo kwenye kitu kile. Hapa ndipo inapotengenezwa nguvu moja kubwa sana inayoweza kuvunja vikwazo na changamoto zozote zinazojitokeza kwenye safari ya mtu huyo.

SOMA; Usichanganye Falsafa, Chagua Moja Na Itumie Vizuri.

Usidanganyike kwamba kipo kitu ukifanya mara moja tu basi usubiri mafanikio. Jua unapaswa kuweka juhudi kila siku na kila mara. Na hata wakati unafanya hivyo, bado unaweza usipate unachotaka. Kwa haraka.

Unahitaji kuwa na uvumilivu, kwa sababu inachukua muda. Unahitaji kuwa na msimamo kwa sababu ni kile unachofanya kwa kurudia rudia ndiyo kinakuletea manufaa. Halafu sasa chagua unafanya nini, kisha kifanye. Usijaribu, fanya. Usiishie njiani nenda njia nzima. Na usitegemee matokeo makubwa haraka, wewe fanya.

Kwa hakika utaweza kufanya makubwa kwa njia hii.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.