#TAFAKARI YA LEO; NI BORA USINUFAIKE KULIKO KUTOKUCHUKUA HATUA…

By | November 27, 2020

“It is better, however, to get no return than to confer no benefits. Even after a poor crop one should sow again; for often losses due to continued barrenness of an unproductive soil have been made good by one year’s fertility.” – Seneca Mkulima wa kweli, ambaye ameyatoa maisha yake (more…)

2157; Ni Vyote Kwa Pamoja, Kipato Na Matumizi…

By | November 26, 2020

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020 mwanamafanikio mwenzetu Simeon Shimbe aliuliza; walimu wengi wa mambo ya fedha wanasisitiza zaidi mtu kuongeza kipato na siyo kupunguza matumizi, lakini kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA umesisitiza zaidi kupunguza matumizi, hiyo ikoje? Nilimjibu ni kweli kuongeza kipato ni msingi muhimu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPENDO HUBADILI KILA KITU…

By | November 26, 2020

“When we love, we always strive to become better than we are. When we strive to become better than we are, everything around us becomes better too.” — Paulo Coelho Unapopenda, unakazana kuwa bora kuliko ulivyokuwa awali. Unapokazana kuwa bora, kila kinachokuzunguka kinakuwa bora pia. Hivyo njia rahisi ya kubadili (more…)

2156; Ya Kila Mtu, Haina Mtu…

By | November 25, 2020

Moja ya sababu zinazopelekea mifumo ya kijamaa kushindwa ni kukosekana kwa uwajibikaji kwenye maeneo yanayotumia mfumo huo. Kwa kuwa kila kitu ni mali ya kila mtu, inakuwa vigumu kuwajibisha watu. Mtu anakuwa na uchungu pale kitu kinapokuwa chake, kuliko kinapokuwa cha wengine. Kwa kuwa kwenye mifumo ya ujamaa kila kitu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TABIA INATENGENEZWA KWA VITENDO…

By | November 25, 2020

“Every habit and capability is confirmed and grows in its corresponding actions, walking by walking, and running by running… therefore, if you want to do something, make a habit of it.” – Epictetus Kila tabia huwa inajengwa na kuimarishwa kwa vitendo, kupitia hatua ambazo mtu anachukua. Kwa kujua hili, tunaweza (more…)

2155; Fanya Kama Unatoa Zawadi…

By | November 24, 2020

Safari ya mafanikio, kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha mara kwa mara, ni ya muda mrefu, inahitaji msimamo na uvumilivu mkubwa. Hali hiyo inakaribisha uchovu, kwa sababu siyo kawaida kwetu binadamu kufanya kitu kwa muda mrefu, hasa pale unapohitajika kukazana kuwa bora kila wakati. Tumekuwa tunashirikishana njia nyingi za kukabiliana na uchovu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WANAOLALAMIKIA KILA KITU…

By | November 24, 2020

“Those who are not grateful soon begin to complain of everything.” — Thomas Merton Watu wanaolalamikia kila kitu kwenye maisha yao, ni watu ambao hawana shukrani. Ukiwa mtu wa shukrani, kuna mambo mengi ya kushukuru kwenye maisha kuliko kulalamika. Hata pale unapokutana na magumu, ukiwa mtu wa shukrani, hutakosa cha (more…)

2154; Ni Kurudia Rudia…

By | November 23, 2020

Nguvu ya asili ipo kwenye msimamo na kurudia rudia. Hakuna chochote ambacho asili inafanya mara moja na kuacha, bali hurudia kwa muda mrefu na hapo ndipo matokeo makubwa hutengenezwa. Chukua mfano wa tone la maji, moja pekee haliwezi kuleta madhara yoyote, lakini tone hilo linapojirudia mara nyingi, linaweza kuvunja mwamba (more…)

2153; Ni Msukumo Kutoka Ndani Au Wivu?

By | November 22, 2020

Kikwazo kikubwa kinachowazuia watu kufanikiwa kwenye jambo lolote lile wanalofanya, ni kuanza kwa sababu zisizo sahihi. Iwe ni kazi ambayo mtu amechagua kufanya au biashara, kuna sababu kuu mbili za mtu kuingia kwenye kitu hicho. Sababu ya kwanza ni mtu kupenda kitu hicho kutoka ndani yake au kukichagua na kuwa (more…)