Utaratibu Wa Kupata Kitabu Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

By | October 21, 2016

Habari rafiki yangu katika mafanikio?
Nichukue nafasi hii kukupa habari njema ya kwamba kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA, jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa sasa kinapatikana katika mfumo wa kuchapishwa. Mwanzo kitabu hiki kiliatikana katika mfumo wa nakala tete (softcopy) ila sasa unaweza kukipata kama kitabu cha kawaida, na kuweza kukisoma popote ulipo.

Ni kitabu kizuri sana kwa wale wote ambao wanapenda kuanzisha na kukuza biashara zao. Kitabu kinaitwa biashara ndani ya ajira, lakini siyo kwa wale waliopo kwenye ajira pekee. Kitabu hiki kinamfaa mtu yeyote anayetaka kuanzisha na kukuza biashara yake, iwe ameajiriwa au la.

Ndani ya kitabu hiki kuna mambo muhimu sana utakayojifunza kama;
1.     Jinsi ya kupangilia muda wako vizuri na kuweza kuudhibiti na kuutumia vizuri.
2.     Biashara unazoweza kuanza kufanya kama bado hujaanza kufanya.
3.     Uwekezaji unaweza kuanza kufanya sasa, ili miaka ijayo uweze kuwa na uhuru wa kifedha.
4.     Mifereji nane ya kipato unayohitaji kutengeneza ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha.
5.     Jinsi ya kutengeneza mfumo bora wa kuendesha biashara yako ili kupata uhuru.
6.     Hatari za kuepuka ili biashara yako ifanikiwe.
7.     Na mengine mengi…

Kama unavyoona hapo, siyo kwa wale walioajiriwa pekee, bali kila mtu ana kitu cha kujifunza kupitia kitabu hiki.
Nakushauri sana rafiki yangu, pata na usome kitabu hiki, hutabaki kama ulivyo sasa.

Utaratibu wa kupata kitabu hiki.

Kwa sasa kitabu kinapatikana kwangu, hivyo kwa wale waliopo dar, unaweza kufika ofisini kwangu Tabata Kimanga na kupata nakala yako ya kitabu, au kulipia kitabu na kuletewa pale ulipo. Utaratibu wa kukiweka kitabu hiki kwenye maduka ya vitabu unaendelea, na taarifa nitawapatia.
Kwa wale waliopo mikoani, kitabu kinatumwa kwa njia ya basi, hivyo unalipia gharama ya kitabu na nauli kisha unatumiwa kitabu kule ulipo. Utaratibu wa kuwapata mawakala kwenye mikoa mbalimbali unaendelea na nitawapa taarifa kadiri tunavyokwenda.

Gharama ya kitabu na namna ya kukipata.

Gharama ya kitabu ni tsh elfu 10 (10,000/=).
Kama upo dar fika ofisini tabata kimanga, utapata nakala yako. Pia unaweza kufanya malipo ya tsh elfu 10 kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253 na kisha kutuma taarifa zako na ukaletewa kitabu pale ulipo.

Kama upo mkoani, utahitajika kutuma gharama za nauli ya kusafirisha kitabu. Hivyo tuma gharama ya kitabu tsh elfu 10 pamoja na nauli tsh elfu 5 (jumla tsh 15,000/=) kwa mpesa 0755 953 887 au tigo pesa 0717 396 253 kisha tuma taarifa zako, majina kamili, namba ya simu na sehemu ulipo, kisha utatumiwa kitabu hiki.

Kwa baadhi ya mikoa mawakala wanapatikana kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini;

Mawakala wa kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA

Mawakala wa kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA

MUHIMU; Kitabu pia kinapatikana kwenye mfumo wa softcopy yaani pdf na kinatumwa kwa njia ya email. Kupata softcopy tuma fedha, tsh 10,000/= kwenye namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kisha tuma ujumbe wenye email yako kwenye moja ya namba hizo na utatumiwa kitabu.

Karibu sana upate maarifa haya muhimu kwa maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Category: VITABU

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.