KARIBU KISIMA CHA MAARIFA

[et_pb_section bb_built=”1″][et_pb_row][et_pb_column type=”4_4″][et_pb_text]

KUHUSU KISIMA CHA MAARIFA

KISIMA CHA MAARIFA ni mtandao ambao unakupatia maarifa mbalimbali ya kuweza kuboresha maisha yako. Ni sehemu ambapo ninakushirikisha kila ninachojua na ninachojifunza kuhusu maisha na mafanikio.

Kupitia KISIMA CHA MAARIFA utapata mbinu nzuri za kuweza kufikia MAFANIKIO MAKUBWA kwenye maisha yako.

Ili kuweza kupata mbinu na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapaswa kuwa mwanachama kwa kujiunga na kulipa ada ya mwaka.

Ili uwe mwanachama unahitaji kulipia ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=) ada hii ni kwa mwaka mzima tangu tarehe unayojiunga, yaani miezi kumi na mbili tangu tarehe uliyojiunga.

Kwa kulipa ada hiyo ya mwaka na kuwa mwanachama unapata haya yafuatayo;

1. Kusoma makala zote kwenye kisima cha maarifa.

Makala za kwenye KISIMA zipo kwenye makundi yafuatayo;

a/. Makala za biashara na ujasiriamali, hapa unajifunza kwa kina kuhusu biashara.

b/. Makala za mbinu za mafanikio na kufikia mafanikio makubwa (WORLD CLASS), hapa unapata nafasi ya kujifunza mbinu zote bora za kufikia mafanikio kwenye maisha yako.

c/. Makala za uchambuzi wa vitabu, kila wiki unapata uchambuzi wa kitabu kimoja, chenye mbinu bora za mafanikio kwenye maisha, kazi na hata biashara.

d/. Makala za KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala za kila siku ambapo unapata mbinu za kuwa na maisha bora sana, kila siku.

e/. Makala za falsafa mpya ya maisha, hapa unapata maarifa kuhusu falsafa ya maisha na jinsi ya kuwa na maisha bora sana, bila ya kujali unaanzia wapi au umefikia wapi.

f/. Makala za uwekezaji ambapo utajifunza kuwa mwekezaji bora na kuweza kunufaika kupitia uwekezaji.

2. Unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la wasap/telegram, ambapo ndani ya kundi hilo unapata yafuatayo;

a/. Kuamka asubuhi na mapema kwa salamu ambayo ni chanya na inaifanya siku yako kuwa chanya.

b/. Kupata tafakari kuhusu maisha kila siku asubuhi, na hivyo kuianza siku yako ukiwa na fikra za kujenga na kusonga mbele zaidi.

c/. Kujifunza mambo mbalimbali kupitia DARASA LA JUMAPILI, ambapo tunajifunza moja kwa moja kutoka kwa wataalamu au watu wanaotoa shuhuda za mafanikio.

3. Kushiriki semina mbili zinazoendeshwa kwa njia ya mtandao.

Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kushiriki semina mbili zinazoendeshwa kwa njia ya mtandao. Semina ya kwanza inakuwa ni ya kuanza mwaka kwa mafanikio, inafanyika mwanzoni mwa mwaka. Na semina ya pili inakuwa kuhusu biashara ambayo inafanyika katikati ya mwaka.

4. Kupata nafasi ya kushiriki semina za moja kwa moja.

Kila mwaka kutakuwa na semina za moja kwa moja, ambazo zitakuwa maalumu kwa wanachama wa KISIMA CHA MAAROFA pekee. Kupitia semina hizi utajifunza na kuweza kushirikiana na wengine ili kufanikiwa zaidi.

Kutakuwa na gharama za ziada katika kushiriki semina hizi, lakini wanaoshiriki ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA TU. Hivyo kuwa mwanachama kunakupa upendeleo wa kushiriki semina hizi.

5. Kuwa karibu na Coach Makirita Amani.

Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unakuwa karibu kabisa na KOCHA MAKIRITA AMANI, inakuwa rahisi kwako kumuuliza chochote ndani ya kundi na akakujibu au kukupa ufafanuzi. Kupitia ukaribu huu na kocha utaweza kunufaika na mengi katika safari yako ya maisha ya mafanikio. Pia inakuwa rahisi kwako kuonana na kocha kwa ajili ya ushauri. Kwa sasa KOCHA hakutani na watu kwa ajili ya ushauri ila wale tu ambao ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA una uhakia wa siku yako kuwa chanya, kupata hamasa ya kuweka juhudi zaidi, na kushawishika kuishi maisha bora sana kwako na kwa wanaokuzunguka.

Kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA hakuna jinsi unaweza kuyakwepa mafanikio, ni lazima utakutana nayo tu, kama utafanyia kazi yale utakayojifunza.

JINSI YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA jaza fomu ya kujiunga kwa kuweka taarifa zako sahihi.  Baada ya kujaza fomu nenda kwenye email yako na utakuta taarifa zako utakazotumia kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Utaweza kulog in kwenye KISIMA CHA MAARIFA ila hutaweza kusoma makala zote mpaka utakapolipia ada ya uanachama.

Kulipia uanachama tuma ada ya mwaka ya uanachama, ambayo ni tsh 100,000/= kwenda kwenye namba zifuatazo; MPESA 0755 953 887, TIGO PESA 0717 396 253 Kama una AIRTEL MONEY unaweza kutuma moja kwa moja kwenye namba ya tigo-0717 396 253.(Jina litakuja AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma fedha hizo utatuma ujumbe wenye jina lako na email yako kwenye moja ya namba hizo na uanachama wako utaidhinishwa.

JAZA FOMU HII KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA

New User Registration
captcha
*Required field

[/et_pb_text][/et_pb_column][/et_pb_row][/et_pb_section]