Tag Archives: KUZA BIASHARA

BIASHARA LEO; Umuhimu Na Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Kwa Wateja Wako.

By | June 12, 2015

Biashara ni uaminifu, kama hakuna uaminifu hakuna biashara. Kama bado unafanya biashara kwa mazoea yale ya zamani kwamba biashara ni kuwaibia watu, usiendelee kusoma makala hii maana tutakavyojadili hapa hutavielewa. Badala yake fungua makala za nyuma kwenye kipengele hiki cha BIASHARA LEO na uanze kujifunza yale muhimu kwanza. Sasa twende (more…)

BIASHARA LEO; Sehemu Mbili Anazokwenda Mteja Wako Unazotakiwa Kuzijua.

By | June 10, 2015

Unapokuwa kwenye biashara, jukumu lako kubwa ni kumjua mteja wako kuliko hata anavyojijua wewe mwenyewe. Labda sio, lakini cha msingi lazima umjue mteja wako vizuri. Changamoto nyingi za biashara zinaanza pale mfanyabiashara anaposhindwa kumjua mteja wake vizuri na hivyo anashindwa kwenda naye vizuri kwenye biashara yake. Kama unasema huna haja (more…)

BIASHARA LEO; Njia Tatu Muhimu Za Kukuza Biashara Yako.

By | June 9, 2015

Unafanyia kazi haya unayojifunza kwenye kipengele hiki cha BIASHARA LEO? Kama unafanyia tushirikishe kwenye maoni hapo chini ni jinsi gani biashara yako inabadilika. Na kama hufanyii kazi tuambie ni kwa nini? Yote tunayojifunza kwenye kipengele hiki sio vitu vya kufurahia kusoma, bali ni vitu unatakiwa kufanya. Unasoma kitu hapa na (more…)

BIASHARA LEO; Hapa Ndio Biashara Yako Inapokosa Maana…

By | May 25, 2015

Unapojaribu kuwa kila kitu kwa kila mtu biashara yako inakosa maana na unashindwa kuwa chochote kwa yeyote. Ufanye nini basi; kuna wa pekee kwa kundi fulani la watu. Usitake kumpata kila mteja aliyepo hapa duniani, bali lenga kuwapata wale watu ambao utaongeza maana kwenye maisha yao, utatatua matatizo yao na (more…)

BIASHARA LEO; Aina Tatu Za Wateja Na Jinsi Unavyoweza Kufaidika Nao.

By | April 29, 2015

Unapoanza biashara, una kazi kubwa ya kufanya kujua wateja wako ni watu wa aina gani. Hili ni jambo muhimu sana ili uweze kuwapatia kile ambacho wanahitaji, uweze kutatua matatizo yao na kisha wakupatie wewe fedha. Japokuwa wateja wako wanawez akuwa na tatizo sawa, lakini bado hawafanani. Kutokana na tabia tofauti (more…)

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Biashara Kubwa Kwa Kuanzia Chini Kabisa, Hata Kama Huna Kitu.

By | April 29, 2015

Semina ya mafanikio kupitia biashara mwaka 2015 imebaki siku mbili tu ili uweze kujiunga. Kama unapitia changamoto zozote kwenye biashara yako au hata kama huna changamoto ila ungependa kufikia mafanikio makubwa usikose kujiunga na semina hii. Mwisho wa kujiunga ni ijumaa hii tarehe 01/05/2015. Baada ya hapo hutapata tena nafasi (more…)

BIASHARA LEO; Hivi Ndivyo Unavyokaribisha Ushindani Kwenye Biashara Yako.

By | April 27, 2015

Moja ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi huwa wanayafanya na yanawagharimu ni kufikiri kwamba watu wengine hawaoni kile ambacho wanakifanya. Wanafikiri kwamba wamejifungia wkenye ulimwengu wao wenyewe na kufanya mambo yao wenyewe. Ukweli ni kwamba kama unafanya biashara na inaonesha mafanikio makubwa, kuna watu wengi wanaiona biashara hiyo na wameshaanza kufikiria (more…)

BIASHARA LEO; Umuhimu Wa Hadithi Ya Biashara Yako.

By | April 3, 2015

Tunaishi kwenye dunia ambayo watu hawanunui kwa sababu tu unauza. Zamani biashara ilikuwa rahisi, uza na watakuja kununua. Fungua biashara na watu watakuja. Tangaza biashara yako kwenye vyombo vinavyowafikia wafikia wengi na utapata wateja wengi. Ila sasa hivi mambo mengi yamebadilika. Watu hawanunui tena kwa sababu wewe unauza, hii ni (more…)