#TAFAKARI YA LEO; WANAPOKUKOSOA FURAHI…

By | June 10, 2021

Kwa sababu ni kiashiria kwamba unafanya kitu kikubwa na cha tofauti. Pia ukosoaji wao unakupima kama kweli unakiamini na kukisimamia kile unachofanya. Ukosoaji, upingaji na ukatishaji tamaa wa wengine, ni vitu vyenye manufaa kwako, maana ukiweza kuvivuka, utakuwa imara kupata chochote unachotaka. Ukurasa wa kusoma ni wanaokukosoa wanakusaidia; www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/09/2352 #NidhamuUadilifuKujituma (more…)

2352; Wanaokukosoa Wanakusaidia…

By | June 9, 2021

2352; Wanaokukosoa Wanakusaidia… Huwa hatupendi watu watukusoe au kutukatisha tamaa kwenye yale makubwa tunayoamua kufanya. Tunaona siyo sawa kwa watu kuchagua kutushambulia wakati tunachofanya kinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa wengi. Lakini kama ambavyo tumekuwa tunashirikishana, huwa kuna upande mzuri wa kila jambo. Hata kama kitu unakiona ni kibaya au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VIKUFANYE KUWA IMARA ZAIDI…

By | June 9, 2021

Hakuna siku maisha yako yatakosa vikwazo na changamoto mbalimbali. Hivyo ni vitu vitakuandama katika kipindi cha uhai wako. Hivyo njia pekee ya kuwa na maisha ya mafanikio na yenye utulivu, ni kutumia kila kikwazo na changamoto kuwa imara zaidi, kuwa bora zaidi baada ya changamoto kuliko ulivyokuwa kabla. Usizikimbie changamoto (more…)

2351; Laini, Ngumu Na Imara…

By | June 8, 2021

2351; Laini, Ngumu Na Imara… Nassim Taleb kwenye kitabu chake cha Antifragile anaeleza mifumo yote inaweza kuwa kwenye kundi moja kati ya haya matatu. Kundi la kwanza ni laini (fragile), hii huwa rahisi kuvunjika pale inapokubwa na tatizo. Mifumo laini huwa haiwezi kuhimili matatizo na changamoto mbalimbali. Mifumo hii inaweza (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ukalimani wa

By | June 8, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia ukalimani wa lugha. Kadiri dunia inavyoungana na kushirikiana, watu wanahitaji kushirikiana kwenye shughuli mbalimbali. Lakini lugha huwa ni kikwazo katika ushirikiano huo. Hapo inajitokeza fursa ya ukalimani, ambapo mtu anayezielewa vizuri lugha mbili, anaweza kusaidia kwenye mawasiliano. Hapa ni njia kumi za kuingiza kipato (more…)

2350; Uhalisia hauna mbwembwe…

By | June 7, 2021

2350; Uhalisia hauna mbwembwe… Angalia kipindi cha mapishi kwenye tv au mtandaoni. Kisha nenda kapike kwa hatua zote ulizojifunza kwenye kipindi hicho. Matokeo ya mwisho hayatakuwa kama unayoona kwenye tv. Kuna mahali utakosea tu, hata kama ni kidogo kiasi gani, labda ni chumvi utazidisha au kupunja, au mafuta yasitoshe au (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNAYEPASWA KUMHOFIA ZAIDI…

By | June 7, 2021

Siyo yule anayeongea sana, bali yule anayekaa kimya. Anayeongea sana anaweka kila kitu wazi kuhusu yeye, hivyo unaweza kujua mipango yake na kujiandaa mapema. Anayekaa kimya hujui anapanga nini na huwezi kujiandaa kwa ajili yake. Hivyo hofia zaidi wale wanaokaa kimya kuliko wanaoongea sana. Lakini pia wapo wanaoongea sana kama (more…)

2349; Nini Unajaribu Kuficha…

By | June 6, 2021

2349; Nini Unajaribu Kuficha… Huwa ipo kauli kwamba ukimuona mtu anajisifia sana kwa kitu fulani, jua hicho kitu hana au anatumia sifa hizo kuficha kitu kingine ambacho hataki kionekane. Mfano mtu anayesema mimi siyo muoga hata kidogo, huwa ndiye muoga zaidi. Anatumia kauli hiyo kuficha uoga wake. Hivyo pia ndivyo (more…)