Huduma Za Kocha

HUDUMA KUU ZA KOCHA DR. MAKIRITA AMANI.

Rafiki yangu mpendwa,

Nikushukuru kwa kipekee sana kwa kuwa mfuatiliaji wa mafunzo mbalimbali ninayoyatoa. Ni imani yangu umekuwa unapata maarifa sahihi na unachukua hatua kwa yale unayojifunza ili maisha yako yaweze kuwa bora zaidi.

Kama ungependa kupata ushauri, mwongozo na hata usimamizi wa kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako, nakukaribisha ujiunge na huduma nyingine ninazotoa.

Lengo kuu la huduma zote zinazotoa ni moja, kuhakikisha wewe unafikia mafanikio makubwa, kwani ninachoamini ni mafanikio yangu yanategemea mafanikio yako.

Hivyo karibu sana tushirikiane, ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

Msingi wa yote ninayofanya upo kwenye imani kwamba maarifa sahihi ndiyo ufunguo pekee wa maisha bora na mafanikio. Kwamba chochote tunachotaka tunaweza kukipata kama tukiwa na maarifa sahihi na kuchukua hatua kupitia maarifa hayo.

Ninaamini sana hili kwa sababu nimeona matokeo yake kwenye maisha yangu, mara zote ambazo nimekuwa nakwama ambacho kimekuwa kinanikwamua ni maarifa sahihi na kuchukua hatua kwenye maarifa hayo.

Na ndiyo maana kanuni kuu ya KISIMA CHA MAARIFA ni hii; MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA.

Rafiki, hapa nakwenda kukushirikisha taarifa ya bidhaa na huduma za maarifa na ukocha ninazotoa, ili tuweze kwenda pamoja vizuri na kila mmoja aweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.

Zifuatazo ni huduma za mafunzo, ukocha na ushauri ninazotoa.

Ili kuweza kupeleka muda na nguvu zangu sehemu sahihi ambayo itakuwa na manufaa makubwa, nimepunguza mambo ambayo nimekuwa nafanya. Kwa sasa huduma kuu ninazotoa zinakuwa nne (04) pekee na itakuwa kama ifuatavyo.

1.     AMKA MTANZANIA NA EMAIL.

Kila siku kuna makala nzuri za mafunzo na hamasa ambazo zitawekwa kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA pamoja na kutumwa kwenye email. Maarifa haya ni bure na yataendelea kuwa bure kabisa. Hutahitaji kulipia chochote.

Pamoja na maarifa haya kuwa bure, yataendelea kuwa ya thamani kubwa sana kiasi kwamba ukiyaweka kwenye matendo utaweza kupiga hatua kubwa sana.

Kila siku tembelea www.amkamtanzania.com kujifunza. Pia hakikisha umejiandikisha kwenye mfumo wetu wa email ili uweze kupokea email za mafunzo kila siku. Kujiandikisha fungua kiungo hiki; www.amkamtanzania.com/jiunge

2.     VITABU.

Nimeandika na ninaendelea kuandika vitabu vingi kwenye eneo la maendeleo binafsi, biashara, fedha na mafanikio. Vitabu ninavyoandika viko kwenye mifumo miwili, nakala tete (softcopy) na nakala ngumu (hardcopy).

Vitabu vya nakala tete vinapatikana kwenye APP ya SOMA VITABU ambayo ni rahisi kupata na kusoma vitabu hivyo. Unapaswa kupakua na kuweka app hiyo kwenye simu au tablet yako na uweze kusoma. Kupakua app na kupata maelezo ya jinsi ya kuitumia, fungua hapa; www.amkamtanzania.com/somavitabuapp

Vitabu vya nakala ngumu ni vile vinavyokuwa vimechapwa na kupatikana kwa mfumo wa kuwa na kitabu halisi. Kupata orodha ya vitabu nakala ngumu na jinsi ya kuvipata fungua hapa; www.amkamtanzania.com/vitabu

3.     CHANNEL YA SOMA VITABU TANZANIA.

Kama unapenda kusoma vitabu na kupata uchambuzi wa kina wa vitabu basi kuna huduma ya uchambuzi wa vitabu inayopatikana kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA. Kupitia channel hii unapata uchambuzi wa vitabu pamoja na vitabu vyenyewe. Kwa kujiunga na channel hii, utaweza kujisukuma kusoma vitabu zaidi kwenye maisha yako.

