#TAFAKARI YA LEO; WENYE CHUKI WAPUUZE…

By | June 2, 2021

Huwa tunapenda kupendwa na kukubalika na kila mtu. Lakini hata tufanyenye, kuna watu wanachagua tu kutuchukia. Hasa pale unapochagua kuyaishi maisha yako na kufanya makubwa, wengi hawatafurahishwa na hilo. Lakini wajibu wako siyo kumfurahisha kila mtu, bali kuyaishi maisha yako. Chagua kuyaishi maisha yako na wapuuze wale wanaokuchukua kwa wewe (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia sanaa.

By | June 1, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia sanaa. Sanaa ni eneo ambalo linawaburudisha watu. Kwa kuwa watu wanapenda burudani, huwa tayari kulipia ili kuipata. Zipo fursa nyingi za kuingiza kipato kupitia sanaa. Hapa ni mawazo kumi unayoweza kufanyia kazi. Kuwa msanii, iwe ni uimbaji, uchoraji, uigizaji n.k. Kuwa meneja wa msanii. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; BILA UKOMO WA MUDA HUTAKAMILISHA KUFANYA…

By | June 1, 2021

Ukomo wa muda ndiyo unaotusukuma kukamilisha kitu, hasa pale tunapokuwa tumewaahidi wengine na kutokukamilisha kwetu kwa wakati kunatugharimu. Kwa kila unachopanga kufanya, jiwekee tarehe kabisa ni lini utakuwa umekamilisha na weka uwajibikaji kwako ili ukamilishe kwenye tarehe hiyo. Nje ya hapo ni vigumu sana kukamilisha chochote kikubwa. Ukurasa wa kusoma (more…)

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia soko la

By | May 31, 2021

Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia soko la hisa… Wengi wanaposikia hisa huwa wanaona ni kitu kikubwa na wasichoweza kujihusisha nacho kwa sababu hawana uelewa. Lakini siyo kitu chenye ukubwa wa kutisha, yeyote anaweza kujifunza na kulielewa soko la hisa kisha kulitumia kuingiza kipato. Hapa kuna njia kumi za kuingiza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ITUMIE HII NGUVU YA MIUJIZA…

By | May 31, 2021

Kusoma ni nguvu ya miujiza inayoweza kuyabadili sana maisha yako. Kusoma kunakujengea mtazamo sahihi, kunaimarisha uwezo wako wa kufikiri na kufanya maamuzi na kukupa utulivu mkubwa. Kusoma pia kunaiwezesha akili yako kusafiri kwenda maeneo mbalimbali na nyakati mbalimbali hivyo kukupa uzoefu mbalimbali. Kumbuka kauli inayosema wapumbavu huwa hawajifunzi, wajinga hujifunza (more…)

2342; Muujiza Unaohitaji Sana Kuutumia…

By | May 30, 2021

2342; Muujiza Unaohitaji Sana Kuutumia… Watu wamekuwa wakiulizwa kama wakipewa nafasi ya kuchagua nguvu moja ya miujiza wangechagua ipi? Wengi hujibu kuwa na nguvu za kunyanyua vitu vizito au kuweza kuruka hewani. Hayo yamekuwa siyo majibu sahihi kwa sababu hata ukiwa na nguvu hizo hazina msaada wowote kwako. Watu wakikuona (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KINACHOKUZUIA KUISHI NDOTO ZAKO…

By | May 30, 2021

Kila mmoja wetu ana ndoto kubwa sana anazotamani kuziishi kwenye maisha yake. Lakini wengi hawaishi ndoto zao, huku wakijipa visingizio mbalimbali wakati sababu ya kweli ni moja, wanakosa ujasiri wa kuziishi ndoto hizo. Kwa kuwa kuishi ndoto kunakutaka uwe wa tofauti, bila ujasiri hutaliweza hilo. Ujasiri unatokana na kujua unachotaka, (more…)

2341; Visingizio ni vingi, sababu ni moja…

By | May 29, 2021

2341; Visingizio ni vingi, sababu ni moja… Muulize mtu yeyote kwa nini hajaanza kuziishi ndoto kubwa alizonazo na majibu huwa ni yale yale kwa wato wote; Sina muda, nimebanwa sana. Sina fedha, kipato hakitoshi. Sina ujuzi, sikupata elimu sahihi. Sina ‘koneksheni’, sijazungukwa na watu sahihi. Majibu hayo yanaweza kuonekana kama (more…)