Tag Archives: HUDUMA KWA WATEJA

BIASHARA LEO; Je Biashara Yako Inaendana Na Wateja Wako?

By | July 10, 2015

Tulishasema kwamba jambo muhimu kabisa kwenye biashara ni kujua mteja wako ni nani. Kama upo kwenye biashara na humjui mteja wako basi hujui ni nini unafanya kwenye biashara yako. Na ninaposema kumjua simaanishi kumjua kwa jina, bali kujua sifa za mteja wako kuanzia umri, kipato, anakoishi na mengine kama hayo. (more…)

BIASHARA LEO; Hili ndio tatizo la kushindana kwa bei na linavyokumaliza.

By | July 9, 2015

Tatizo la kushindana kwa bei kwenye biashara ni kwamba linawamaliza wote mnaoshindana. Watu wengi huwa wanafikiri kwamba kwa kuweka bei ndogo basi ndio wanavutia wateja wengi. Hivyo wanaweka bei ndogo na mwanzoni wateja wanakuja kweli, baadae mshindani wako naye anashusha bei na wateja wanaenda kwake tena. Mnafanya mchezo huu kwa (more…)

BIASHARA LEO; Je Umemridhisha Mteja Wako Leo?

By | July 8, 2015

Kama jibu lako ni sina mteja basi jitathmini vizuri. Kwanza kabisa kila mmoja wetu ana mteja, kama wewe ni mtu mzima na unaishi basi una mteja au una wateja wengi sana. Wateja hawaishii kwa wafanyabiashara tu. Wateja wapo kwa kila mtu. Kama wewe ni mfanyabiashara, mteja wako au wateja wako (more…)

Umuhimu wa mafunzo kwa wafanyakazi wa biashara yako.

By | June 29, 2015

Kama unafanya biashara kubwa maana yake una watu wengi ambao wanakusaidia kwenye biashara hiyo. Biashara yako haiwezi kukua na kuendelea kama huna watu wazuri ambao wanafanya kazi kwenye biashara hiyo. Na hata kama una biashara ndogo malengo yako ni kukua zaidi ya hapo ulipo sasa. Ili kukua utahitaji kuwa na (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Chaguo Mbadala.

By | June 27, 2015

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipoteza wateja kwa kushindwa kufanya kitu rahisi sana, kutoa chaguo mbadala kwa wateja wako. Kwa mfano mteja amekuja anataka kitu fulani ambacho wewe huna, badala ya kumwambia tu mimi sina hicho na aondoke, unaweza kumwambia sina hicho unachotaka ila kuna hiki kingine ambacho kinafanya kazi sawa na (more…)

BIASHARA LEO; Sababu Za Kijinga Zinazokupotezea Wateja Kwenye Biashara Yako.

By | June 25, 2015

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamika biashara ni ngumu, biashara hazina wateja, biashara zina ushindani mkali na mengine mengi. Lakini kila ukichunguza biashara nyingi unaona makosa mengi ya kijinga ambayo wafanyabiashara wamekuwa wanafanya na yanawafukuza wateja. Yaani naweza kusema kwamba kama biashara inakufa, asilimia 90 ya sababu za kufa kwa biashara hiyo (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Viwili Muhimu Kujua Kuhusu Wateja Wa Biashara Yako.

By | June 24, 2015

Kwanza kabisa kama ambavyo nimekuwa nasisitiza, usiwe kwenye biashara ambayo hujui mteja wako ni nani. Tafadhali sana, chukua muda wa kumjua mteja wako au achana na biashara hiyo. Humsaidii yeyote kwa kutojua mteja wa biashara yako, na biashara itakuwa ngumu sana kwako kama hujui mteja wako ni nani. Sasa kikubwa (more…)

BIASHARA LEO; Je Unatangaza Biashara Au Unapiga Kelele Kwenye Mitandao Ya Kijamii?

By | June 18, 2015

Mitandao ya kijamii ni sehemu nzuri sana ya kutangaza biashara yako. Hii ni sehemu ambayo wateja wako wanakuwepo kwa muda mrefu na wanafuatilia mambo mbalimbali. Lakini changamoto moja inakuja kamba wengi wa watu wanaotangaza kwenye mitandao hii, kiuhalisia hawatangazi, bali wanapiga kelele. Na kwa jamii ya sasa, watu hawataki kelele, (more…)

BIASHARA LEO; Changamoto Ya Kupanga Bei Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo.

By | June 15, 2015

Kupanga bei kwenye biashara ni changamoto kubwa sana unayotakiwa kuifanyia kazi vizuri kama kweli unataka kupata mafanikio makubwa kupitia biashara unayofanya. Watu wengi wamekuwa wakifikiria kwamba ukishusha bei basi utapata wateja wengi sana. Huu sio ukweli kuuza vitu kwa bei ya chini kunaweza kuwa kikwazo kwako kupata wateja wengi zaidi (more…)

Vitu muhimu vya kuzingatia ili kukuza biashara yako.

By | June 15, 2015

Peter Drucker, aliyekuwa mtaalamu wa usimamizi kwenye biashara, aliwahi kusema kwamba kwa kuwa lengo la biashara ni kutengeneza wateja, biashara yoyote ina majukumu mawili tu ya msingi; masoko na ubunifu. Vitu hivi viwili ndio vinaleta faida kwenye biashara, vingine vyote vinaleta gharama. Leo katika makala hii ya kona ya mjasiriamali (more…)