#TAFAKARI YA LEO; SIYO UNACHOPATA, BALI UNAVYOKUWA….

By | May 8, 2021

Manufaa makubwa ya safari ya mafanikio siyo kile unachopata unapokuwa umefanikiwa, bali aina ya mtu unayekuwa baada ya kuwa umefanikiwa. Safari ya mafanikio itakubadili sana wewe kwa kiwango kikubwa, itakufanya uwe bora kuliko ulivyo sasa. Hivyi kaa kwenye safari hii, siyo kwa sababu utapata vitu fulani, ila kwa sababu utakuwa (more…)

2319; Manufaa Mengine Ya Safari Ya Mafanikio…

By | May 7, 2021

2319; Manufaa Mengine Ya Safari Ya Mafanikio… Mtu mmoja aliyefanikiwa sana aliwahi kuulizwa kama kufika kwenye kilele cha mafanikio kumempa hali ya kuridhika, kama kumekuwa kama alivyotarajia. Akajibu hapana. Akaulizwa tena ana ushauri gani kwa wale wanaopambana na safari ya mafanikio, hasa kwa uzoefu wake wa kufikia mafanikio lakini asiridhike (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISUBIRI KUANZA KUISHI…

By | May 7, 2021

Maisha ndiyo haya haya, usiyapoteze kwa kusubiri mpaka kila kitu kiwe tayari ndiyo uanze kuyaishi. Kufanya hivyo ni kuchagua kuyapoteza maisha yako. Maisha yako tayari yamekamilika kwa ndani, hupaswi kusubiri chochote cha nje ili kuanza kuyaishi. Ishi sasa vile unavyotaka, kwa maisha halisi kwako na chochote unachoona bado hujawa nacho (more…)

2318; Kitu rahisi kuahirisha…

By | May 6, 2021

2318; Kitu rahisi kuahirisha… Huwa tunajifunza sana kuhusu madhara ya tabia ya kuahirisha mambo. Pale unapopanga utafanya kitu fulani halafu wakati wa kutekeleza ulichopanga unapofika hufanyi hivyo. Tabia hii ni kikwazo kwa mafanikio ya wengi. Kwa sababu muda unapotea ambao hauwezi kurudi tena. Kuna kitu kingine ni rahisi kuahirisha, lakini (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FURAHA ISIWE LENGO….

By | May 6, 2021

Njia ya uhakika ya kuikosa furaha ni kuweka malengo ya kupata furaha kupitia yale unayofanya. Utapambana kuyafanya lakini hutapata furaha au ukipata itakuwa ya muda mfupi tu. Furaha haitafutwi au kukimbiliwa, bali furaha huwa inavutiwa na namna mtu anayaishi maisha yake na kufanya mambo yake. Unapojisalimisha kufanya kitu kikubwa kuliko (more…)

2317; Kukimbiza Kipepeo…

By | May 5, 2021

2317; Kukimbiza Kipepeo… Kutafuta furaha kwenye maisha ni sawa na kumkimbiza kipepeo. Kadiri unavyomkaribia ndivyo anavyozidi kukimbia zaidi. Lakini usipomkimbilia kipepeo, ukiwa ‘bize’ na mambo yako mengine, unashangaa kipepeo anakufuata mwenyewe. Ukifanya kitu kwa sababu unategemea kupata furaha unaishia kutokuipata furaha, hata kama umekikamilisha inavyopaswa. Lakini unapokuwa ‘bize’ kufanya kitu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KILE UNACHOFANYA…

By | May 5, 2021

Ndiyo mchango wako katika kuifanya dunia kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi. Kwa kukifanya vizuri na kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuongeza thamani kubwa kwa wengine, unakuwa umetoa mchango mkubwa sana. Hata kwa misaada, utasaidia wengi kwa kufanya kazi au biashara yako vizuri, kutengeneza kipato kikubwa na kukitoa (more…)

2316; Mchango Wako Ni Kupitia Kazi Yako…

By | May 4, 2021

2316; Mchango Wako Ni Kupitia Kazi Yako… Kila mtu ana ndoto ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi kwake na kwa watu wengine. Kila mtu anapenda kuwasaidia wale wenye uhitaji kwenye maisha. Lakini wengi huvurugwa katika kutekeleza mipango hiyo. Wengi huhangaika na mambo yasiyo sahihi katika kutimiza malengo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIKWAZO NI MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI…

By | May 4, 2021

Kutokufanikiwa kwako hakutokani na kukosa rasilimali, bali kunatokana na matumizi mabaya ya rasilimali ambazo tayari unazo. Mfano rasilimali kubwa kabisa ni muda na nguvu zako. Kila siku una masaa yale yale 24, kama hufanikiwi siyo kwa sababu umepunjwa muda, ila kwa sababu unautumia vibaya, kwa mambo yasiyo na tija. Kadhalika (more…)

2315; Uchoshi Ndiyo Mafanikio…

By | May 3, 2021

2315; Uchoshi Ndiyo Mafanikio… Kama huwezi kuukubali uchoshi (boredom) na kuishi nao, huwezi kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Mafanikio ni marudio ya muda mrefu ya vitu vinavyoboa. Wengi hufikiri mafanikio ni matokeo ya tukio moja kubwa la kishujaa, lakini sivyo. Fikiria kwenye fedha, wengi tunapenda hadithi za mtu aliyetoka (more…)