Author Archives: Makirita Amani

About Makirita Amani

Makirita Amani ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1844; Uwekezaji Ulioufanya Kwenye Mafanikio Yako…

By | January 18, 2020

Huwezi kwenda kwenye shamba, ukapanda mbegu halafu ukaondoka na kusubiri kuja kuvuna. Asili haifanyi kazi hivyo, ni lazima ufanye uwekezaji mkubwa kwenye shamba hilo kama unataka kupata mazao mengi na mazuri. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio yako, huwezi kusema unataka kufanikiwa, ukajiwekea maono na malengo yako ya mafanikio halafu (more…)

1843; Unapokuwa Huna Uhakika Ufanye Nini…

By | January 17, 2020

Kila mtu kuna wakati huwa anajikuta njia panda, anakosa uhakika wa kitu gani afanye. Unajikuta una machaguo mengi na hujui kipi ni sahihi kwako kufanya. Huu ndiyo wakati ambapo wengi hupoteza muda wakifikiria kipi sahihi kwao kufanya. Wengi hukimbilia kujifunza zaidi, kufanya tafiti zaidi, kuomba ushauri kwa wengi zaidi. Lakini (more…)

1842; Acha Kujidanganya, Huwezi Kupata Muda…

By | January 16, 2020

Muda huwa haupatikani, bali muda unatengenezwa. Ukijiambia kwamba ukipata muda utafanya kitu fulani, unajidanganya. Kwa sababu huwezi kupata muda, bali unaweza kutengeneza muda. Wote tunajua jinsi ambavyo mambo ya kufanya ni mengi na muda wa kuyafanya ni mchache. Hivyo kufikiri kuna siku muda utajitokeza wenyewe, ni kujifariji tu. Utapata muda (more…)