2117; Uhuru Wa Kweli Ni Ule Unaoujenga Mwenyewe…

By | October 17, 2020

Hakuna uhuru unaopatikana kwa kutegemea wengine, unaweza kuona kuna uhuru kwenye hilo lakini ni swala la muda tu kabla watu hao unaowategemea hawajaja na masharti yao, ambayo yanaweza kuwa kikwazo kwako. Tuchukue mfano mzuri wa mitandao ya kijamii, wakati inakuja kila mtu alishangilia kwamba sasa mawasiliano yana uhuru kamili. Huhitaji (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTAPIMWA KWA VIWANGO VYAKO MWENYEWE…

By | October 17, 2020

“In the world people take a man at his own estimate; but he must estimate himself at something. Disagreeableness is more easily tolerated than insignificance.” – Johann Wolfgang von Goethe Watu huwa wanakuchukulia kwa namna unavyojichukulia wewe mwenyewe. Kama unajiheshimu basi pia watu watakuheshimu. Na kama unajidharau na wao pia (more…)

2116; Kizazi Laini Laini…

By | October 16, 2020

Mtu mmoja amewahi kusema kama watu wanaoishi sasa watachukuliwa na kurudishwa kwenye aina ya maisha ambayo watu waliishi kwenye karne ya kwanza, basi karibu wote watafariki kwa haraka sana. Hii ni kwa sababu mazingira ya sasa ni rahisi sana ukilinganisha na mazingira ya kipindi hicho. Mazingira hayo rahisi yamefanya sehemu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIKIMBILIE KUCHUKUA HATUA UKIWA NA HASIRA…

By | October 16, 2020

“The cause of anger is the sense of having been wronged, but one ought not trust this sense. Don’t make your move right away, even against what seems overt and plain; sometimes false things give the appearance of truth.” – Seneca Hasira huwa ni zao la hisia, pale unapoamini kwamba (more…)

2115; Unapokuwa Njia Panda, Iangalie Asili…

By | October 15, 2020

Asili huwa inajiendesha kwa kanuni zake yenyewe na haijawahi kushindwa kwenye hilo. Kila kitu kinaenda kwa taratibu zake na asili haina uonevu wala upendeleo. Asili haina wema wala ubaya, bali inaenda kwa namna ambayo ni bora kwa asili kwa ujumla. Simba kumla swala inaweza kuonekana ni uonevu kwa swala, lakini (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISUBIRI HAMASA, ANZA KUFANYA…

By | October 15, 2020

“Amateurs sit and wait for inspiration, the rest of us just get up and go to work.” – Stephen King Kitu kikubwa kinachowatofautisha wabobezi na wachanga ni hamasa. Wachanga huwa wanasubiri hamasa ije ndiyo waanze kufanya. Na kwa sababu hamasa haitabiriki wala haitegemeki, huwa wanachelewa kuanza kufanya na hivyo hawafanyi (more…)

2114; Linda Rasilimali Hizi Tano…

By | October 14, 2020

Wale wanaofanya makubwa kwenye maisha yao siyo kwamba wana tofauti kubwa sana na wanaoshindwa kufanya makubwa. Bali wanajitambua zaidi kuliko wengine. Na katika kujitambua kwao, wanazijua rasilimali muhimu za kulinda ili waweze kufanya makubwa. Hizo ni rasilimali ambazo zikipotea huwa zina madhara makubwa ya kumzuia mtu asipige hatua. Rasilimali hizi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO ULIPOSIMAMA, BALI UNAKOELEKEA…

By | October 14, 2020

“The great thing in this world is not so much where we stand as in what direction we are moving.” – Oliver Wendell Holmes Sr. Jambo muhimu zaidi kwenye maisha yako siyo pale uliposimama sasa, bali kule unakoelekea. Haijalishi kwa sasa uko wapi, kama upo kwenye uelekeo sahihi, utafika mahali (more…)

2113; Fanya Kitu Kuwa Bora Zaidi Ya Kilivyo Sasa…

By | October 13, 2020

Kuna watu wanaamini ushindani ndiyo njia nzuri wa kuwasukuma kufanya makubwa zaidi. Lakini hilo siyo kweli, ushindani huwa unamfanya mtu asahau kule anakotaka kufika na kuanza kuangalia wengine wanafanya nini ili kuwazidi. Kinachotokea, hata kama umewashinda wale unaoshindana nao, unakuwa umepoteza, kwa sababu hujawa wewe. Mafanikio ya kweli hayaletwi na (more…)