#TAFAKARI YA LEO; HUWEZI KUJISIFIA HEKIMA…

By | May 13, 2021

Unaweza ukawaambia watu kwamba umesoma vitabu vingi au unajua mambo mengi sana. Lakini huwezi kuwaambia watu kwamba una hekima kubwa. Hekima ni kitu ambacho watu wanakiona kwako, kutokana na jinsi unavyoyatumia maarifa ambayo umeyapata. Hivyo pata maarifa mengi uwezavyo, ila yatumie kujijengea hekima, kwa kuyaweka kwenye matendo yale uliyojifunza. Hakuna (more…)

2324; Maarifa Na Hekima…

By | May 12, 2021

2324; Maarifa Na Hekima… Huwezi kuwa na hekima bila ya kuwa na maarifa, lakini unaweza kuwa na maarifa usiwe na hekima. Maarifa ni kujua vitu vingi, hekima ni kujua jinsi ya kutumia maarifa hayo. Maarifa unayapata, ila hekima unaishi. Maarifa yanakusanywa, ila hekima inanolewa. Unaweza kuyapoteza maarifa lakini hekima inadumu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAKATI WA MABADILIKO…

By | May 12, 2021

Ili kupata matokeo ya tofauti kwenye maisha yako, lazima ubadilike. Lakini mabadiliko siyo rahisi kwa sababu yanakwenda kinyume na mazoea na hatuna uhakika ni matokeo ya aina gani yatakuja. Mabadiliko yanatisha unapoyakaribia na ni rahisi kuyatoroka. Unapaswa kuwa na mkakati wa kukuwezesha kuyakabili mabadiliko ili uweze kupata matokeo ya tofauti. (more…)

2323; Mambo ya kuzingatia wakati wa mabadiliko

By | May 11, 2021

2323; Mambo ya kuzingatia wakati wa mabadiliko magumu… Kila mtu huwa anapitia kipindi cha mabadiliko magumu kwenye maisha yake. Ni katika vipindi hivyo ndipo wanaofanikiwa na wanaoshindwa wanapotengana. Wanaofanikiwa wanavitumia vipindi vya mabadiliko vizuri, huku wanaoshindwa wakivitumia vibaya. Haya ni mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa mabadiliko magumu ili yakupeleke (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HEKIMA NA UPUMBAVU….

By | May 11, 2021

Hekima na upumbavu ni vile vile tangu enzi na enzi, hakuna kipya kwenye hayo. Mabadiliko yapo kwa namna vinatumika kwenye enzi husika. Wenye hekima wamekuwa wanafanya mambo yale yale huku wapumbavu pia wakifanya yale yale. Huna haja ya kuja na hekima au upumbavu mpya, angalia tu namna wengine wamekuwa wanaishi (more…)

2322; Hekima mpya na upumbavu mpya…

By | May 10, 2021

2322; Hekima mpya na upumbavu mpya… Watu wenye hekima wa vizazi vyote wamekuwa wakisema mambo yale yale. Na hayo ndiyo mambo sahihi ambaye yeyote akiyazingatia anakuwa na maisha bora. Hakuna hekima mpya ni zile zile ila zinaboreshwa kuendana na kizazi husika. Kujijua wewe mwenyewe, kuishi kusudi la maisha yako, kuwatendea (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA HUWAAMBII WATAJUAJE?

By | May 10, 2021

Kama watu wanakufanyia vitu ambavyo vinakuudhi ni kwa sababu labda hawajui kama vitu hivyo vinakuudhi au wanafanya makusudi. Lakini kwa sehemu kubwa wanakuwa hawajui. Na wewe huwaambii, unategemea wawe wanajua wenyewe, kitu ambacho hakitokei. Chochote unachotaka watu wajue kuhusu wewe, waambie wewe mwenyewe. Ili wanapofanya tofauti na unavyotaka, ujue wazi (more…)

2321; Usiyazungushe maisha…

By | May 9, 2021

2321; Usiyazungushe maisha… Maisha ni magumu tayari, hivyo usiyafanye kuwa magumu zaidi ya halivyo. Usiyazungushe sana maisha kwa vitu ambavyo viko wazi kabisa. Kama kuna kitu unakitaka, kitake kweli na weka wazi kwamba unakitaka. Usilete michezo au mitego ukitaka wengine waweze kusoma mawazo yako wajue unataka nini. Wewe ndiye wa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNACHOWASHAURI WENGINE KINAKUATHIRI NA WEWE…

By | May 9, 2021

Huwa kuna kichekesho cha mtu alienda kuchota maji kisimani akakuta kuna watu wengi. Akatafuta mbinu ya kuwadanganya ili waondoke na aweze kuchota maji. Hivyo akawaambia mbona nyie mko hapa wakati kuna gari linatoa zawadi nzuri liko kule? Watu hao wakamuuliza unasema kweli? Akajibu ni kweli kabisa, wengine wanajipatia zawadi na (more…)

2320; Unapowashauri wengine, unajishauri

By | May 8, 2021

2320; Unapowashauri wengine, unajishauri mwenyewe… Watu wengi huogopa kutoa ushauri kwa wengine kwa kujiona hawajastahili kufanya hivyo. Wengi hudhani ili uweze kutoa ushauri basi lazima uwe na uzoefu mkubwa kwenye eneo hilo. Lakini hiyo siyo sahihi, unaweza kutoa ushauri hata kama huna uzoefu mkubwa kwenye jambo hilo. Kwa sababu unapomshauri (more…)