Category Archives: UWEKEZAJI LEO

UWEKEZAJI LEO; Maana Ya Gawio Katika Uwekezaji Na Utolewaji Wake.

By | October 19, 2017

Kampuni au taasisi ambayo inauza hisa zake kwenye soko la hisa, inapaswa kutoa hesabu zake za mwaka kila mwaka. Katika hesabu hizi kampuni itaonesha mapato, matumizi, faida na hata hasara. Iwapo kampuni imepata faida mwisho wa mwaka wa fedha, faida ile inapaswa kurudi kwa wanahisa wa kampuni hiyo. Ile sehemu (more…)

UWEKEZAJI LEO; Ongezeko La Thamani Ya Mtaji Katika Uwekezaji.

By | October 17, 2017

Ukinunua kiwanja leo kwa shilingi milioni moja, halafu baada ya mwaka mmoja ukauza kiwanja hicho kwa shilingi milioni mbili, kuna ongezeko la thamani la mtaji ulioweka. Wewe uliweka mtaji ambao ni shilingi milioni moja, lakini baada ya mwaka mtaji huo umekua na kufikia milioni mbili. Ongezeko la thamani ya mtaji (more…)

UWEKEZAJI LEO; Kwenye Uwekezaji Waepuke Watu Wa Aina Hii…

By | October 12, 2017

Watu wengi wamekuwa wakipata hasara kwenye uwekezaji kwa sababu hawatumii akili zao kutafuta maarifa sahihi na kufanya maamuzi sahihi. Badala yake wamekuwa wakitegemea wengine wawafanyie hivyo. Wamekuwa wakisubiri wengine wawaambie nunua hisa hizi, utapata faida kubwa na kadhalika. Wengi wanabeba ushauri huo kama ulivyo, wananunua hisa fulani, au kuwekeza eneo (more…)

UWEKEZAJI LEO; Faida Za Mpango Wa Pamoja Wa Uwekezaji Na Jinsi Ya Kushiriki Kwenye Mpango Wa Aina Hii.

By | October 10, 2017

Kwenye masoko ya mitaji tumekuwa tunajifunza amana za aina mbili, hisa na hatifungani. Katika uwekezaji kwenye amana hizi, mwekezaji anaweza kuchagua yeye mwenyewe anunue hisa na hatifungani zipi. Lakini hili linamtaka awe mfuatiliaji wa karibu wa hisa na siko la hisa kwa ujumla. Wakati mwingine kuchagua hisa zipi nzuri kununua (more…)

UWEKEZAJI LEO; Tofauti Ya Mbahatisha Hisa Na Mlanguzi Hisa Kwenye Uwekezaji.

By | October 6, 2017

Katika uwekezaji kwenye hisa, kuna nyakati mbili ambazo wawekezaji huweza kutengeneza faida kubwa au kupata hasara kubwa. Nyakati hizi zimekuwa zikisoma uelekeo wa soko na watu kuchukua hatua ambazo zinawanufaisha au kuwapa hasara. Nyakati hizo mbili ni kama ifuatavyo; Mbahatisha hisa (BEAR MARKET). Hii ni hali inayotokea pale bei ya (more…)

UWEKEZAJI LEO; Vodacom Wametangaza Kutoa Gawio La Kwanza Kwa Wawekezaji.

By | October 4, 2017

Moja ya faida za kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa ni kupata gawio pale kampuni inapopata faida. Kampuni inawalipa wanahisa wake sehemu ya faidia iliyopata, huku wakiendelea kubaki na hisa zao. Yaani ni sawa na kuweka mtaji kwenye biashara, na ukapata faida huku mtaji wako ukiendelea kuwepo. Kampuni ya Vodacom Tanzania, (more…)

UWEKEZAJI LEO; Faida Tano Za Kuwekeza Kwenye Hatifungani.

By | October 2, 2017

Moja ya uwekezaji kwenye masoko ya mitaji ni kununua hatifungani, ambapo unaikopesha fedha kampuni au taasisi kwa makubaliano ya kulipwa kwa riba. Watu wengi wamekuwa hawaelewi vizuri uwekezaji huu wa hatifungani, kwa sababu hauongelewi sana na kwa hapa Tanzania, hatifungani zinazopatikana sokoni siyo nyingi kama hisa. Leo nakwenda kukushirikisha faida (more…)

UWEKEZAJI LEO; Dalali Wa Soko La Hisa Ni Mtu Wa Aina Gani Na Jinsi Ya Kuchagua Dalali Mzuri.

By | September 28, 2017

Wengi wetu tunaposikia neno dalali tunajua ni mtu ambaye anafanya biashara ya kuuza vitu vya wengine, kwa kuongeza bei ili apate fedha. Kwa fikra hizi tuna mtazamo mbaya kuhusu madalali na kuona ni watu wanaolangua wengine. Hivyo tunaposikia tena kwenye soko la hisa kuna madalali, tunastuka na kukosa amani. Tunajiuliza (more…)

UWEKEZAJI LEO; Aina Kuu Mbili Za Soko La Hisa.

By | September 26, 2017

Soko la hisa limegawanyika kwenye aina kuu mbili, kulingana na hisa zinazouzwa sokoni. Aina ya kwanza ni soko la awali (primary market). Hili ni soko la hisa ambapo hisa ndiyo zinaingia sokoni kwa mara ya kwanza. Hapa kampuni au taasisi inakuwa ndiyo inaandikisha hisa zake kwenye soko la hisa. Katika (more…)

UWEKEZAJI LEO; Faida Tano Za Kununua Na Kuwekeza Kwenye Hisa.

By | September 21, 2017

Watu wengi wamekuwa wakiona uwekezaji kwenye ununuzi wa hisa na amana nyingine kama aina ngumu ya uwekezaji, ambayo inaweza kufanywa na watu wenye fedha nyingi na wenye elimu kubwa. Yote hayo ni uongo, kila mtu anaweza kuwekeza kwenye hisa, hata mwenye kipato kidogo na asiye na elimu kubwa. Uwekezaji kwenye (more…)