KARIBU TUFANYE KAZI PAMOJA.

Karibu tufanye kazi pamoja

Karibu tufanye kazi pamoja

Habari Rafiki yangu?

Ni mimi Rafiki na Kocha wako Makirita Amani.

Karibu kwenye ukurasa huu muhimu kuhusu mimi na jinsi tunavyoweza kufanya kazi kwa pamoja.

Mimi ni kijana wa Kitanzania, ambaye nimedhamiria kufanya makubwa kwenye nchi yangu na kwa wale wanaonizunguka. Malengo yangu makubwa ni kuwa Bilionea ili kuweza kuwasaidia wengi zaidi na pia kuwa raisi wa nchi yangu Tanzania(mwaka 2040) ili niweze kutoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu.

Mimi ni mwandishi, mshauri na mjasiriamali.

Ninaendesha mitandao miwili, AMKA MTANZANIA  na KISIMA CHA MAARIFA.

Ni mwandishi wa makala na vitabu vya maisha, kazi, biashara na mafanikio.

Mimi ni mshauri na kocha wa biashara na maisha ya mafanikio.

Pia ni mkurugenzi wa kampuni ya KICHAMATA INVESTMENT COMPANY LIMITED (KICOL), kampuni ambayo inahusika na uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali.

Jinsi ya kufanya kazi na mimi.

Nimekuwa napokea simu na jumbe nyingi kila siku za watu ambao wanahitaji tufanye kazi pamoja katika ushauri au kuwa kocha wao. Lakini muda wangu ni mfupi na hivyo siwezi kuwasiliana na kila mtu. Hivyo nimetengeneza njia bora ya kuweza kumsaidia kila anayehitaji ushauri kutoka kwangu. Hapa kuna njia SITA(6) unazoweza kufanya kazi na mimi, niwe kama mshauri au kocha wako;

Njia ya kwanza ni kusoma makala zangu.

Kwa wale ambao bado hawajanijua vizuri, unaweza kusoma makala zangu bure kabisa ambazo zipo kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA. Pia unaweza kunifuatilia kwenye mitandao ya Facebook, Twitter, LinkedIn na Instagram kwa kutafuta @coachmakirita. Huhitaji kulipia chochote. Kuna mengi ambayo utajifunza na kama utayafanyia kazi basi maisha yako hayatabaki kama yalivyo sasa.

Njia ya pili ni kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kama unataka tuwe karibu zaidi, uwe unapata kila ninachofikiria, kila siku kwa mwaka mzima, pamoja na kukutana na watu wengine wenye mawazo chanya ya mafanikio, basi karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kupitia KISIMA CHA MAARIFA kila siku unapata makala za KURASA ZA MAFANIKIO na pia unapata TAFAKARI ya kuianza siku yako, kila siku.

Ili kujiunga unahitajika kulipia ada ndogo ya tsh laki moja (100,000/=) ambayo ni ada ya mwaka mzima tokea unapojiunga. Kupitia kisima cha maarifa tunakuwa karibu sana kama marafiki. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye neno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap kwenda namba 0717 396 253.

Njia ya tatu ni USHAURI WA MARA MOJA.

Kama kuna jambo ambalo linakusumbua na ungependa kupata ushauri wangu basi tunaweza kuwasiliana na nikakushauri. Ushauri unahitaji muda, siyo kitu cha dakika moja, tano au kumi. Tunahitaji kuwa na mazungumzo yasiyopungua nusu saa na wakati mwingine kwenda mpaka saa moja. Huwa sitoi ushauri kwa njia ya ujumbe wa simu, badala yake tunakuwa na mazungumzo, ambayo tumepanga kabisa na tunasikilizana vizuri. Na ushauri natoa kwa njia ya mazungumzo ya simu pekee, ana kwa ana ni vigumu sana kukutana kutokana na ufinyu wa muda. Ila kama utapenda tuonane ana kwa ana tuwasiliane.

