Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Jukumu Kuu La Masoko Ni Kuwafanya Watu Wazungumzie Biashara Yako…

By | September 30, 2018

Watu wanaotafuta ‘kiki’ ili wawe kwenye maneno ya watu, wanatumia njia sahihi ya masoko, lakini kwa namna ambayo ni mbaya. Jukumu kuu la masoko ni kuwafanya watu wazungumzie biashara yako au huduma unayotoa. Pale watu wanapokuzungumzia, ndiyo wengi zaidi wanakujua na wao wanatamani kuja kupata huduma ambayo wengine wamepata na (more…)

BIASHARA LEO; Kusema Hapana Kwa Fursa Nzuri…

By | September 29, 2018

Kitu kimoja ambacho kinapelekea baadhi ya biashara zinazoanza vizuri na kukua kisha zinaanguka vibaya, ni wafanyabiashara kushindwa kusema hapana kwa fursa nzuri zinazojitokeza mbele yao. Iko hivi, unaanza biashara ukiwa na maono fulani kwenye akili yako. Unataka biashara yako iwe ya aina fulani, iwasaidie watu wa aina fulani na ikupe (more…)

BIASHARA LEO; Wingi Wa Wateja Na Ubora Wa Wateja…

By | September 28, 2018

Wafanyabiashara wengi huwa wanafurahi sana pale wanapokuwa na wateja wengi. Kwa sababu wanaamini wingi wa wateja ndiyo mafanikio ya biashara. Na huwa hawaelewi pale wanapokuwa na wateja wengi lakini biashara inakufa, hapo ndipo wanaamini kwamba kuna chuma ulete. Haiwezekani wauze kwa wateja wengi halafu biashara isipate faida. Ipo kampuni moja (more…)

BIASHARA LEO; Usiajiri Watu Wanaotaka Kazi, Ajiri Watu Wanaotaka Hiki…

By | September 27, 2018

Changamoto nyingi zinazotokana na kuajiri kwenye biashara, zinatokana na watu wanaotafuta kazi ya kufanya. Watu ambao wanakuambia wanaweza kufanya kazi yoyote na wanaoangalia ni nini wanalipwa pekee. Hawa ni watu ambao unaweza kuwapata kirahisi sana, unaweza kuwalipa rahisi pia, lakini pia utawapoteza kirahisi na kazi yoyote wanayoiweka inakuwa ya urahisi, (more…)

BIASHARA LEO; Bishara Unayofanya Leo, Siyo Biashara Utakayofanya Kesho…

By | September 26, 2018

Unapaswa kuifanya biashara yako vizuri sana leo, Na wakati huo huo kujiandaa na mabadiliko yanayoendelea kutokea kwenye biashara yako. Kwa sababu biashara unayofanya leo, siyo biashara utakayofanya kesho, mwaka ujao, miaka 5 ijayo na hata miaka 10 ijayo. Mambo yanabadilika, watu wanabadilika na mahitaji yao yanabadilika pia. Watu wanataka vitu (more…)

BIASHARA LEO; Uza Kitu Ambacho Unapata Shida Ya Kukipata…

By | September 25, 2018

Kama unajiambia unataka kuingia kwenye biashara lakini hujui biashara gani ufanye, nina ushauri mmoja mzuri sana kwako. Uza kitu ambacho unapata shida ya kukipata. Najua kwenye maisha yako kuna vitu unatafuta, ambavyo umekuwa hupati au hata ukipata siyo kwa namna ambavyo ulitaka kupata. Habari njema ni kwamba, siyo wewe mwenyewe (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Hajali Kuhusu Ushindani Wako Na Wafanyabiashara Wengine…

By | September 24, 2018

Kama kila biashara ingeweka rasilimali zake kwenye kuwahudumia vizuri wateja wake, biashara zingefanikiwa sana. Lakini biashara nyingi zimekuwa zinatafuta njia za mkato za kupata wateja, na moja ya njia hizo ni kuwaangusha washindani wao wa kibiashara. Kama una washindani wa kibiashara, jambo jema kabisa unaloweza kufanya kwa ajili yako ni (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Aliyekulazimisha Uje Kununua Hapa, Umekuja Mwenyewe…

By | September 23, 2018

Fikiria umeenda kwenye biashara, una shida ya kitu fulani, umeoneshwa kile pale, bei yake kiasi fulani. Unataka kujua zaidi kama kitakusaidia, muuzaji anakuambia hebu usinisumbue, kama unataka chukua kama hutaki acha. Utajisikiaje? Najua utajisikia vibaya sana, na kwa kuwa sasa hivi wauzaji wa chochote unachotaka ni wengi, basi utaenda kwa (more…)

BIASHARA LEO; Fasheni Zinapita, Biashara Yako Ni Ya Kudumu…

By | September 22, 2018

Kama umechagua kuingia kwenye biashara, basi biashara yoyote unayochagua kufanya, angalia miaka mingi ijayo. Angalia miaka mitano ijayo, miaka kumi ijayo na hata miaka 50 ijayo. Je biashara hiyo itakuwepo na je itakuwa imekua zaidi kuliko sasa? Nakuambia hivi kwa sababu kuna uwekezaji mkubwa utakaouweka mwanzo wa biashara yako, uwekezaji (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kuondoa Ukomo Wa Kipato Kwenye Biashara Yako.

By | September 21, 2018

Watu wengi wanapoanza biashara, wanaona ukuaji wa kipato, ambao unawaridhisha sana na kuwapa hamasa ya kuweka juhudi zaidi. Wanaweka juhudi na kipato kinaongezeka zaidi, wanazidi kufurahi na kupata hamasa pia. Wanaongeza tena juhudi na muda wa kazi, na kipato kinaongezeka. Hapo wanajifunza kwamba ukiongeza juhudi na muda, basi kipato kinaongezeka. (more…)