Tag Archives: UONGOZI

Kilichotokea Afrika Kusini Na Somo Kubwa La Sisi Watanzania Kujifunza.

By | May 5, 2015

Siku za hivi karibuni kumetokea machafuko nchini Afrika Kusini yaliyosababishwa na wananchi ambao ni wazawa wa nchi hiyo, kuwavamia na kuwafukuza wananchi ambao ni raia wa nchi nyingine. Machafuko hayo sio ya kwanza kutokea kwa Afrika Kusini na hata kwa Afrika kwa ujumla. Kumekuwepo na maandamano na machafuko ya aina (more…)

Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka Kwa Rais Wa Tanzania Mwaka 2040.

By | January 1, 2015

Napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kuwatakia watanzania wenzangu wote kheri na hongera ya kuuona mwaka 2015. Sio watu wote walioanza mwaka 2014 wamepata nafasi ya kuuona mwaka 2015, hivyo ni jambo la kushukuru kwa nafasi hii ya kipekee. Mwaka 2014 huenda ulikuwa mwaka uliokuwezesha kufanikisha mengi na pia kushindwa (more…)

Nenda Kapige Kura, Au Usipige Na Fanya Hivi…

By | December 14, 2014

Leo ni siku ya kupiga kura kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa, najua unajua hili, ila imebidi niliandike tena ili tupate pa kuanzia. Kama ulikuwa hujui leo ndio siku ya uchaguzi basi tuna tatizo kubwa zaidi. Kwa takwimu mbalimbali za chaguzi zilizopita tunaona idadi kubwa ya watu waliojiandikisha hawapigi kura. (more…)

Mahitaji Manne Ya Mtu Kuwa Kiongozi.

By | November 23, 2014

Ili uweze kuwa kiongozi bora na mwenye mafanikio kuna vitu vinne unavyotakiwa kuwa navyo na uweze kuvisimamia. Kwa kujua na kusimamia vitu hivi kutakuwezesha kufanikiwa sana kama kiongozi. 1. Kuweza kujisimamia mwenyewe. Kiongozi bora ni yule ambaye anayeweza kujisimamia mwenyewe. Ni lazima uweze kujiwekea malengo na mipango yako mwenyewe na (more…)

Nguzo Kuu Ya Uongozi; Tekeleza Kile Unachoahidi.

By | November 9, 2014

Katika kujijenga kuwa kiongozi bora na imara kuna misingi mingi ya uongozi ambayo unatakiwa kuifuata. Kushindwa kufuata misingi hii kutapelekea uongozi wako kushindwa na hata kudharaulika sana. Moja ya nguzo muhimu za uongozi ni kutekeleza kile unachoahidi. Kuongea ni rahisi sana na hivyo watu wengi hujikuta wakiongea mambo ambayo hawana (more…)

Tukemee Tabia Hii Mbaya Kama Taifa.

By | November 3, 2014

Jana tarehe 02/11/2014 kulikuwa na mdahalo wa katiba ulioandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere uliokuwa unafanyika katika ukumbi wa ukumbi wa ubungo plaza. Katika mdahalo huo waliokuwa wajumbe wa iliyokuwa tume ya katiba walialikwa kuzungumza na baadae wananchi waliohudhuria nao wangepata nafasi ya kuzungumzia katiba pendekezwa. Lengo kubwa la mdahalo (more…)

Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Ni Muhimu Sana. Tuzingatie Mambo Haya Matano.

By | November 2, 2014

Tarehe 14/12/2014 itakuwa siku muhimu sana katika miaka mitano ijayo. Siku hii itakuwa ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Watu wengi sana hawaupi uchaguzi huu nafasi kubwa na wameelekeza macho na masikio yao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hili ni kosa kubwa sana ambalo tunafanya watanzania wenzangu. (more…)

Ushauri Muhimu Kwa Wanafunzi Wa Kidato Cha Nne.

By | October 31, 2014

Jumatatu ijayo tarehe 03/11/2014 wanafunzi wa kidato cha nne wanakwenda kuanza mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne. Hii ni hatua muhimu sana kwenye maisha yao kwani ndio itapelekea ndoto zao nyingine kuwa kweli. Kama mwananfunzi ana ndoto ya kuwa injinia, rubani, daktari au mwalimu, mitihani hii ni muhimu kwake (more…)

Viongozi 100 Walioibadili Dunia.

By | October 14, 2014

Hii hapa ni orodha ya viongozi 100 walioibadili dunia kutokana na falsafa zao na misimamo yao. Viongozi hawa wako katika kada mbalimbali ikiwemo siasa, biashara, taaluma, dini na hata wanaharakati. Unaweza kubonyeza majina yao ili kujifunza zaidi. 1. Jesus Christ (c.5BC – 30AD) Spiritual Teacher, central figure of Christianity. 2. (more…)

Tabia Tatu Za Viongozi Dhaifu, Na Jinsi Ya Kuepuka Kuwa Mmoja Wao.

By | October 13, 2014

Ni vizuri sana kujifunza kutoka kwa viongozi waliofanikiwa maana hapa unapata njia ya vitu gani vya kufanya ili na wewe uweze kufanikiwa kama kiongozi. Ni vizuri pia kujifunza kutoka kwa viongozi walioshindwa kwa sababu kupitia kushindwa kwao unajua ni vitu gani vimewafanya washindwe na hivyo kuviepuka ili na wewe usiishie (more…)