UWEKEZAJI LEO; Vodacom Wametangaza Kutoa Gawio La Kwanza Kwa Wawekezaji.

By | October 4, 2017

Moja ya faida za kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa ni kupata gawio pale kampuni inapopata faida.

Kampuni inawalipa wanahisa wake sehemu ya faidia iliyopata, huku wakiendelea kubaki na hisa zao. Yaani ni sawa na kuweka mtaji kwenye biashara, na ukapata faida huku mtaji wako ukiendelea kuwepo.

Kampuni ya Vodacom Tanzania, ambayo imeingia kwenye soko la hisa miezi michache iliyopita, imetangaza kukusudia kutoa gawio lake la kwanza kwa wawekezaji walionunua hisa za kampuni hiyo.

voda gawio

Gawio hilo litatolewa iwapo mkutano mkuu wa mwaka utaridhia pendekezo hilo. Mkutano mkuu wa mwaka unatarajiwa kufanyika tarehe 27/10/2017.

Kiasi cha gawio ambacho Vodacom inatarajia kutoa ni shilingi 12 na senti 74 kwa kila hisa moja ya kampuni hiyo.

Hii ina maana kwamba kujua kiasi cha gawio ambacho mwekezaji unapata, unazidisha idadi ya hisa zako kwa tsh 12.74.

SOMA; UWEKEZAJI LEO; Tofauti Ya Uwekezaji Kwenye Hisa Na Hatifungani.

Iwapo hili litaridhiwa na mkutano mkuu wa mwaka, gawio hili litalipwa tarehe 30/11/2017.

Watu watakaoendelea kununua hisa mpaka tarehe 10/10/2017 watapata gawio ili. Ila watakaonunua kuanzia tarehe 11/10/2017 hawatapata hili gawio lililotangazwa kwa mwaka huu.

Gawio litalipwa kwa wawekezaji kwa njia ya benki, mpesa, tigo pesa na airtel money.

Gawio hili limekuja kipindi kifupi sana tangu watu wanunue hisa za Vodacom, hivyo ni dalili nzuri kwamba wawekezaji walionunua hisa za Vodacom wataweza kunufaika zaidi baadaye.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

One thought on “UWEKEZAJI LEO; Vodacom Wametangaza Kutoa Gawio La Kwanza Kwa Wawekezaji.

  1. Pingback: UWEKEZAJI LEO; Maana Ya Gawio Katika Uwekezaji Na Utolewaji Wake. – Kisima Cha Maarifa

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.