UKURASA WA 785; Njia Bora Kabisa Ya Kulalamika Ni Hii.

By | February 23, 2017

Kama unavyojua, kitu ambacho nimekuwa nakusihi mara nyingi sana usifanye ni kulalamika. Nimekuwa nakuonesha namna gani kulalamika na kulaumu wengine hakutaweza kukuletea wewe mafanikio. Kwa sababu unapoona wengine hawajafanya vile ulivyofikiri ni sahihi kwako, unakuwa umewakabidhi wao mamlaka juu ya maisha yako. Unakuwa umewaambia kwamba nyie ndiyo mnaoweza kunipa mafanikio au kuninyima.

IMG-20170217-WA0002

 

Lakini sivyo inavyopaswa kuwa, hakuna mwenye mamlaka au mwenye uwezo wa kukupa au kukunyima wewe mafanikio ila wewe mwenyewe, labda sasa ukubali kumpa mwingine mamlaka hayo.

Sasa kwa kuwa huwezi kukubaliana na kila kitu ambacho wengine wanafanya juu yako, unahitaji kuchukua hatua. Na hivyo hapa leo nakushirikisha njia bora kabisa ya wewe kulalamika, ambapo pale mtu atafanya tofauti na ulivyotegemea, uweze kupata matokeo unayotaka.

Njia bora kabisa kwako kulalamika ni kufanya kitu, kile ambacho hakijaenda kama ulivyotaka kiende. Unaamua kuchukua hatua wewe mwenyewe, ya kuhakikisha unapata kile ambacho ulikuwa unategemea kufanya.

SOMA; Njia Ya Kuwa Bora Ni Ngumu, Lakini Nzuri Kusafiri…

Wengi wamekuwa wakilalamika kwa kuongea na kurusha lawama, lakini imekuwa haiwasaidii kwa sababu maneno tu hayana nguvu. Ila unapoamua kuchukua hatua, kuna mambo mengi unabadili na inaleta matokeo ya tofauti.

Kama kuna mtu amefanya ukose kitu fulani, usipoteze muda wako kumlalamikia kwamba bila yeye mambo yako yangekuwa mazuri, badala yake toka na nenda wewe mwenyewe kahakikishe mambo yako yanakuwa mazuri.

Hutafikia mafanikio makubwa kwa kuongea ongea na kufikiri wengine watachukua hatua. Utafikia mafanikio kwa kuchoshwa na unachopata sasa, kuamua mwenyewe kuchukua hatua na kuleta majibu ya tofauti.

Hivi ndivyo watu wanavyofikia mafanikio makubwa, licha ya kuzungukwa na changamoto nyingi. Husubiri mpaka mtu akuambie, badala yake unachukua hatua mwenyewe.

Kama kuna kitu hukipendi, fanya kila uwezalo kukibadili au kuweza kukipokea kwa njia ambayo kitakuwa bora kwako.

Lalamika kwa vitendo na siyo kwa maneno.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.