Category Archives: #TUVUKE PAMOJA

#TuvukePamoja; TAFUTA ENEO LA KUHODHI.

By | May 26, 2020

Katika changamoto kubwa ya kiuchumi tunayopitia ambayo imesababishwa na mlipuko wa vizuri vya Corona, biashara nyingi zinakufa na kazi zinapotea. Wengi wanafunga biashara zao na hawatakuja kuzifungua tena, Wengi pia wanapunguzwa kazi na hawatakuja kupata kazi hizo tena. Ni hali ambayo inawashtua wengi, kwa kuwa hakuna aliyeitegemea, maana kila kitu (more…)

#TuvukePamoja; UWEKEZAJI SAHIHI KWAKO KUFANYA…

By | May 24, 2020

Katika kipindi hiki tunachopitia changamoto kubwa, uwekezaji sahihi kwako kufanya ni kuwekeza ndani yako binafsi. Changamoto kama hizi zinatuonesha ni wapi tuna udhaifu na mapungufu, zinatuonesha nini tumekuwa tunafanya kwa mazoea. Hivyo ni wakati sahihi kwako kufanya uwekezaji wa kuwa bora zaidi kwenye yale maeneo ambayo una udhaifu na mapungufu. (more…)

#TuvukePamoja; MUDA WA UPWEKE NA UTULIVU

By | May 21, 2020

Kwenye changamoto tunayopitia na hata nyingine nyingi, Ni rahisi sana kila wakati kuwa imetingwa na mambo mbalimbali. Yaweza kuwa kazi zako mwenyewe, Inaweza kuwa taarifa mbalimbali za yale yanayoendelea, Au kwa kuwa na muda mwingi, unajikuta unamaliza wote kwa kuzurura mitandaoni au kuangalia tamthilia na maigizo mbalimbali. Kitu ambacho tunakikwepa (more…)

#TuvukePamoja; UTARATIBU WA KUIENDESHA SIKU (ROUTINE)

By | May 19, 2020

Katika wakati huu ambao tunapitia changamoto kubwa, kila mmoja anahitaji mfumo bora wa kuendesha maisha yake. Mfumo ambao hautakwamishwa na chochote kile. Moja ya vitu vitakavyokusaidia sana kwenye kuziishi siku zako vizuri, Ni kutengeneza utaratibu wa siku yako ambao utauishi kila siku. Utaratibu huo unaitwa ROUTINE. Hapa unapangilia jinsi ambavyo (more…)

#TuvukePamoja; EPUKA HALI HASI…

By | May 18, 2020

Kwa kile tunachopitia sasa, jukumu kubwa ulilonalo ni kuepuka kabisa hali yoyote ambayo ni hasi. Kama kuna watu ukiongea au kuwasiliana nao wanaongea mambo hasi na kulalamika jinsi mambo yalivyo magumu, acha mara moja kuongea au kuwasiliana nao. Kama kuna vyombo vya habari au vipindi ambavyo ukifuatilia unakutana na taarifa (more…)

#TuvukePamoja; SHUKRANI.

By | May 16, 2020

Haijalishi unapitia nini, kuna kitu cha kushukuru. Unaposhukuru, unaangalia upande chanya wa maisha yako. Na kwa kuwa akili zetu hutuonesha kile tunachofikiria, Unapokuwa mtu wa shukrani, mambo mazuri zaidi yanakuja kwako. Katika kipindi hiki tunachopitia changamoto, kuwana kijitabu (diary) na kiite kitabu cha shukrani. Kisha kila siku andika yale unayoshukuru (more…)

#TuvukePamoja; CHAGUA KITU UTAKACHOKIFANYA KILA SIKU…

By | May 15, 2020

Katika changamoto hii ya covid 19 tunayopitia sasa, ni rahisi sana kuona mambo hayawezekani. Hilo linapelekea kukata tamaa na kukosa nguvu ya kuendelea na mapambano. Hivyo hicho ni kitu cha kwanza cha kupambana nacho, kuhakikisha kila siku unayo hamasa na nguvu kubwa ya kuendelea na mapambano, bila ya kujali matokeo (more…)

#TuvukePamoja; Maisha na covid 19.

By | May 14, 2020

Kama ambavyo nimekuwa nashirikisha mara kwa mara, na kama ambavyo taarifa mpya zinaonesha, ugonjwa huu wa covid 19 utachukua muda kuondoka. Na mategemeo ya kuondoka kwa ugonjwa huu ni pale dawa au chanjo itakapopatikana, kitu ambacho kinakadiriwa kuchukua siyo chini ya miezi 18. Hivyo tunapaswa kujifunza kuendelea na maisha katika (more…)