#TAFAKARI YA LEO; UNAOSTAHILI UNACHOLIPWA…

By | May 18, 2021

Watu wengi huwa wanalalamikia kipato wanachoingiza, wakisema ni kidogo sana na siyo sahihi kwao. Wanaona wanastahili kulipwa zaidi ya hapo. Kwenye uchumi wa soko huria, unastahili kile unacholipwa, hata kama ni kidogo kiasi gani, kwa sababu kinaendana na thamani unayozalisha. Hivyo kama unataka kulipwa zaidi, wajibu wako ni mmoja, zalisha (more…)

2329; Kanuni ya kipato…

By | May 17, 2021

2329; Kanuni ya kipato… Kitapo unachoingiza kinatokaba na kanuni ya kisayansi ambayo ukiielewa na kuifanyia kazi, utaweza kukuza sana kipato chako. Kanuni hiyo ina vitu vinne muhimu sana. Kitu cha kwanza ni uhitaji wa kile ambacho unafanya. Kama unachofanya au kuuza ni hitaji la msingi la watu, watasukumwa kuja kulipata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAUMIVU NA MATESO…

By | May 17, 2021

Maumivu ni sehemu ya kawaida kwenye maisha yetu hapa duniani. Mambo huwa hayaendi kama tunavyotaka sisi na hilo huleta maumivu. Lakini mateso kwenye maisha ni kitu ambacho mtu unakichagua mwenyewe. Unachagua mateso pale unapokataa kukubaliana na ilichotokea na ambacho kipo nje ya uwezo wako au unapolazimisha kitu kiende unavyotaka wewe. (more…)

2328; Vyanzo viwili vya msongo…

By | May 16, 2021

2328; Vyanzo viwili vya msongo… Huwa tunapatwa na msongo au kwa lugha nyingine kuvurugwa pale nambo yanapokwenda tofauti na tulivyotegemea. Ni rahisi kuona kilichosababisha msongo kwako ni kile kilichotokea. Lakini hiyo siyo kweli. Kinachokusababishia msongo ni namna unavyopokea kile kilichotokea. Kwa wengi hupokea kwa aina mbili na hizo ndiyo huwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MATANGAZO SIYO MASOKO…

By | May 16, 2021

Watu wengi hudhani kutangaza biashara ndiyo kufanya masoko. Matangazo ni sehemu ya masoko ila siyo sehemu pekee. Masoko ni mfumo wa kuifanya biashara ijulikane na wateja, washawishike kununua na waendelee kuiamini biashara hata baada ya kununua. Masoko yanahusisha kila eneo la biashara kuanzia kwenye kuandaa bidhaa au huduma, kutengeneza hadithi (more…)

2327; Hatua tano za masoko…

By | May 15, 2021

2327; Hatua tano za masoko… Masoko ni sehemu muhimu ya biashara yoyote ambayo mtu anafanya. Bila masoko hakuna wateja na bila wateja hakuna mauzo. Bila mauzo hakuna faida na bila faida hakuna biashara. Hivyo unaweza kuona jinsi masoko yalivyo kiuongo muhimu kwenye biashara. Wengi wanashindwa kwenye biashara kwa sababu hawana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VIASHIRIA VIKO WAZI…

By | May 15, 2021

Huwa tunawalalamikia watu kwamba wamebadilika, wakati tunaanza nao mahusiano au ushirikiano walikuwa namna fulani ila baadaye tunaona wamebadilika na kuwa kikwazo. Ukweli ni kwamba watu siyo wamebadilika, bali wameonesha uhalisia wao, wamekuwa hawawezi tena kuendelea kuficha uhalisia wao. Lakini tangu awali, kuna viashiria ambavyo watu walikuwa wanatuonesha ambapo kama tungevizingatia, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; EPUKA HUU MTEGO…

By | May 14, 2021

Kuna watu falsafa yao ya kutafuta fedha ni wanachoangalia ni kama fursa inaingiza fedha, hawajali fedha hizo zinapatikanaje, wao kama kitu kina faida wanafanya. Watu hawa hujikuta wananasa kwenye fursa ambazo zinaingiza faida kubwa siyo kwa sababu zina thamani ambayo watu wananufaika nayo, bali kwa sababu zina uhaba. Kwa uhaba (more…)