Ili kupata ushauri kutoka kwangu unahitajika kuchangia gharama za ushauri ambazo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwa mazungumzo yasiyozidi nusu saa na tsh elfu 30 (30,000/=) kwa mazungumzo yasiyozidi saa moja. Ili kupata ushauri unahitajika kutuma kiasi cha fedha kinachoendana na muda wa ushauri kwenye namba 0755953887 au 0717396253 na kisha tunapanga muda wa kufanya mazungumzo hayo.

Njia ya NNE ni mimi KUKUANDIKIA MAKALA AU KITABU.

Kama una blog, gazeti au jarida na ungependa mimi nikuandikie makala tunaweza kufanya kazi pamoja. Pia kama una wazo la kutaka kuandika kitabu tunaweza kufanya kazi pamoja na nikakuandikia kitabu kama unavyotaka wewe. Makala au kitabu nitakachokuandikia utasema ni nini unataka na unataka viandikweje na pia utamiliki wewe mwenyewe na utaamua utumieje.

Gharama ya huduma hii kwa sasa ni tsh elfu 30(30,000/=) kwa makala moja, makala mbili tsh elfu 50(50,000/=). Gharama za uandishi wa kitabu tuwasiliane.

Njia ya TANO ni MAFUNZO KWA VIKUNDI NA WAFANYAKAZI.

Kama mna kikundi ambacho mngependa kupata mafunzo ya biashara, ujasiriamali na mafanikio, naweza kutoa mafunzo kwa kikundi chenu kwa njia ya moja kwa moja au njia ya mtandao kupitia makundi ya wasap. Pia kama una wafanyakazi kwenye kampuni au biashara yako naweza kutoa mafunzo ya kuwawezesha kuwa na ufanisi mkubwa kwenye kazi zao na kuweza kutengeneza faida kubwa kwenye biashara yako. Ili kupata utaratibu wa mimi kutoa mfunzo kwenye kikundi chenu au wafanyakazi wako, tuwasiliane kwa simu 0717 396 253.

Njia ya SITA ni MIMI KUWA KOCHA WAKO.

Kama ungependa mimi nikusimamie moja kwa moja kwenye kile unachofanya, naweza kuwa kocha wako. Faida za mimi kuwa kocha wako ni kwamba tunapanga malengo na mipango pamoja na kisha nakuwa nakufuatilia kwenye utekelezaji wa malengo na mipango hiyo. Ninapokuwa kocha wako, tunawasiliana mara moja kila wiki, hasa siku ya jumamosi au jumapili, tunapitia wiki inayokwisha na kupanga wiki inayokwenda kuanza.

Ili mimi niwe kocha wako unahitaji kulipia ada ya mwezi ambayo ni tsh laki mbili (200,000/=).

Hata hivyo nafasi za kuwa kocha ninazoweza kutoa ni chache, hivyo kabla hujatuma ada ya mimi kuwa kocha wako, tuwasiliane kwanza ili kujua kama nafasi zipo ndiyo tuweze kuanza.

Njia nyingine muhimu ya kujifunza kupitia mimi ni kusoma vitabu ambavyo nimeandika, vitabu hivi vinapatikana kwenye mtandao wa KISIMA CHA MAARIFA. Bonyeza hayo maneno na utapata vitabu vizuri vya kujisomea.

Karibu sana rafiki yangu tufanye kazi kwa pamoja,

Nina mengi ninayoweza kukushirikisha, kwa uzoefu wangu binafsi, kupitia uzoefu wa wengine ambao nimewashauri na pia kupitia mafunzo ninayopata kwa kusoma vitabu na tafiti mbalimbali za maisha, biashara na mafanikio.

“Dhumuni langu kubwa kwenye maisha ni kuwasaidia watu kuishi maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa kupitia mafundisho yangu, maandiko yangu na ukocha wangu.” Makirita Amani.

Je wewe unataka kuwa mmoja wa hawa wanaoweza kunufaika na ninachofanya? Karibu tufanye kazi kwa pamoja.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Success Coach, Author and Entrepreneur

Blogs; www.amkamtanzania.com and www.kisimachamaarifa.co.tz

Contacts; +255 717 396 253 / +255 755 953 887

Email; amakirita@gmail.com / makirita@kisimachamaarifa.co.tz