UKURASA WA 755; Ushindi Kwa Mteja Wako…

By | January 24, 2017

Kwanza kila mmoja wetu ana mteja, iwe una biashara au la, iwe umeajiriwa au umejiajiri, kuna mtu ambaye unategemea apokee kile unachofanya, au unachosema au unachoandika, vyovyote vile. Kila mtu ana mtu ambaye anamtegemea kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa faida au siyo kwa faida.

Kitu cha kwanza kabisa tunachopaswa kujua kuhusu wateja wetu ni tabia zao. Tunapaswa kujua tabia zinazowasukuma kuja kwetu. Tunapaswa kujua kwamba watu hawaji kwa sababu wametuona tunafanya, ila wamekuja kwa sababu kuna kitu kimewasukuma kuja. Kwamba wana mahitaji au matatizo.

Kitu kimoja muhimu unapaswa kufanya kwa wateja wako ni kuwapa ushindi, kila mtu anapenda ushindi, kila mtu anataka kushinda. Na ushindi ni tofauti kwa kila anayekuja kwenye kile unachofanya. Ushindi ni kuondokana na changamoto mtu aliyonayo au kupata mahitaji yake.

SOMA; Unapimaje Ushindi Kwenye Maisha Yako?

Hivyo kazi yako kubwa ni kutoa ushindi kwa wateja wako, wape watu ushindi na watakuja zaidi na zaidi. Hakuna asiyependa ushindi, ushindi ni mzuri, ushindi unamfanya mtu ajisikie vizuri, ajione wa thamani.

Kila unachofanya kwenye kazi au biashara yako, fikiria kitu kimoja kikuu, ninampaje mteja ushindi? Hili ndiyo swali la kujiuliza kila siku, hili ndilo swali linalopaswa kuongoza maamuzi yako kila siku kwenye lile ambalo unafanya.

Ni ushindi gani ambao unampa mteja wako?

Weka ushindi zaidi kwa wateja wako, na biashara yoyote unayofanya itakuwa na faida, kazi yoyote unayofanya itakuwa na maana kwako na kipato kitaongezeka. Yote hayo ni kutokana na ushindi wanaopata wateja wako.

Nenda kampe mteja ushindi mkubwa leo.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.