#TAFAKARI YA LEO; KUMILIKI KAZI…

By | May 3, 2021

Kazi ndiye rafiki wa kweli, rafiki atakayekufikisha kwenye mafanikio makubwa lakini pia asiyekuwa na wivu wala kukatisha tamaa. Lakini kazi zote hazifanani, kuna kuifanya kazi husika, kuyasimamia wanaofanya kazi na kumiliki kazi inayofanyika. Japo zote ni kazi, ila kiwango cha malipo kinatofautiana sana. Wewe kazana uwe mmiliki wa kazi inayofanyika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAAMUZI YA MAKUBALIANO…

By | May 2, 2021

Maamuzi ya kufanya kwa makubaliano ili kumridhisha kila mtu huwa maamuzi mabovu sana kwako. Maamuzi yoyote yanayofikiwa na kundi kubwa la watu huwa ni maamuzi ya kawaida na hata utekelezaji wake huwa siyo mzuri. Maamuzi yanapaswa kusimama kwenye ukweli na siyo kumridhisha kila mtu. Ili ufanikiwe, lazima uwe tayari kufanya (more…)

2313; Maamuzi Ya Kamati…

By | May 1, 2021

2313; Maamuzi Ya Kamati… Huwa kipo kichekesho kwamba kamati ni kikundi cha watu wasio na uwezo na ambao hawapo tayari waliopewa jukumu lisilokuwa muhimu. Maamuzi yanayofanywa na kamati ni yale ambayo mtu mmoja hataki kulaumiwa kwa maamuzi anayofanya. Hilo hupelekea maamuzi yanayofikiwa na kamati kuwa ya kubembelezana na siyo yanayosimamia (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI MAAMUZI YAKO…

By | May 1, 2021

Pale maisha yako yalipo sasa ni matokeo ya maamuzi ambayo umefanya siku za nyuma. Hata kutokufanya maamuzi ni sehemu ya maamuzi, kwa sababu unakuwa umeruhusu wengine ndiyo wakufanyie maamuzi. Na ukifanya maamuzi halafu usichukue hatua nayo pia ni maamuzi umefanya kutokuchukua hatua na yamekufikisha ulipo sasa. Njia pekee ya kuyabadili (more…)

2312; Ukishafanya Maamuzi…

By | April 30, 2021

2312; Ukishafanya Maamuzi… Kinachofuata ni kuyatekeleza, kujifanyia tathmini na kuboresha kadiri unavyokwenda. Na siyo kuanza kuyahukumu maamuzi yako mwenyewe baada ya kuwa umeyafanya, hata kama umekosea kwenye kuyafanya, kujihukumu haitasaidia. Bali unapaswa kujitathmini na kuyaboresha. Pia siyo kupoteza muda kutaka kila mtu aelewe na kukubaliana na maamuzi hayo. Wengi hawataelewa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA HAWAKUELEWI NI SAWA…

By | April 30, 2021

Kama watu wanakulalamikia kwamba hueleweki, hawayaelewi maisha yako hilo lisikusumbue sana. Maana hakuna yeyote anayeiona dunia kwa namna unavyoiona wewe. Imani, mtazamo, fikra na uzoefu ulionao ni wa kipekee, ukiishi kwa kuzingatia hayo, utakuwa tofauti kabisa na wengine. Na kuwa tofauti haimaanishi unakosea, bali inamaanisha unafanya kilicho sahihi kwako. Watu (more…)

2311; U mpweke…

By | April 29, 2021

2310; U mpweke… Umewahi kutamani watu wakione kitu kwa namna fulani unavyokiona wewe lakini wanashindwa kufanya hivyo? Umewahi kuwa na hisia fulani kwenye jambo lakini wengine wakawa na hisia tofauti unayoshindwa kuielewa? Unapojikuta kwenye hali hiyo usione kama una tatizo, bali tambua ndivyo kila mtu alivyo. Kila mmoja wetu anaiona (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTULIVU WA MAISHA…

By | April 29, 2021

Utulivu wa maisha huwa unaanzia kwenye utulivu wa fikra. Kama fikra hazijatulia, maisha pia hayawezi kutulia. Kwa fikra kuzurura hovyo, kunapelekea mtu kupatwa na msongo wa mawazo. Kuzidhibiti fikra zako zikae kwenye kile unachofanya kwa wakati husika ni njia bora ya kutengeneza utulivu wa maisha yako. Anza sasa kudhibiti na (more…)

2310; Njia ya kupunguza msongo…

By | April 28, 2021

2310; Njia ya kupunguza msongo… Chanzo kikuu cha msongo wa mawazo huwa ni kuyaruhusu mawazo yazurure yatakavyo. Unakuwa unafanya kitu kimoja, ila mawazo yako yako kwenye kitu kingine tofauti kabisa. Kwa mawazo yako kuzurura, yanatengeneza kitu kisichokuwepo, wakati kilicho mbele yako hukofanyi vizuri. Kinachotokea ni muda unakuwa umeisha, umejipa hofu (more…)