Mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara.

By | July 13, 2021

Mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara. Mauzo ndiyo injini ya biashara yoyote ile. Bila mauzo hakuna fedha inayoingia kwenye biashara na hapo hakuna biashara. Kila biashara inaweza kuongeza mauzo zaidi ya inavyofanya sasa, hata kama mauzo yako juu kiasi gani. Hapa ni mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara (more…)

2386; Kama bado unajiuliza, jibu ni hapana…

By | July 13, 2021

2386; Kama bado unajiuliza, jibu ni hapana… Hakuna siku unaamka asubuhi na kujiuliza kama uko hai au la, kama uko hai unajua uko hai. Vitu unavyojua kwa hakika kwenye maisha yako huwa hujiulizi ulizi kila wakati, tayari majibu unayo. Hilo lipeleke kwenye kila eneo la maisha yako, ukiona bado unajiuliza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUNUFAIKA NA UNAYOSOMA…

By | July 13, 2021

Watu wengi hawanufaiki na yale wanayosoma, kwa sababu shule zimewaharibu. Shuleni mtu alisoma ili kufaulu mtihani, mtihani ukishapita basi hajali tena yale aliyosoma. Kwenye maisha husomi ili kujibu mtihani, bali unasoma ili kuyafanya maisha yako kuwa bora. Hivyo kwa kila unachojifunza, unapaswa kukitafakari ba kuona jinsi ya kukitumia kwenye maisha (more…)

2385; Kula na Kumeng’enya…

By | July 12, 2021

2385; Kula na Kumeng’enya… Unapokula chakula, hakiingii moja kwa moja kwenye mwili wako kama ulivyokila. Badala yake kinameng’enywa kwanza, kinavunjwa kwenye vipande vidogo vidogo na kisha kufyonzwa kwenye mwili. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kusoma. Kusoma ni kama kula, unachosoma siyo kinachoingia kwenye akili yako, bali kile unachochakata. Hivyo usifurahie (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUJIDANGANYA NA KUJIFARIJI…

By | July 12, 2021

Sababu nyingi unazojipa za kwa nini hujaweza kufanya au kupata unachotaka siyo sababu halisi, bali ni visingizio tu. Kwa visingizio hivyo umekuwa unajidanganya na kujifariji, kitu ambacho ni kikwazo kwa mafanikio yako. Kama kuna kitu unajipa kama sababu ya kikwazo, lakini wengine wameweza kuvuka kitu hicho, basi hiyo siyo sababu, (more…)

2384; Sababu na visingizio…

By | July 11, 2021

2384; Sababu na visingizio… Kuna vitu huwa unapanga au kupenda kufanya, lakini unashindwa kukamilisha kama ulivyopanga. Huwa unatoa sababu mbalimbali kwa nini umeshindwa kufanya au kupata unachotaka. Lakini kiukweli kabisa nyingi unazotoa siyo sababu, bali ni visingizio. Sababu ni vile vikwazo au changamoto za kweli kabisa, ambazo zinamzuia kila mtu. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; GEUZA HOFU KUWA FURAHA…

By | July 11, 2021

Jamii imekutengenezs kuhofia mambo yasiyo na tija yoyote kwako. Mfano kuhofia wengine wanakuchukukiaje, kuhofia kukosolewa na hata kuhofia kupitwa na yanayoendelea kwenye mitandao. Hofu zote hizo hazina manufaa yoyote kwako. Ili kuziondoa zisiwe kikwazo, zigeuze kuwa furaha. Furahia pale wengine wanapokupinga au kukukosoa na kama ni watu sahihi jifunze kwao, (more…)

2383; Furahia Kupitwa…

By | July 10, 2021

2383; Furahia Kupitwa… Mitandao ya kijamii imekuwa inakunasa kwenye uraibu kwa kukufanya uone kama unapitwa. Sisi binadamu tunahofia sana kupitwa na yale muhimu, maana kutokupitwa ndiyo kuliwawezesha watangulizi wetu kuepuka hatari mbalimbali na kuweza kuendeleza kizazi cha binadamu hapa duniani. Kipindi cha nyuma ilikuwa hatari sana kwa mtu kukaa na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USICHANGANYE VIPAUMBELE…

By | July 10, 2021

Mafanikio makubwa ndiyo kipaumbele cha kwanza kabisa kwenye maisha yako, hupaswi kuruhusu kitu kingine kuingilia kipaumbele hicho. Utaona wengine wakihangaika na mambo mbalimbali kwenye maisha na kutamani kufanya kama wao. Lakini jua wengi hawafiki kwenye mafanikio makubwa na sababu kuu ni kuhangaika na mambo mengi badala ya kuweka vipaumbele sahihi. (more…)