UKURASA WA 912; Nunua Muda Kwanza….

By | June 30, 2017

Wazungu wanasema buy some time…

Kuna wakati unajikuta kwenye hali ngumu, ambapo hujui ni maamuzi gani sahihi kufanya. Katika hali hiyo unakuwa huna taarifa za kutosha, na maamuzi yoyote ya haraka unayoweza kuchukua, yanaweza kuharibu mambo zaidi, kuliko kuyatengeneza.

Huu ndiyo wakati ambao unapaswa kununua muda kwanza, kuacha muda upite kwanza kabla hujafanya maamuzi. Kujipa muda kidogo badala ya kukimbilia maamuzi.

Lakini sasa, wakati unanunua muda hukai na kusubiri tu kama vile muujiza utatokea. Badala yake huu ni wakati ambao utafanya kazi sana, kazi kubwa mno, ila kwa chini chini.

SOMA; Tumia Muda Wako Vizuri.

Kazi kubwa utakayoifanya kwenye muda huo unaonunua ni kuchimba zaidi kwenye ile changamoto unayopitia. Kuielewa kwa kina, kujua mambo mbalimbali yanayochangia, kujua madhara yake, kujua hatua za kuchukua na kujua madhara ya kila hatua unayoweza kuchukua.

Tumia muda huo kuangalia kila namna unavyoweza kuboresha hatua unazochukua, ili ziwe na manufaa kwa wote wanaohusika, na kuweza kuleta matokeo bora.

Muhimu ni usikimbilie kufanya maamuzi kwenye jambo ambalo huna uhakika, jipe muda wa kulifanyia kazi ili uweze kuchukua maamuzi bora na yenye manufaa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.