Category Archives: SIKU 30 ZA MAFANIKIO

SIKU YA 21; Sheria Za Asili Zitakazokuletea Utajiri Na Mafanikio.

By | September 21, 2014

Ni muhimu kukumbuka kwamba watu wote waliofikia mafanikio makubwa walikuwa wamejitoa kweli kwa ajili ya kufikia mafanikio. Waliamini bila kuyumbishwa kwamba dunia imejaa utajiri na kinachohitajika ni wewe kuwa na ufunguo wa siri wa kufungua milango itakayokuletea mafanikio. Leo tutajifunza sheria za asili ambazo zinaweza kukuletea mafanikio na utajiri mkubwa. (more…)

SIKU YA 20; Siri Saba Zinazotumiwa Na Watu Wenye Mafanikio Makubwa.

By | September 20, 2014

Katika tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa watu matajiri na wenye mafanikio makubwa imeonekana kwamba karibu kila mmoja ambaye amefikia mafanikio makubwa ametumia siri saba kufikia mafanikio hayo. Leo tutajifunza siri hizo saba na kama ukianza kuzitumia hakuna kitakachoweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa. 1. Malengo na maono makubwa. Watu wote waliofanikiwa walikuwa (more…)

SIKU YA 19; Tumia Fomula Hii Ya Mafanikio Na Utajiri.

By | September 19, 2014

Kuna njia nyingi za kupata mafanikio makubwa kwenye maisha. Mafanikio yanaweza kupatikana na yeyote ambaye anatumia njia zilizothibitishwa za kuweza kufikia mafanikio makubwa. Ni lazima mawazo yanayoingia kwenye akili yako yawe ya kitajiri ndio uweze kufikia utajiri. Kumbuka duniani kuna rasilimali nyingi sana za kumfanya kila mtu kuweza kufikia mafanikio (more…)

SIKU YA 18; Jinsi Ya Kuweka Malengo Ya Faida.

By | September 18, 2014

Katika sehemu hii tutajifunza mambo mawili muhimu; 1. Jinsi ya kuweka malengo ya fedha kwenye maisha. 2. Jinsi ya kuendeleza ujuzi ulionao ili kufikia malengo yako ya kifedha. Kuweka malengo yako ya kifedha. Kuna malengo manne ya kifedha unayoweza kujiwekea. Malengo hayo ni; 1. Malengo ya kipato. Haya ni malengo (more…)

SIKU YA 17; Jinsi Tengeneza Bahati Yako Mwenyewe

By | September 17, 2014

Mamilioni ya watu wanaenda na maisha bila ya kujua yanawapeleka wapi. Watu hawa wanafanya kile ambacho kinafanywa na kila mtu au kinachoonekana ni cha kawaida kufanya. Hawa ni watu ambao wanaamini kuna bahati na wao hawajapata bahati hiyo ndio maana maisha yao hayajawa vizuri. Sasa wewe ondoka kwenye kundi hili (more…)

SIKU YA 16; Jinsi Ya Kushinda Vikwazo Kwenye Maisha Yako.

By | September 16, 2014

Nguvu kubwa ya kufanya na kukamilisha mipango yetu ipo ndani ya akili zetu. Tunajifungia kwenye gereza la akili zetu kwa kufanya yale ambayo tunayafanya kila siku. Hatuiachii akili yetu uhuru wa kutambua na kutumia fursa nyingine ambazo zinapatikana. Tatizo kubwa la wengi wetu, kutokana na woga au kutokujiamini hawaruhusu akili (more…)

SIKU YA 15; Mpango Mzuri Wa Matumizi Ya Muda Wako Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | September 15, 2014

Binadamu tunafanya mambo yetu kama vile tuna muda usioa na kikomo. Ukweli ni kwamba katika vitu ambavyo tunavyo kwa kiwango kidogo sana ni muda. Muda ni zawadi ambayo ipo kwa ukomo. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuongeza hata sekunde moja kwenye siku hata angekuwa na uwezo au fedha nyingi kiasi gani. (more…)

SIKU YA 14; Jinsi Ya Kutengeneza Haiba Inayoendana na Mabadiliko.

By | September 14, 2014

Haiba ya mtu inatokana na tabia na sifa za mtu huyo. Binadamu wote katika vipindi tofauti vya maisha yao hutengeneza tabia mbalimbali za kufikiri, kuhisi na hata kutenda. Baadhi ya tabia hizi hutengenezwa kwa kujua, nyingine hutengenezwa kwa kutokujua. Jumla ya tabia zote alizonazo mtu ndio zinatupatia haiba ya mtu (more…)

SIKU YA 13; Siri Ya Kufanya Maamuzi Yenye Mafanikio.

By | September 13, 2014

Katika maisha yako ya kila siku kuna maamuzi mengi sana ambayo unayafanya. Maamuzi unayoyafanya yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye kufikia mafanikio makubwa. Fikiria maamuzi makubwa mabayo umewahi kufanya kwenye maisha yako. Je ulipitia hatua gani kufanya maamuzi hayo? Je wakati unafanya maamuzi hayo ulikuwa katika hisia gani? Je unafikiri (more…)

SIKU YA 12; Nguvu Za Kufiki Mafanikio.

By | September 12, 2014

Kwa kila hatua utakayochukua kwenye maisha yako itatengeneza nguvu na nguvu hiyo itakusukuma kuelekea kwenye mafanikio au kuelekea kwenye kushindwa. Kuna nguvu za asili ambazo zikitumiwa vizuri zinaleta mafanikio na zikitumiwa vibaya zinasababisha kushindwa. Kuna nguvu nne zinazoweza kukuletea mafanikio kama ukizijua na kuzitumia vizuri. Nguvu ya kwanza ya mafanikio; (more…)