Gharama za kujiunga na channel hii ni tsh elfu 5 (5,000/=) kwa mwezi ambayo utalipa kila mwezi, au tsh elfu 50 (50,000/=) kwa mwaka ambapo utalipa kila mwaka. Wiki ya kwanza ya kujiunga na channel hii ni bure, hivyo una wiki nzima ya kupima kama channel hii ni bora kwako, na baada ya hapo unachagua kuendelea kujifunza kwa kulipa ada.

Karibu sana kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA hapa utajifunza na kupata hamasa ya kusoma vitabu, kupata maarifa sahihi, kuchukua hatua na kufikia mafanikio makubwa.

Kujiunga na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, fungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania kisha bonyeza JOIN CHANNEL.

4.     KISIMA CHA MAARIFA.

Huduma ya nne ya maarifa na ukocha ninayotoa ni KISIMA CHA MAARIFA. Hii ndiyo huduma kuu ambayo mtu yeyote makini na aliyejitoa kweli kufanikiwa anapaswa kujiunga nayo ili aweze kufikia mafanikio makubwa.

Hii ndiyo hatua ya kwanza ambayo kila anayetaka kujifunza zaidi kupitia kazi zangu anapaswa kujiunga nayo.

Kila anayetaka ushauri na hata ukocha kutoka kwangu, anapaswa kwanza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ndiyo ngazi ya kwanza ambayo mtu anapaswa kuipanda ili twende pamoja kwenye safari hii ya mafanikio. Naweza kusema pia kwamba hii ndiyo tiketi ambayo mtu anapaswa kuwa nayo ili tuwe karibu kwenye safari hii ya mafanikio.

KISIMA CHA MAAARIFA ni huduma ya kujiunga na kulipa ada ya mwaka mzima ambao unakuwa kwenye huduma hii. Gharama za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa sasa ni tsh laki tatu (300,000/=) ambayo inalipwa kwa mara moja na kulipwa tena mwaka unapoisha tangu mtu alipolipa. Ada hii inabadilika kadiri muda unavyokwenda.

Ada hiyo ni kubwa kwa wengi, lakini ni ndogo mno ukilinganisha na manufaa utakayopata kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama bado hujawa kwenye familia hii bora kabisa kwa mafanikio yako, unajichelewesha, jiunge na uanze kunufaika sasa.

FAIDA KUBWA SITA ZA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA.

Kama ambavyo nimekushirikisha hapo juu, KISIMA CHA MAARIFA ndiyo huduma kuu ya mafanikio ninayotoa. Ndiyo huduma ambayo nimeweka nguvu zangu nyingi kuhakikisha kila anayeitumia ananufaika kweli.

Zifuatazo ni faida sita kubwa za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

  1. MAFUNZO YA KILA SIKU, KILA JUMA NA TATHMINI YA MWEZI.

Unapojiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kila siku unapata mafunzo bora sana yatakayokusukuma kuchukua hatua zaidi ili kufanikiwa.

Kwanza kabisa unaianza siku kwa tafakari, ambayo inakufanya ufikiri tofauti na kukuondoa kwenye msongo pamoja na kukupa hamasa ya kupiga hatua zaidi.

Pili unapata makala ya KURASA ZA MAFANIKIO, hizi ni makala fupi zenye ujumbe muhimu sana kuhusu safari ya mafanikio.

Tatu unapata mjadala wa pamoja na wale ambao wapo kwenye safari ya mafanikio kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Pia unapata mafunzo na mijadala ya ziada kwenye mtandao wa MWONGOZO WA MAFANIKIO kupitia www.mafanikio.substack.com

Nne unapata nafasi ya kutoa na kupokea kutoka kwa wengine kupitia huduma ya ALHAMISI YA UTOAJI (Giving Thursday). Kila Alhamisi tunakuwa na huduma hii ya utoaji ambayo inaongozwa kwa msingi wa MAARIFA, RASILIMALI na CONNECTION, unapata vitu hivyo kutoka kwa wengine na wewe unawapa wengine pia.

