Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

2007; Fursa Iliyokuwa Inakusubiri Wewe…

By | June 29, 2020

Ukiona watu wanakuna kwako na fursa, wanakuonesha fursa inayokufaa sana na kukushawishi ujiunge na fursa hiyo la sivyo utaikosa basi kuwa na uhakika kwenye jambo hili, wewe ni fursa kwa watu hao. Kama wanachokuambia ni fursa kweli, unafikiri ingekaa muda wote ikusubiri wewe? Unafikiri hao wanaokusisitiza ni fursa wangepoteza muda (more…)

2006; Uhuru Ni Kujitambua…

By | June 28, 2020

Mtoto mdogo akitaka kitu anakitaka kama anavyotaka yeye, hawezi kukubali kitu kingine isipokuwa kile anachotaka yeye. Kupata kile anachotaka anaweza kufikiri ni uhuru, lakini huo siyo uhuru. Uhuru siyo kupata kile ambacho mtu anataka kwa namna anayotaka yeye. Huko ni kuendeshwa na hisia au mihemko na siyo kuwa huru. Uhuru (more…)

2004; Dakika Kumi Zinaweza Kufanya Nini?

By | June 26, 2020

Kitu kimoja ninachokiamini, na nitaendelea kuamini hivyo maisha yangu yote ni kwamba wale wanaosema hawana muda wa kufanya vitu fulani wanavyotaka kufanya huwa wanadanganya. Siyo kweli kwamba hawana muda, ila tu hawataki kufanya, sasa kwa kuwa hawataki kuukabili ukweli, wanatumia kisingizio cha muda. Kwenye siku kuna masaa 24 ambayo ukiyageuza (more…)

2003; Tatizo Siyo Kipaji…

By | June 25, 2020

Wakati tunasoma, somo la hisabati lilikuwa linaonekana ni somo gumu kwa wanafunzi walio wengi. Hivyo wale ambao walikuwa wanaliweza somo hilo walionekana kuwa na kipaji. Kulikuwa na kauli kabisa kwamba ‘hesabu ni kipaji’ Kwenye mafanikio pia, wapo wengi wanaoamini kwamba mafanikio yanahitaji mtu uwe na kipaji fulani. Na hapo wanatumia (more…)

2002; Mchezo Lazima Uendelee…

By | June 24, 2020

Hakuna mtu ambaye kila kitu kinaenda kama alivyopanga kwenye maisha yake. Lakini wapo watu wanaoendelea kufanikiwa licha ya kukutana na vikwazo vingi, huku wengine wakishindwa kwa vikwazo hivyo hivyo. Wale wanaofanikiwa ni wenye mtazamo wa kutoruhusu chochote kiwe kikwazo kwa safari yao. Wanachukulia safari ya mafanikio kama mchezo au onesho (more…)

1999; Hushtuki Tu…

By | June 21, 2020

Ulipata kazi ya kwanza, ikawa hailipi vizuri, ukaicha. Ukapata nyingine, bosi akawa anakunyanyasa, ukaiacha pia. Ukapata nyingine, hiyo ukawa huelewi na wafanyakazi wengine, nayo ukaiacha pia. Na bado unalalamika kwamba hupati kazi nzuri. Hushtuki tu? Umepata mwenza wa kwanza, tabia mkawa hamuendani, mkaachana, ukapata wa pili, tena mkashindwa kuelewana, ukapata (more…)