VIGEZO VYA UANACHAMA

Vigezo Saba Vya Kuwa Mwanachama Wa KISIMA CHA MAARIFA.

Habari rafiki,

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Dhumuni kubwa la KISIMA CHA MAARIFA, tangu tumeanza kwama 2014 mpaka leo imekuwa kupata maarifa sahihi ya kutuwezesha kuchukua hatua na kufanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Hivyo mambo makuu ni mawili hapo;

  1. KUPATA MAARIFA.
  2. KUCHUKUA HATUA.

Kwa eneo la maarifa tunayapata mengi sana hapa, maarifa ambayo ni muhimu na tunaweza kuyatumia.

Kwa eneo la kuchukua hatua ndiyo halijakamilika kwa wote.

Wapo ambao wanachukua hatua na wapo ambao wanafurahia kupata maarifa lakini wanabaki pale pale.

Nafasi za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, hasa kwenye kundi la WASAP zinazidi kuwa finyu kutokana na wengi kuhitaji nafasi hii ya mafunzo.

Hivyo ili kuhakikisha mtu unapata nafasi hii ya kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kuwepo, kuna vigezo muhimu ambavyo unapaswa kuvitimiza.

Kujiunga mara ya kwanza kama nafasi ipo kunategemea kulipa kwako ada. Lakini ili kuendelea kuwa mwanachama, ada pekee haikutoshi kupata nafasi hiyo, bali unahitaji kutimiza vigezo hivi sana, ambavyo kwa jumla vinaleta alama kumi.

Vigezo saba vya kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

  1. Kulipa ada ya mwaka kwa wakati (alama 1)

Hapa unahitaji kulipa ada yako kwa wakati.

Kigezo cha ada ni cha lazima, lakini pekee hakikutoshi kuendelea kuwa mwanachama.

  1. Kushiriki mijadala ya KISIMA CHA MAARIFA (alama 1).

Hapa unapaswa kushiriki mijadala mbalimbali inayoendeshwa kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Unaweza kushiriki kwa kuuliza maswali, kutoa michango, kijibu maswali na hata kuwashirikisha wengine yale ambayo umejifunza.

  1. Taarifa za kila mwezi (alama 2)

Kila mwezi kuna zoezi la kufanya tathmini ya mwezi huo umeendaje kwa upande wako. Yapo maswali ambayo nimekuwa nayatuma yenye kukufanya utafakari maeneo muhimu ya maisha yako na kuona hatua ambazo unapiga.

Unapaswa kutoa taarifa za kila mwezi na hii itakupa alama moja.

  1. Biashara na uwekezaji (alama 1).

Hapa unapaswa kuwa na biashara au uwekezaji au njia yoyote ya ziada ya kukuingizia kipato, hasa kwa wale walioajiriwa.

  1. Kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi, angalau vitabu 10 kwa mwaka. (Alama 1)

Hapa unahitaji kujifunza kupitia usomaji wa vitabu, kitabu kimoja kila mwezi na angalau vitabu 10 kwa mwaka. Kama unapata changamoto ya kusoma vitabu unaweza kujiunga na program ya KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU. Hii itakusaidia kuweza kusoma kitabu kimoja kila mwezi. Kwa maelezo zaidi kuhusu program ya kurasa kumi, bonyeza maandishi haya.

  1. Personal coaching (alama 2).

Hapa unahitaji, angalau mara moja kwa mwaka kuingia kwenye program ya personal coaching ambapo kwa mwezi mzima tunafanyia kazi kitu fulani ambacho umekuwa unakwama au kushindwa kufanyia kazi kwenye maisha yako, kazi zako au biashara zako.

Kwenye program hii mimi nakuwa kocha wako moja kwa moja na kwa mwezi mmoja nakufuatilia kwa karibu kwenye kile unachotaka kupiga hatua. Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma hii ya PERSONAL COACHING bonyeza maandishi haya.

  1. Kuhudhuria semina ya mwaka (alama 2).

Kila mwaka tuna mkutano wetu wa KISIMA CHA MAARIFA wa kukutana ana kwa ana. Huu ni mkutano muhimu wa kila mmoja wetu kuhudhuria, ambapo tunajifunza na kushirikiana zaidi kwa pamoja. Kushiriki mkutano huu wa mwaka kunakupatia alama mbili.

Tathmini ya alama hizi.

Jumla ya alama ni 10.

Ili kuendelea kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kupata alama tano na kuendelea.

Chini ya alama tano, hata kama upo tayari kulipa ada, hutaipata nafasi hii tena.

Kwa watakaoweza kupata alama 10/10 hawa watakuwa na zawadi zao zaidi, hasa kupata nafasi ya kufanya kazi pamoja na kwa karibu kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao.

MUHIMU; Hii tathmini nitakuwa naifanya mwenyewe pale mtu anapokuwa amefikia ukingoni mwa ada yake.

Hivyo ukiona ada yako imeisha na umeondolewa bila ya kuambiwa ulipe ada ya mwaka unaofuata, jua alama zimekuwa chini.

Karibu sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, karibu sana tuyafanye maisha yetu kuwa bora na ya mafanikio kwenye kila eneo.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha