UKURASA WA 849; Kuhodhi Ukweli…

By | April 28, 2017

Kuna vitu vingi kwenye maisha ambavyo watu wanaweza kuhodhi, na vikawapa faidia dhidi ya wengine. Kutokana na kuwahi kwao, wanazipata nafasi au fursa nzuri ambazo wanaokuja baadaye hawawezi kupata kama wao. Kwa mfano mtu ambaye anahodhi ardhi sehemu fulani, labda kwa kuwahi kwake au kwa kuinunua kwa bei rahisi mapema. Mtu huyu kadiri siku zinavyokwenda ana ardhi inavyoongezeka thamani, anazidi kuwa na faida.

IMG-20170319-WA0002

Lakini kipo kitu kimoja, chenye faida sana ambacho bado hakuna ambaye amekihodhi. Hata uchelewe kiasi gani, kitu hicho kipo wazi kwa kila mtu kukitumia kwa ajili ya mafanikio yake. Kitu hicho ni ukweli.

Hakuna anayehodhi ukweli, kwamba ukweli huu ni wangu na mimi tu ndiye ninayepaswa kuutumia, au kama unataka kuutumia lazima unilipe. Ukweli uko wazi kwa kila mtu na kila wakati, ni maamuzi tu ya mtu mwenyewe katika kuufanyia kazi ukweli uliopo na kuona matunda yake.

SOMA; Kudanganya Na Kutosema Ukweli Wote…

Ila sasa, pamoja na uwazi huu wa ukweli, bado watu hawajisumbui katika kuutafuta ukweli, bado watu wataendelea kudanganywa na kufanya maamuzi wasiyoyajua vizuri. Na kwa sababu hizo, kuna watu ambao wanaendelea kunufaika na hali hii ya watu kutokupenda kujua ukweli. Au hata kama wanapenda, basi kutokuwa tayari kujitoa ili kuujua ukweli.

Popote ulipo kwenye maisha yako, kipaumbele chako kiwe kuujua ukweli, usifanye vitu kwa mazoea, bali fanya kwa kujua kwa nini unafanya.

Ukweli ni mwingi na utaendelea kuwa huru kwa kila mtu kuutumia.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.