UKURASA WA 838; Mmoja Kati Ya Wengi Na Mmoja Kati Ya Wachache…

By | April 17, 2017

Huyu ni mmoja kati ya wengi wanaofanya kitu hichi….

Huyu ni mmoja kati ya wachache sana wanaofanya kitu hichi….

Ni tofauti gani unaiona kwenye sentensi hizo mbili hapo juu?

IMG-20170306-WA0003

Mmoja kati ya wengi.

Unapokuwa mmoja kati ya wengi, unakuwa katikati ya kundi kubwa la watu ambao wanafanya kile ambacho unakifanya wewe, huenda kwa namna ile ile ambayo unaifanya wewe.

Kwa kuwa mmoja kati ya wengi, hali ya hewa inaweza isiwe nzuri sana, kwa wingi wa wanaofanya, unashindwa kujitofautisha na kuwa wa kipekee. Hii inapelekea kushindwa kufanikiwa na kuishia kuwa kawaida, kwa sababu wengi wapo kawaida.

Unapokuwa mmoja kati ya wafanyabiashara wengi mnaofanya biashara fulani, maana yake mnagawana wateja waliopo na inafika hatua huwezi kwenda zaidi ya pale. Unakuwa umechagua njia ambayo hata uende kasi kiasi gani, bado huwezi kufika mapema zaidi.

SOMA; Ushindi Kwa Mteja Wako…

Mmoja kati ya wachache.

Unapokuwa mmoja kati ya wachache, maana yake unafanya kitu ambacho kinafanywa na watu wachache sana. Hapa unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweza kufikia mafanikio makubwa kwa sababu hali ya hewa inakuwa nzuri, na wale wanaotegemea unachofanya ni wengi huku wafanyaji ni wachache. Unakuwa na fursa kubwa ya kukua na kufanya makubwa zaidi.

Unapofanya biashara ambayo wewe ni mmoja kati ya wachache wanaofanya, maana yake una wateja wengi wanaokutegemea, una uwezo wa kukua zaidi ya ulivyo sasa na ushindani ni mdogo. Unaweza kuweka rasilimali zako kwenye ukuaji zaidi na siyo kwenye kushindana.

Unawezaje kuwa mmoja kati ya wachache?

Angalia kile ambacho wengine hawaangalii, fanya kile ambacho wengine hawafanyi, na muhimu zaidi fanya vitu vigumu. Wengi wanapenda kufanya vitu rahisi, hivyo vigumu vinakuwa na wachache na ndipo hazina kubwa ilipo.

Watu wanapenda kuanza biashara rahisi, biashara ambazo tayari zinafanywa na kila mtu. Kweli wanakuwa na biashara ambazo ni za uhakika, na hatari ya kushindwa ni ndogo, lakini sasa ushindani ni mkali na hata wakiweka juhudi, kuna kiwango hawawezi kuvuka.

Usiangalie urahisi, angalia kipi cha tofauti unachoweza kufanya. Fedha inafuata tofauti, hivyo kadiri unavyoweza kutengeneza tofauti, ndivyo unavyoweza kutengeneza fedha.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.