#TAFAKARI YA LEO; TUMIA AU POTEZA…

By | June 14, 2021

Kuna mambo mengi umewahi kujifunza kwenye maisha yako na kujiambia siku moja utayatumia, lakini umeshayasahau kabisa.Kuna mawazo mazuri yamewahi kukujia na ukajiambia utakuja kuyafanyia kazi ila umeyasahau kabisa.Kama hutatumia mawazo au maarifa unayoyapata wakati bado ni ya moto kabisa, nafasi ya kuyapoteza ni kubwa.Kila unapojifunza kitu, jiulize hapo hapo unawezaje (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya

By | June 13, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya mbao. Samani mbalimbali zinatengenezwa kwa kutumia mbao. Hilo linafanya uhitaji wa mbao kuwa mkubwa na kutoa fursa ya kibiashara kwa wale wanaoweza kushughulika na upatikanaji wa mbao. Hapa ni mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia biashara ya mbao. Kununua na kuuza mbao (more…)

2356; Usisubiri Yapoe…

By | June 13, 2021

2356; Usisubiri Yapoe… Kitu pekee ambacho nimekuwa nanufaika nacho kwenye maarifa mbalimbali ninayopata ni kujiuliza nawezaje kuyatumia na kisha kuchukua hatua mara moja, kabla hata maarifa hayo hayajapoa. Huduma zote ambazo nimeweza kuanzisha na kuboresha mpaka sasa ni kutokana na utaratibu huu wa kuyatumia maarifa yakiwa ya moto badala ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UKIINGIZA UCHAFU UTATOA UCHAFU…

By | June 13, 2021

Akili yako ni kompyuta yenye uwezo wa hali ya juu mno. Huwa inachakata chochote kinachoingia na kuzalisha matokeo. Kama uchafu unaingia kwenye akili, akili inauchakata na kutoa uchafu zaidi. Vile ulivyo sasa kwenye maisha yako ni matokeo ya kile ulichoruhusu kiingie kwenye akili yako. Kama unataka kuyabadili maisha yako, anza (more…)

2355; Utapiamlo Wa Akili…

By | June 12, 2021

2355; Utapiamlo Wa Akili… Watu wengi hasa kwenye zama hizi wana utapiamlo wa akili. Kama ilivyo kwamba usipoulisha mwili vizuri unapata utapiamlo wa mwili, ndivyo pia usipoilisha akili vizuri unapata utapiamlo wa akili. Ili kuondokana na utapiamlo wa akili, unapaswa kuilisha akili yako kilicho sahihi. Unapaswa kuwa na dayati maalumu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; PAMBANA MPAKA UFIKIE LENGO…

By | June 12, 2021

Ukishajiwekea lengo, kinachofuata ni wewe kupambana mpaka ulifikie lengo hilo. Usipoteze nguvu zako kwenye kujishawishi kulibadili lengo kwa sababu unaona huwezi kulifikia. Badili mikakati na njia unazotumia, lakini usibadili lengo. Hata kama huoni namna ya kulifikia lengo, wewe amini kwenye lengo lako na kaa kwenye mchakato. Tathmini kila hatua unazochukua (more…)

2354; Ng’ang’ana na lengo, siyo njia…

By | June 11, 2021

2354; Ng’ang’ana na lengo, siyo njia… Kitu muhimu kabisa na unachopaswa kung’ang’ana nacho kwenye maisha yako ni malengo makubwa uliyonayo. Piga, ua garagaza, hakikisha unapambana kwa kila namna kuyafikia malengo hayo makubwa. Lakini hupaswi kung’ang’ana na njia moja katika kuyafikia malengo yako. Njia zipo nyingi, kuna ambazo ni sahihi na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA MAISHA YA MAJARIBIO….

By | June 11, 2021

Watu wengi huendesha maisha yao kama vile bado wapo kwenye majaribio au mazoezi ya kuja kuishi maisha yenyewe. Kila wakati wanaahirisha kuishi, wakiwa shule wanajiambia wataanza kuishi wakihitimu na kupata kazi. Wakipata kazi wanajiambia wataanza kuishi wakistaafu. Wakistaafu wanajikuta wameshachelewa na wanakufa. Maisha yako ndiyo hayo unayoyaishi sasa, hakuna siku (more…)

2353; Unaweza Kutabiri Kwa Haya Matano…

By | June 10, 2021

2353; Unaweza Kutabiri Kwa Haya Matano… Unaweza kutabiri iwapo biashara mpya itafanikiwa au kushindwa kwa kuangalia maeneo haya matano. Moja ni wazo, je wazo ni sahihi kwa mwanzilishi wa biashara. Kila wazo ni zuri, lakini inategemea sana nani anatekeleza wazo hilo. Kama mtekelezaji hana hamasa na msukumo mkubwa kwenye wazo (more…)