Maelekezo Kwa Wageni

Maelekezo Ya KISIMA CHA MAARIFA Kwa Wanachama Wageni.

Habari mwanamafanikio?

Hongera sana kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, na kuingia kwenye familia ya wanamafanikio, familia ya watu wanaochukua hatua ili kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi kila siku.

Ili kunufaika na KISIMA CHA MAARIFA, yafuatayo ni maelekezo muhimu kuhusu KISIMA CHA MAARIFA.

  1. KUNDI LA WASAP.

Kwenye kundi la wasap, kila siku tunaianza siku yetu kwa tafakari ambayo inatufikirisha na kutupa njia mpya ya kuiendea siku yetu.

Pia kila mwisho wa siku tunakuwa na mjadala wa kushirikishana yale ambayo tumejifunza kwenye siku husika, pamoja na kushirikishana changamoto mbalimbali tunazopitia. Hichi pia ni kipindi cha maswali na majibu mbalimbali.

Kila siku ya jumapili kuna DARASA LA JUMAPILI ambapo tunapata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na maisha ya mafanikio. Kupata masomo ya madarasa ya jumapili yaliyopita fungua kiungo hichi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/category/kutoka-kwa-kocha/darasa-la-jumapili/

Ni muhimu sana kushiriki kwenye mafunzo haya ya kundi la wasap ili kujifunza na kuhamasika kuchukua hatua.

  1. MTANDAO WA KISIMA CHA MAARIFA.

Mtandao wetu wa KISIMA CHA MAARIFA, www.kisimachamaarifa.co.tz una makala nyingi na muhimu za kupata maarifa ya mafanikio, kuanzia kwenye biashara na ujasiriamali, fedha na uwekezaji na hata falsafa na imani.

Kusoma makala hizi, tembelea mtandao huu kila siku kwenye www.kisimachamaarifa.co.tz

  1. SEMINA MBALIMBALI.

Semina mbalimbali ambazo nimekuwa naendesha kwa njia ya mtandao mafunzo yake yanapatikana kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

  1. SEMINA YA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/seminafedha/
  2. SEMINA YA KUANZA MWAKA 2018 KWA MAFANIKIO, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/semina2018/

 

  1. VITABU VYA KUJISOMEA.

Kupata vitabu vya kujisomea ambavyo nimeandika, fungua ukurasa huu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu/

  1. VIGEZO VYA KUENDELEA KUWA MWANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA.

Ili kuendelea kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, ada pekee haitakupa nafasi hiyo. Bali vipo vigezo saba, vyenye idadi ya alama kumi unavyopaswa kufanyia kazi. Soma vigezo hivyo hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/vigezo/

  1. HUDUMA NYINGINE ZA KOCHA MAKIRITA.

Kupata huduma nyingine ninazotoa, tembelea ukurasa huu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha/

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA,

Karibu sana tujifunze na kuchukua hatua ili kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz