2401; Hisia, Hadithi, Mantiki…

By | July 28, 2021

2401; Hisia, Hadithi, Mantiki… Hivyo ni vitu vitatu tunavyotumia katika kufanya maamuzi yote kwenye maisha yetu. Huwa tunadhani tunafanya maamuzi kwa mantiki, kisha kuyajengea hadithi na kuwa na hisia nayo. Lakini sivyo tunavyofanya. Huwa tunafanya maamuzi kwa hisia kwanza, kisha tunatengeneza hadithi inayotetea maamuzi hayo na mwisho ndiyo tunatafuta mantiki (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UGUMU WA MABADILIKO…

By | July 28, 2021

Kama unataka kubadili matunda ambayo mtu unazalisha, kukata matawi hakutasaidia. Unapaswa kung’oa kabisa shina la mtu huo na kupanda mti mwingine. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mabadiliko ya maisha yetu. Hutaweza kuyabadili maisha kwa kuhangaika na tabia pekee, bali anza kwa kubadili imani ya ndani yako. Tabia ulizonazo ni matokeo (more…)

2400; Kinachofanya mabadiliko kuwa magumu

By | July 27, 2021

2400; Kinachofanya mabadiliko kuwa magumu kwako… Ni kwa sababu unahangaika na kitu kisichokuwa sahihi. Unaweka juhudi zako eneo ambalo haliwezi kuzalisha mabadiliko. Unahangaika na matokeo badala ya kile kinachozalisha matokeo hayo. Unahangaika na matawi badala ya shina. Kama unataka kuyabadili maisha yako, usihangaike na yale matokeo unayopata sasa, bali hangaika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUSHINDWA KABLA YA KUANZA…

By | July 27, 2021

Unayashindwa maisha, kazi au biashara kabla hata hujaanza kwa sababu unawaiga wengine. Unapofanya kama wanavyofanya wengine, watu wanakuwa hawana sababu ya kuja kwako. Unakuwa umewaambia kwamba wewe huna umuhimu wowote. Njia pekee ya kushinda ni kuwa wewe, wewe ambaye ni wa kipekee, ambaye hujawahi kutokea na hutakuja kutokea tena. Weka (more…)

2399; Jenga nguvu ya ushindani…

By | July 26, 2021

2399; Jenga nguvu ya ushindani… Kama kuna vitu viwili vinavyofanana na ambavyo vipo sehemu moja, kimoja hakina umuhimu. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye biashara. Kama kuna biashara mbili zinazofanana kwa kila kitu, moja siyo muhimu. Na kama biashara zinazofanana ni nyingi, nyingi pia zinakuwa siyo muhimu. Inakwenda hata kwenye kazi. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAAMUZI NA MATOKEO…

By | July 26, 2021

Usiunganishe moja kwa moja maamuzi unayofanya na matokeo unayopata. Maamuzi sahihi yanabaki kuwa sahihi hata kama matokeo yake ni tofauti na ulivyotarajia. Usikimbilie kubadili maamuzi kwa sababu matokeo siyo mazuri, badala yake badili mbinu unazofanyia kazi. Kuwa na mchakato wa kufikia maamuzi sahihi na pia kuwa na mchakato wa kufanyia (more…)

2398; Usibadili Maamuzi, Badili Mikakati…

By | July 25, 2021

2398; Usibadili Maamuzi, Badili Mikakati… Umeamua kwamba ni sahihi kwako kuingia kwenye biashara. Ni kitu ambacho umeona kinatoka ndani yako kweli. Umeiona fursa nzuri, Na unaona ndiyo njia ya uhakika ya kuishi kusudi lako na kuzifikia ndoto zako kubwa. Unaingia kwenye biashara ukiwa na hamasa kubwa. Unaona jinsi unakwenda kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAJUE KUHUSU WEWE, ILA WASIKUJUE…

By | July 25, 2021

Mafanikio yana gharama kubwa. Na mafanikio yanapoambatana na umaarufu, yanakuwa na gharama kubwa zaidi. Wengi kabla hawajafanikiwa hutamani sana wapate umaarufu kwani huamini mafanikio yanayoendana na umaarufu ndiyo mazuri. Lakini wakishafanikiwa na kuwa maarufu ndiyo wanagundua jinsi hilo lilivyo mzigo mkubwa. Unapofanikiwa na kuwa maarufu unakuwa lengo la mashambulizi kwa (more…)

2397; Mambo ya kuzingatia unapokuwa juu…

By | July 24, 2021

2397; Mambo ya kuzingatia unapokuwa juu… Kila mtu anapenda kwenda juu, kufika kwenye kilele cha juu kabisa cha mafanikio. Lakini wengi huangalia upande mmoja tu wa kuwa juu, upande wa mazuri. Kuwa juu kuna upande wa mabaya yake, ambao unaambatana na changamoto mbalimbali. Ipo kauli inayosema kadiri unavyokwenda juu, ndivyo (more…)