UKURASA WA 899; Endesha Maisha Yako Kama Biashara….

By | June 17, 2017

Msingi mkuu wa biashara ni huu; FAIDA = MAUZO – MANUNUZI NA MATUMIZI.

Biashara inapata faida, na hivyo kuendelea pale inapotengeneza faida, na faida inapatikana pale mauzo yanapokuwa makubwa kuliko manunuzi na gharama za biashara.

Kadhalika kwenye maisha yako, ili uweze kuwa na maisha bora yenye uhuru wa kifedha, mapato yako lazima yawe zaidi ya matumizi. Huu ni msingi muhimu sana kifedha, kwa sababu sina haja ya kukukumbusha kwamba fedha ni muhimu sana kwenye maisha ya kila siku.

Sasa ninaposema uendeshe maisha kama biashara siishii tu kwenye kusema mapato ni zaidi ya matumizi, badala yake unahitaji kuna na hesabu zako za mapato na matumizi.

Lazima uwe na bajeti ambayo inaonesha vyanzo vyako vya mapato na kiasi unachopata kwa kila mwaka. Na pia lazima uwe na mipango ya matumizi. Kwa sababu matumizi ya msingi ni yale yale, hivyo unaweza kuyapangilia vizuri.

SOMA; Dawa Ya Msongo Wa Mawazo Ni Hii.

Ukipanga vitu hivi kabla hata hujaanza kipindi chako cha bajeti, labda mwezi au mwaka, inakupa ukomo wa matumizi na uelewa wa kipato chako. Kwa njia hii utajua ni wakati gani unavuka mstari wa matumizi kuzidi mapato.

Watu wengi hawana mpango wowote wa mapato wala matumizi, hivyo kinachotokea ni wakipata fedha wanatumia mpaka iishe, halafu wanakopa. Hii inawaweka kwenye hali ya madeni na utumwa wa kifedha.

Yaendeshe maisha yako kama biashara, panga na simamia mzunguko wako wa fedha.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.