2154; Ni Kurudia Rudia…

By | November 23, 2020

Nguvu ya asili ipo kwenye msimamo na kurudia rudia. Hakuna chochote ambacho asili inafanya mara moja na kuacha, bali hurudia kwa muda mrefu na hapo ndipo matokeo makubwa hutengenezwa. Chukua mfano wa tone la maji, moja pekee haliwezi kuleta madhara yoyote, lakini tone hilo linapojirudia mara nyingi, linaweza kuvunja mwamba (more…)

2152; Unalipa Sasa Au Utalipa Baadaye?

By | November 21, 2020

Kwenye maeneo mbalimbali yanayotoa huduma hasa za starehe, huwa yana taratibu zinazotofautiana za malipo. Kuna eneo ukienda unalipa kwanza ndiyo upewe huduma, wakati eneo jingine unapata huduma kwanza halafu unalipa mwisho. Kwa vyovyote vile huduma utapata, lakini lazima utalipia. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu, kuna gharama za kulipa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KILA KITAKACHOTOKEA KITAKUWA CHENYE MANUFAA KWAKO…

By | November 21, 2020

“Do not be concerned too much with what will happen. Everything which happens will be good and useful for you.” — Epictetus Mara nyingi umekuwa unahofia kuhusu mambo yanayoweza kutokea siku zijazo. Hofu hizo zimekuwa zinakuzuia usichukue hatua ulizopanga kuchukua. Na hilo linakuwa kikwazo kwa mafanikio yako. Kitu muhimu unachopaswa (more…)

2151; Kukubali Kutokukubaliana…

By | November 20, 2020

Mara nyingi watu wamekuwa wanashangaa nawezaje kukubaliana na kila mtu, hata kama anaamini na kusimamia kile ambacho ni tofauti kabisa na mimi. Nina mifano mingi ya namna ambavyo watu wamekuwa wanashangazwa na hilo na hata wengine kukasirishwa. Mfano tunaweza kuwa tunajadiliana jambo, ambapo niko upande fulani, halafu baada ya muda (more…)

2150; Nguvu Unazozitawanya Hovyo…

By | November 19, 2020

Nguvu, muda na pesa ni rasilimali muhimu sana kwenye safari ya mafanikio. Muda tumekuwa tunauzungumzia sana, jinsi ambavyo unapaswa kutumia fedha kuokoa muda badala ya kutumia muda kuokoa fedha. Tumejifunza sana kuhusu ukomo wa muda, kwamba ukishapotea haurudi tena, hivyo tunapaswa kuwa na ubahili nao kuliko tunavyokuwa na ubahili na (more…)