Tano unapata nafasi ya kujifanyia tathmini kila mwezi ili kujua pale ulipo, na kule unakokwenda. Kila mwezi unatumiwa maswali ya kujifanyia tathmini kwa hatua ulizochukua na matokeo uliyopata. Maswali hayo yanakusaidia kujitambua na kuona wapi unalegalega ili kuweza kupiga hatua na kufanikiwa zaidi. Pia unapata ushauri wa karibu wa Kocha kulingana na tathmini yako ya mwezi.

  1. KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA pia unapata nafasi ya kuwa mwanachama wa KLABU YA KISIMA CHA MAARIFA. Hizi ni klabu za mafanikio ambapo mnakutana ana kwa ana wale wote mliopo eneo la karibu, ndani ya mkoa mmoja au wilaya moja.

Kwa kuwa ndani ya klabu hizi, unapata nafasi ya kujifunza na kuhamasika kutoka kwa wengine pia.

Kila mwezi mnakutana kama klabu mara moja, ambapo mnashirikishana maarifa ya kitabu ambacho kila mmoja amesoma, mnashirikishana mipango ambayo kila mmoja amefanyia kazi, changamoto alizokutana nazo na mipango ya mwezi unaofuata.

Pia kwa kuwa kwenye klabu hizi mnapata nafasi ya kutembeleana na kujifunza pamoja na kushauriana zaidi.

Klabu pia zitakuwa zinafanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kutoa misaada kwa wenye uhitaji, kuboresha mazingira na huduma nyingine za kijamii kama elimu na afya.

Muhimu zaidi, klabu hizi zitakuwa zinatembelewa na Kocha Dr Makirita Amani mara kwa mara ili kutoa mafunzo zaidi na kufuatilia maendeleo ya kila mmoja wetu.

Kwa kifupi, kuwa kwenye KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya kitu bora kabisa unachoweza kufanya kwenye maisha yako na kikakulipa sana.

  1. PERSONAL COACHING.

Hii ni huduma ambapo mimi nakuwa kocha wako moja kwa moja kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kupitia huduma hii, unakuwa na kitu ambacho unapanga kukifanyia kazi lakini umekuwa unaahirisha au huna hamasa ya kuanza na kuendelea.

Kupitia personal coaching tunafanya kazi kwa karibu na ninakufuatilia kuhakikisha unafanya kile ambacho umepanga kufanya.

Gharama ya huduma hii zipo ndani ya ada ya KISIMA CHA MAARIFA, hivyo ukishalipa ada ya mwaka, tayari una nafasi ya kupata PERSONAL COACHING kwa mwezi mmoja. Unachagua mwezi mmoja kwenye mwaka ambapo tutafanya PERSONAL COACHING ili uweze kupiga hatua kwa lolote ulilokwama.

Iwapo kuna kitu unataka kufanya, tabia unataka kubadili au mambo unataka kuyabadili, lakini unashindwa kuanza au ukianza unaishia njiani, PERSONAL COACHING itakusaidia sana.

  1. SEMINA YA KUKUTANA ANA KWA ANA.

Kila mwaka tunakuwa na semina kubwa ya kukutana ana kwa ana. Semina hii huwa inafanyika mara moja tu kwa mwaka na wanamafanikio kutoka sehemu mbalimbali za nchi pamoja na nje ya nchi tunakutana kujifunza na kuhamasika ili kuendelea na safari hii ya mafanikio.

Kwenye semina hizi, kunakuwa na mafunzo bora kabisa ya mafanikio. Lakini pia kitu kikubwa unachopata kwenye semina hii ni kusikia hadithi za wanamafanikio wengine ambao wameweza kutoka chini na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao.

Faida kubwa pia ya kushiriki semina hizi ni kukuza mtandao wako wa mafanikio. Maana kwenye semina hizi unakutana na watu mbalimbali, hivyo wapo ambao utaweza kujifunza zaidi kwao na wengine ukashirikiana nao kwenye kazi au biashara unazofanya.

