Category Archives: TABIA ZA MAFANIKIO

Njia Nzuri Ya Kusema HAPANA Kistaarabu, Kwa Wale Ambao Hawawezi Kusema Hapana.

By | May 13, 2017

Moja ya tabia zinazotuzuia kufanikiwa, ni tabia yetu ya kusema ndiyo kwenye kila kitu ambacho tunaombwa na wengine. Katika makala ya mambo manne yanayokuzuia kufanikiwa (unaweza kuisoma kwa kubonyeza maandishi haya) nilieleza kwamba hujawa na roho mbaya vya kutosha. Nikikueleza umuhimu wa kusema hapana kwa yale mambo ambayo wengine wanakutaka (more…)

Jinsi Unavyoweza Kuwa Mwaminifu Kwenye Ulimwengu Wa Sasa Uliojaa Kila Aina Ya Hila.

By | May 6, 2017

Msingi wetu mkuu tunaouishi kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA. Hizi ni nguzo tatu muhimu sana kwenye mafanikio ya maisha yetu, kuanzia kwenye kazi, biashara, mahusiano, afya na kila eneo la maisha yetu. Uadilifu unaendana sana na uaminifu, japo siyo kitu kimoja. Uaminifu ni kile unachosema na (more…)

FURSA NDANI YA TATIZO; Mambo Matano(05) Ya Kufanya Pale Unapokuwa Umekwama.

By | May 5, 2017

Waswahili wanasema, mipango siyo matumizi. Wakiwa na maana kwamba unaweza kupanga sana, lakini inapofika kwenye utekeleaji, mambo yanaweza kwenda tofauti na ulivyotegemea. Na kwa uzoefu wangu na wengine ambao nimekuwa nawaangalia, mara nyingi sana mambo huenda tofauti kabisa na mategemeo ambayo watu wanakuwa nayo. Inapofika hali kama hii, wengi hukata (more…)

Mambo Kumi(10) Muhimu Usiyojua Kuhusu Mafanikio, Na Jinsi Yanavyokurudisha Nyuma.

By | July 14, 2015

Najua umeshasoma makala nyingi sana kuhusu mafanikio, makala ambazo zinasema mbinu hizi za mafanikio mbinu zile za mafanikio. Na unapoona makala nyingine tena inayokuambia kuna mambo kumi usiyoyajua kuhusu mafanikio, unaweza usiamini. Lakini twende pamoja na utagundua kwamba mambo haya kumi kuna ambayo huyajui kabisa na kuna ambayo unayajua ila (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati Unajenga Tabia Za Mafanikio.

By | July 7, 2015

Mafanikio ni tabia, vingine vyote ni nyongeza tu.       Unaweza kuiweka kauli hiyo mahali ambapo unaweza kuiona kila siku ili iwe msisitizo kwako kuchukua hatua ya kujijenge atabia nzuri na zitakazokufikisha kwenye mafanikio. Kwanza kabisa tunaanza kwa kujenga tabia, halafu baadae ytabia zinatujenga. Kwa mfano kama umewahi kujifunz (more…)

SHUKRANI; Uhusiano Kati Ya Tabia Ya Shukrani Na Mafanikio Makubwa.

By | June 9, 2015

Mpenzi msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA, bado tunaendelea kujifunza tabia ya shukrani katika kipengele hiki cha kujijengea tabia za mafanikio. Baada ya kuona umuhimu na jinsi ya kujijengea tabia ya shukrani, leo tutaona uhusiano kati ya tabia ya shukrani na mafanikio makubwa. Kama unavyojua, lengo la KISIMA CHA MAARIFA ni (more…)

SHUKRANI; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Shukrani.

By | May 5, 2015

Karibu kwenye kipengele hiki cha kujijengea tabia za mafanikio ambapo mwezi huu tunaendelea na kujijengea tabia ya shukrani. Tabia ya kushukuru ni moja ya tabia zinazoweza kumpatia mtu furaha na kumwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha. Hii ni tabia ambayo kwa kuwa nayo inakufungulia milango mingi ya fursa ambazo unaweza (more…)

SHUKRANI; Faida Za Kujijengea Tabia Ya SHUKRANI.

By | April 15, 2015

Karibu kwenye kipengele hiki cha kujijengea tabia za mafanikio. Hizi ni tabia muhimu sana kwa kila mmoja wetu ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Kama ambavyo wote tunajua, kila kitu kinaanza na tabia, hivyo unavyojenga tabia bora unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwez akuboresha maisha yako. Mwezi huu wa nne tunajijengea (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Kujijengea Tabia Ya Shukrani.

By | April 7, 2015

Habari za leo msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA, karibu kwenye kipengele hiki cha jinsi ya kujijengea tabia za mafanikio. Kupitia kipengele hiki tunajifunza tabia mbalimbali ambazo ni muhimu sana wewe kuwa nazo ili kuweza kufikia mafanikio. Kama wote tunavyojua ni kwmaba tunajenga tabia halafu baadae tabia zinatujenga. Tatizo kubwa tulilonalo (more…)

KIPAUMBELE; Uhusiano Kati Ya Mafanikio Makubwa na Kuweka Kipaumbele.

By | March 31, 2015

Kama tulivyoona kwenye makala zilizopita kwenye tabia hii ya kujiwekea kipaumbele, kuba faida nyingi sana za kujiwekea kipaumbele kwenye maisha yako. Tuliona jinsi ambavyo dunia ya sasa imejaa kelele nyingi hivyo kama hujachagua kitu kimoja cha kufanya utajikuta unafanya kila kinachojitokeza mbele yako. Leo katika makala hii kwenye kipengele hiki (more…)