All Courses

ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION)

Fedha ni hitaji la msingi kabisa kwenye maisha yetu, ni kitu ambacho kinatuwezesha kupata mahitaji yetu ya msingi na maisha kuweza kwenda.

Fedha ndiyo kitu ambacho tunapigania kila siku, tunafanya kazi na biashara zetu, pamoja na mengine lakini pia kupata fedha ili kuweza kuendesha maisha yetu.

Pamoja na umuhimu huu mkubwa wa fedha kwenye maisha yetu, watu hawana elimu sahihi ya fedha. Hii ni kwa sababu mfumo wetu wa elimu haufundishi kuhusu mambo yanayohusu fedha binafsi, na kwenye jamii siyo wengi wenye uelewa juu ya hilo.

Kutokana na kukosekana kwa elimu hii muhimu ya fedha, watu wamekuwa wanafanya makosa mengi sana kwenye maisha yao kwa upande wa fedha. Kwa mfano;

1. Watu wengi hawaweki akiba, wanatumia kipato chote mpaka kinaisha.

2. Watu wengi wanaingia kwenye madeni ambayo yanawatesa sana kwenye maisha yao.

3. Watu hawana uwekezaji ambao unaweza kuwapa uhuru wa kifedha baadaye.

Hayo na mengine mengi, yamekuwa yanawafanya watu kuendelea kuwa masikini maisha yao yote.

Kupitia kozi hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, tunakwenda kujifunza mambo yote muhimu tunayopaswa kuyafahamu kuhusu fedha. Kuanzia kuipata fedha, kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kuweka akiba, kuwekeza na hata kulinda fedha zetu zaidi.

Kitu kizuri zaidi kwenye kozi hii ni kwamba tutapata elimu kuhusu kodi na bima ambayo ni maeneo muhimu sana kwenye fedha zetu.

Kama hiyo haitoshi, tutajifunza umuhimu wa kuancha wosia juu ya urithi wa mali zako.

Kikubwa zaidi ambacho utajifunza kwenye kozi hii, ni kuweza kuwaandaa watoto kuwa na elimu sahihi ya kifedha. Utajifunza misingi ya kuwajengea na wakati gani wa kujenga misingi hiyo.

Karibu sana kwenye kozi hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, uweze kujifunza na kuondoka kwenye umasikini.

Kwa kusoma kozi hii utaweza kujijengea msingi sahihi wa kifedha ambao utakuwezesha;

1. Kuongeza kipato chako na njia za kutengeneza kipato.

2. Kuondoka kwenye madeni.

3. Kuweza kuweka akiba na fedha za dharura.

4. Kuanza biashara na uwekezaji.

5. Kuwajengea watoto wako msingi wa kifedha ili wasifanye makosa uliyofanya wewe.

Hii siyo kozi ya kukosa kama kweli upo makini na eneo la fedha.

ADA YA KOZI YA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Ili kuweza kupata masomo haya ya elimu ya msingi ya fedha, unapaswa kulipa ada ya tsh 20,000/= (tsh elfu 20 tu). Malipo yanafanyika kwa njia ya simu, MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253. Ukishatuma fedha, tuma majina yako kamili na email kwenye moja ya namba hizo ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki kozi hii.

Karibu sana.

Instructor:  Makirita Amani
already started
SWAHILI
FREE
Details

0 thoughts on “All Courses

 1. george katyenyi

  Naamini kama nusu ya vijana wa leo na kesho pia wa Kitanzania tukiwa na maono haya tutaleta mabadiliko katika nchi hii.

  1. Amani Makirita

   Asante kwa maoni. Nilipanga kuenda taratibu ili kila mmoja aweze kuelewa na kujifunza kwa hatua. Kama maoni yakiwa mengi tutaongeza urefu. Mara nyingi makala hazizidi maneno elfu moja ili kutochoka wakati wa kusoma.

 2. hussein hanafi

  Naungana na mdau hapo juu makala iwe ndefu zaidi au uiongezee idadi ya siku ya kutoka…ushatufundisha vizuri sana namna ya kusoma kwa mazingatio..kwa yule ambaye spidi yake ya kusoma ndogo itabidi awe anasoma polepole kulingana na spidi yake..tuna hamu kubwa ya kukimbizana na muda ili tuyajue mengi zaidi..sasa hivi hatutambai bali tunakimbia..ingawa wanasema slow but sure nadhan hiyo imekua slow zaidi kwetu…asante sana wazo langu ni hilo tu

 3. Samson Aron

  Unagusa sana hisia zangu,

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
  Nimeanza kuwa mwalimu wa uchumi bila kuingia darasani, nimeanza kufikiri mambo makubwa kuliko mwanzo sasa siwazi tena kuendelea kuwa mtumwa wa kazi za watu bali nawaza nianze kujiajiri mwenyewe.

  Nimeanza kutafuta habari sahihi kwa kile ninachokihitaji kukipata, usomaji wa vitabu imeanza kuwa kama desturi yangu na najifunza mambo makubwa yaliyojificha ndani yake.

  Nilichogundua ni kwamba maisha tunayofundishwa mashuleni na majumbani kwa asimilia kubwa tunaambiwa bila Elimu ya chuo kikuu huwezi kuwa tajiri na utaishia kuwa masikini.

  Nimepata bahati ya kumsikiliza MZEE MFUGALE kwenye ushuhuda wake aliuzwa hivi; unajuta kwa kutosoma? Alisema sijawahi juta hata siku moja sababu niliosoma nao wakawa na elimu kubwa wengi ni maskini wakubwa.

  Endelea kutuelimisha japo Mtanzania kwa kusoma vitu kama hivi ni vigumu sana maana tunapenda kufuatilia habari za udaku na mapenzi lakini habari njema hututaki tunaona ni ndefu na zinachosha.

  1. Amani Makirita

   Asante sana Samson kwa kuendelea kujifunza na kuanza kuchukua hatua. Ni kweli kabisa kwamba elimu hii ni muhimu ila sio wote wanaona umuhimu wake. Tuendelee kuwashirikisha wenzetu ili nao wapate mambo haya mazuri.
   Karibu sana, TUENDELEE KUWA PAMOJA.

 4. Godlove Ulomi

  kaka sna uwezo wa kukulipa kazi hi kubwa ufanyayo ya kiuzalendo.Chukua neno hill .Mungu na azdi kukubarki na kukuongezea miaka Mara kumi ya uliyo nayo

 5. Godlove Ulomi

  kaka kiukwel kwa elimu hii hata hiyo elf hamsn ni ndogo sana.thamani yake akiln n kubwa kushinda.mazuzu hawawez kulitambua hlo

  1. Amani Makirita

   Asante sana Godlove,
   Ni kweli gaharama ya elimu hii ni kubwa sana ila kwa kuwa tunapenda kila mtanzania aweze kuipata tunaweka gharama ambazo yeyote mwenye nia ya kujifunza anaweza kumudu.
   TUKO PAMOJA.

 6. Godlove Ulomi

  kiongozi asante kwa kunitoa kwenye tatzo la akil litwalo UTINDIO Wa UBONGO,kwani mafundisho haya yanatbu sana tatzo hilo.anayekufa maskin utindio huwa umemtawala kwa 90%.asante kwa TBA nzur