Gharama za kushiriki semina hii ya ana kwa ana inategemea eneo inapofanyika na wakati pia.

  1. GAME CHANGERS.

Hii ni huduma ya ukocha ambayo naitoa kwa kikundi cha watu watano kwa pamoja. Kupitia huduma hii, watu watano ambao kila mtu ana kitu anataka kufanyia kazi au hatua anataka kupiga, wanakuwa kwenye kundi moja na wanakuwa wanafuatiliana kwa karibu kila mmoja.

Huduma hii inampa mtu manufaa mawili kwa pamoja, moja ni COACHING ambapo unakuwa karibu na kocha anayekupa mwongozo na mbili ni MASTERMIND GROUP ambapo unazungukwa na wengine ambao nao wana mpango wa kufanya kitu kikubwa na hivyo mnafuatiliana na kusukumana kwa pamoja.

Pia mara moja kila wiki tunakuwa na simu ya pamoja (conference call) ambapo tunakuwa kwenye simu ya pamoja wote, kila mtu anaeleza yale anayofanyia kazi, anahojiwa kwa kina na wengine na kutoa mrejesho wa yale anayofanyia kazi, au aliyoshauriwa kufanyia kazi kipindi kilichopita.

Huduma hii ya ukocha ya GAME CHANGERS inatolewa kwa misimu, hivyo nakuwa natangaza kipindi cha watu kujiunga na huduma hii.

Huduma hii ni kwa wiki 5, ambazo watu wanafanya kazi pamoja na kuhakikisha ndani ya wiki hizo tano kila mtu anaondoka na kitu alichofanya au kuzalisha.

Gharama ya huduma hii ni tsh 500,000/= ambayo ni kwa kipindi hicho cha wiki 5. Ada inalipwa kabla ya huduma kuanza na inalipwa yote kwa pamoja.

  1. LEVEL UP.

Hii ni huduma maalumu ya ukocha kwa wale watu ambao wanataka kupiga hatua kubwa kabisa kwenye maisha yao. Hii ni maalumu kwa wale watu ambao wamefanikiwa halafu mafanikio yakawa mtego kwao. Yaani mtu anakuwa amepiga hatua kwenye maisha yake, lakini akafika sehemu ambao anaona hapigi hatua tena. Anakuwa amedumaa na hana tena hamasa ya kusonga mbele.

Huduma hii naitoa kwa mtu mmoja mmoja ambaye nafanya naye kazi kubwa na kwa karibu sana kwa kipindi cha wiki 10. Katika wiki hizi kumi, tunatengeneza kabisa upya mfumo wa mtu wa kufikiri, tunatengeneza mpango mpya wa kufanyia kazi na kuufanyia kazi kuhakikisha hamasa inarudi upya na mtu anaendelea kuweka juhudi.

Gharama za huduma hii ya LEVEL UP ni tsh 2,000,000/= kwa kipindi chote cha wiki 10 na inalipwa kabla ya huduma kuanza.

Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwani ukishajiunga, una uwanja mpana sana wa kujifunza na kuwa karibu na Kocha na utaweza kupiga hatua zaidi kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Ili kupata huduma yoyote iliyoelezwa hapa, wasiliana na kocha kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 kwa simu au ujumbe wa kawaida au kwa ujumbe wa wasap namba 0717 396 253 na utaelezwa upatikanaji wa nafasi kwenye bidhaa unayohitaji pamoja na utaratibu wa malipo.

Karibu sana rafiki tuwe pamoja kwenye safari hii ya mafanikio. Nimekuwa najifunza sana kupitia wale ninaofanya nao kazi, na nimegundua kufanya kazi kwa karibu na watu wachache kunaleta matokeo makubwa sana. Ndiyo maana unaona huduma ya KISIMA CHA MAARIFA inalenga kufanya kazi na watu wachache. Nafasi kwenye huduma hii ya KISIMA CHA MAARIFA ni chache kuliko uhitaji wa watu, hivyo kama umesoma hapa na kuona ni kitu unachohitaji kweli basi nakushauri usisite, chukua hatua sasa na utajishukuru sana baadaye.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr. Makirita Amani.

Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

www.amkamtanzania.com/kocha