UKURASA WA 761; Ukweli Haulazimishwi…

By | January 30, 2017

Ukweli huwa unabaki kiwa ukweli, haulazimishwi wala haubembelezwi, bali unakuwa wazi na kila mtu anajionea mwenyewe.

Ukiona mtu analazimisha ukweli, jua kuna kitu kinafichwa ndani yake. Ukiona wewe mwenyewe unalazimisha ukweli ili watu waamini kwenye kile unachotaka waamini, basi jua kuna shida mahali. Na shida kubwa ni kwamba siyo ukweli, bali kuna kitu kimefichika.

Ukweli unaweza kufichwa kwa muda, ila ipo siku unabaki wazo hadharani na hapo hakuna awezaye kuuficha tena.

Unachohitaji wewe ni kuishi maisha yako ya kweli, kufanya kile ambacho unaweza kufanya na kutimiza kile ambacho umeahidi. Kwa njia hii utafika popote unapotaka kufika na hutakuwa na hofu ya watu kujua unachoficha.

SOMA; Waambie Ukweli Uwapoteze

Wengi wamekuwa wakiishi uongo na kulazimisha uonekane kama ukweli kwa nje.

Watu ambao wanajaribu kuishi maisha ya juu kuliko uwezo wao kwa wakati huo, wanalazimika kuingia kwenye mikopo ambayo inawaumiza zaidi baadaye. Wengine wamekuwa wakidanganya namna wanavyofanya kazi, kwa nje wanataka waonekane ni wafanyakazi hodari ila wanapokuwa kwenye kazi zao wanatafuta kila njia ya kukwepa majukumu yao. Na hilo linaonekana wazi kwenye maisha wanayoenda nayo, yanakuwa siyo bora kama ambavyo yangekuwa ikiwa wangefanya kazi kwa uhodari.

Sehemu kubwa ya dunia wanaigiza, wanajaribu kulazimisha ukweli ambao haupo na ndiyo maana watu wengi wanaingia kwenye matatizo ambayo ni ya kujitakia wenyewe.

Ninachokushauri wewe mwanamafanikio mwenzangu, ni usijaribu kulazimisha ukweli, usijaribu kuficha uongo kwa kuweka ukweli kidogo nje. Kama kitu siyo kweli kitaonekana tu, haijalishi kimefichwa mbali kiasi gani.

Usilazimishe ukweli, ishi ukweli.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.