Category Archives: KITABU; A Guide to the Good Life The Ancient Art of Stoic Joy

Hiki ni kitabu kinachoeleza kuhusu falsafa ya ustoa.
Falsafa ya Ustoa ni moja ya falsafa ambazo zimekuwepo tangu enzi za tawala za Ugiriki na Roma. Ni falsafa ya maisha ambayo inamwezesha mtu kuwa na maisha ya utulivu, na yenye furaha muda wote bila ya kujali anapitia nini.
Karibu usome makala za uchambuzi wa kitabu hichi na pia kukisoma kitabu chenyewe na kuweza kuishi falsafa hii ambayo itafanya maisha yako kuwa bora.

KUISHI FALSAFA YA USTOA.

By | April 9, 2017

Kama ambavyo tumejifunza mpaka sasa, ustoa ni moja ya falsafa nzuri sana za maisha kwa sababu inatupa utulivu ndani ya nafsi zetu na kutuwezesha kuwa na maisha bora bila ya kujali tunapitia nini. Lakini kuishi falsafa hii ya ustoa kwa mgeni inaweza kuwa changamoto kubwa. Hii ni kwa sababu wengi (more…)

KUIFIKIRIA FALSAFA YA USTOA.

By | April 9, 2017

Kama ambavyo tumeona, ni muhimu sana mtu kuwa na falsafa ya maisha, kwa sababu bila ya falsafa, hakuna hatua kubwa mtu anaweza kupiga. Na kama ambavyo tumejifunza kwenye falsafa ya ustoa, dhumuni kuu la falsafa ya ustoa ni kuwa na utulivu kwenye maisha, kwa kuishi kulingana na asili. Zipo falsafa (more…)

USTOA WA KISASA – Anguko la ustoa wa zamani.

By | April 9, 2017

  Kama ambavyo tumeona, falsafa ya ustoa ilikuwa na nguvu kubwa wakati wa utawala wa Roma. Marcus Aurelius ndiye aliyekuwa mstoa wa mwisho mwenye nguvu. Marcus pia alikuwa mtawala wa Roma, lakini hakuipandikiza falsafa hii kwa waroma, aliishi yeye kama yeye. Baada ya Marcus, na kifo cha wastoa kama Epictetus (more…)

KUWA MSTOA – Anza Sasa Na Jiandae Kudhihakiwa.

By | April 9, 2017

Kuiishi falsafa ya ustoa siyo kitu rahisi, Kwanza kutokana na mazoea ambayo tayari tunayo, tunahitaji kubadili mengi tuliyokuwa nayo kwenye maisha na kubadili maisha yetu kwa ujumla. Na hakuna kitu kigumu kwa wengi kama wao wenyewe kuridhia kubadilika. Pia ugumu unakuja pale wengine wanapokuchukulia kwamba falsafa yako ni ya ajabu. (more…)

KIFO – Mwisho Mzuri Wa Maisha Mazuri.

By | April 9, 2017

  Kinachofanya watu wachukie uzee siyo tu hali mbaya ya afya, bali kuwa na uhakika kwamba kifo kimekaribia. Watu wengi wanaogopa sana kifo kwa sababu kuu mbili; 1. Kutokuwa na uhakika nini kitatokea baada ya kifo. 2. Kuhofia kwamba mtu hajayaishi maisha yake, hivyo kuhitaji muda zaidi ili kuyaishi maisha. (more…)

UZEE.

By | April 9, 2017

Vijana huwa wanaona dunia kama ni mali yao. Huona wana uwezo wa kufanya chochote wanachotaka kufanya na hawaoni umuhimu wa kuwa na maisha ya utulivu. Ni vigumu sana kumshawishi kijana kuielewa falsafa ya Ustoa kwa sababu anaona ana kila kitu. Lakini kijana anapofikia utu uzima, anapoanza kukosa kile anachotaka, ndiyo (more…)

Kuishi Uhamishoni/Kizuizini.

By | April 9, 2017

  Enzi za utawala wa Roma, wanafalsafa walikuwa wakipata shida kubwa sana ya kufukuzwa kwenye nchi zao na kwenda kuishi uhamishoni. Wengine walihukumiwa kufa kabisa. Kwa watu wa kawaida, kwenda kuishi uhamishoni, sehemu ambayo hujaizoea na hakuna unayemjua, kunatosha kukuvuruga na kukuondolea furaha. Lakini wastoa wote waliofukuzwa na kwenda uhamishoni, (more…)

MAADILI BINAFSI – Kuhusu Maisha Ya Anasa.

By | April 9, 2017

Moja ya vitu vinavyowavuruga watu ni kukazana sana kutafuta fedha ili kuishi maisha ya anasa. Kuweza kuvaa nguzo nzuri na zinazowavutia wengine, pia kula vyakula vitamu ba kuishi majumba ya kifahari. Kutaka na kupata vitu vizuri siyo kubaya iwapo dhamira ya moyo wetu ipo safi. Lakini kama tunafanya ili tu (more…)

MAADILI BINAFSI – Kuhusu Kutafuta Umaarufu.

By | April 9, 2017

Seneca anasema, watu hawana furaha kwa sababu hawajui hasa ni nini wanataka kwenye maisha yao. Wanakazana kutafuta umaarufu wakiamini wakiwa nao watakuwa na furaha, lakini kila umaarufu una gharama zake. Kwanza kabisa unapotaka wengine wakukubali, maana yake inabidi ufanye yale wanayotaka wao. Na hivyo huwezi kuishi maisha yako, hivyo hata (more…)

HASIRA – Jinsi ya kushinda hali ya kutokuwa na furaha.

By | April 9, 2017

  Hasira ni moja ya hisia hasi tunazokutana nazo kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye siku zetu. Kwa kuwa wastoa tunapenda kuwa na utulivu, hasira zinavuruga utulivu wetu. Hovyo wastoa wanatushauri kutoendekeza hasira. Seneca anasema kwamba hasira ni ukichaa wa muda mfupi, yaani unapokuwa na hasira, huna tofauti na kichaa (more…)