Author Archives: Makirita Amani

About Makirita Amani

Makirita Amani ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1848; Hamasa Ya Nje Na Ndani…

By | January 22, 2020

Njiti ndogo ya kiberiti inawasha moto mkubwa ambao unaweza kupika au kuunguza kitu kikubwa. Je unafikiri kilichopika au kuunguza ni njiti ile ya kibiriti? Najua unajua siyo. Kama ingekuwa hivyo, tungetegemea njiti hiyo ya kiberiti iweze kuunguza maji ukiyawasha, au kuunguza mchanga ukiuwasha kama unayowasha kuni au mafuta. Sababu inayopelekea (more…)

#TAFAKARI YA USIKU; SIYO WEWE UNAYEAMUA KESHO YAKO…

By | January 20, 2020

“People do not decide their futures, they decide their habits and their habits decide their futures.” – F.M. Alexander Huwa tunajiambia na kuamini kwamba sisi ndiyo waamuzi wa kesho yetu. Lakini huo siyo uhalisia, siyo sisi ambao tunaamua kesho yetu, bali ni tabia zetu ndiyo zinaamua kesho hiyo. Ukijijengea tabia (more…)

1846; Tatizo Na Fedha…

By | January 20, 2020

Fedha siyo kila kitu, lakini inahusika karibu kwenye kila kitu kwenye maisha yetu, hivyo kujitenga na fedha ni vigumu sana, hasa kwa maisha ambayo tumeshayazoea. Kitu ambacho kinatupeleka kwenye msingi muhimu wa kuzingatia inapokuja kwenye matatizo na fedha. Kama una tatizo ambazo fedha inaweza kutatua basi huna tatizo, bali tatizo (more…)

1845; Ukishaamua, Ukishaahidi…

By | January 19, 2020

Kinachofuata ni kutekeleza, kama ulivyoamua na kama ulivyoahidi. Usianze kutafuta sababu za kwa nini huwezi kufanya ulichoamua au kwa nini huwezi kutekeleza ulichoahidi. Ni wewe mwenyewe uliyefanya maamuzi hayo, ni wewe mwenyewe uliyeahidi, jiheshimu na tekeleza. Zama tunazoishi sasa ni za watu laini, watu ambao wanafanya maamuzi lakini hawayatekelezi, wanaahidi (more…)