Category Archives: TABIA ZA MAFANIKIO

KIPAUMBELE; Tabia zinazoharibu kipaumbele chako kwenye maisha.

By | March 24, 2015

Pamoja na umuhimu mkubwa wa kuwa na kipaumbele kwenye maisha, bado watu wengi sana hawana kipaumbele au hata kama wakiwa nacho wanashindwa kukitekeleza. Kuna changamoto nyingi sana zinazowafanya watu kushindwa kuweka kipaumbele au kushindwa kufanyia kazi kipaumbele walichoweka. Na changamoto hizi zinaanzia kwenye tabia ambazo mtu anakuwa nazo. Katika makala (more…)

KIPAUMBELE; Jinsi Ya Kuweka Kipaumbele Kwenye Maisha Yako.

By | March 17, 2015

Karibu kwenye kipengele hiki cha jinsi ya kujijengea tabia za mafanikio na mwezi huu wa tatu tunajijengea tabia ya kuweka kipaumbele kwenye maisha yetu. Tunaishi kwenye dunia yenye kelele nyingi sana, bila ya kuw ana kipaumbele unaweza kuona muda unakwenda huku hujafanya chochote cha maana. Katika makala hii ya leo (more…)

Umuhimu na faida za kuwa na kipaumbele kwenye Maisha.

By | March 11, 2015

Tunaishi kwenye dunia ambayo kuna vitu vingi sana vya kufanya lakini muda ni mfupi. Labda tusiseme muda ni mfupi, bali muda umekuwa ni ule ule tokea zamani ila siku hizi mambo ya kufanya yamekuwa mengi sana. Kadiri maendeleo ya teknolojia yanavyotokea, tunapata vitu vingi sana vya kufanya. Kwa mfano ukianza (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Kuweka Kipaumbele Kwenye Maisha Yako.

By | March 3, 2015

Miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, kipaumbele pekee cha mwanadamu kilikuwa kula na kujilinda dhidi ya hatari. Katika nyakati hizo chakula kilikuwa kikipatikana kwa kuwinda au kuchimba mizizi. Hivyo mtu aliamka asubuhi akiwa na kipaumbele kikuu ambacho ni kutafuta chakula. Na usiku aliporudi kulala, kipaumbele kilikuwa kujilinda dhidi ya wanyama (more…)

UAMINIFU; Uhusiano kati ya tabia ya uaminifu na mafanikio Makubwa.

By | February 24, 2015

Uaminifu ni moja ya tabia muhimu sana unazohitaji kujijengea. Hii ni kwa sababu kwa tabia ya uaminifu itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa sana kuliko ambayo ungeyafikia kama usingekuwa na tabia ya uaminifu. Leo tutaona uhusiano wa karibu kati ya tabia ya uaminifu na mafanikio makubwa kwenye maisha. Kama tulivyoona kwenye siku (more…)

UAMINIFU; Jinsi ya kuepuka mazingira yanayokuondolea tabia ya uaminifu.

By | February 18, 2015

Mpaka sasa tumeshaona uaminifu ni tabia muhimu sana ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Hii ni kwa sababu unapokuwa mwaminifu watu wengi wanakuamini na wanakuwa tayari kushirikiana na wewe. Leo tutajadili jinsi ya kuepuka mazingira ambayo yanakuondolea tabia ya uaminifu. Hapa tutaangalia mbinu muhimu ambazo zitakuondoa kwenye mtego ambao utakufanya ufanye (more…)

UAMINIFU; Jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu.

By | February 10, 2015

Kama tulivyoona kwenye makala iliyopita, uaminifu ni tabia muhimu sana kw amtu yeyote anayetaka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake. Kuna watu ambao wanafikiri ukiwa masikini au ukiwa huna mafanikio basi huwezi kuwa mwaminifu. Na watu hawa hufikiri kwamba wakishakuwa na mafanikio basi wataanza kuwa waaminifu. Kosa kubwa sana, haufanikiwi (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Tabia Ya Uaminifu.

By | February 3, 2015

Kuna vitu vitatu muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kufikia mafanikio makubwa. Vitu hivyo ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kuwa mwaminifu na kuwa muadilifu. Ukikosa kimoja kati ya vitu hivi vitatu ni sawa na jiko la mafiga matatu ambalo limekosa figa moja, haliwezi kupika. Ukikosa vyote vitatu ni (more…)

Uhusiano Kati Ya Mafanikio Na Tabia Ya Kuahirisha Mambo.

By | January 20, 2015

Katika kipengele hiki cha tabia za mafanikio tunaendelea kujifunza jinsi ya kujijengea tabia ya kutokuahirisha mambo. Kama ambavyo tumekuwa tukiona awali, tabia ya kuahirisha mambo imekufanya mpaka sasa umeshindwa kufanya mambo makubwa sana kwenye maisha yako. Leo tutaangalia uhusiano kati ya mafanikio na tabia ya kuahirisha mambo. Uhusiano kati ya (more…)

Vitu vinavyochochea tabia ya kuahirisha mambo na jinsi ya kuviepuka.

By | January 6, 2015

Kama isingekuwa tabia ya kuahirisha mambo maisha yako yangekuwa tofauti sana na yalivyo leo. Maisha yako yangekuwa bora sana na huenda ungeshatekeleza baadhi ya ndoto zako. Lakini sisi ni binadamu na mara kwa mara tunaanguka kwenye udhaifu wetu. Tabia ya kuahirisha mambo inamuathiri karibu kila mtu. Ni rahisi sana kupanga (more…)