Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 198; Tuko Upande Mmoja.

By | July 17, 2015

Katika shule moja kulikuwa na kundi la wanafunzi watukutu ambao walikuwa wakionea wanafunzi wenzao. Wanafunzi hao walikuwa wakikuta mwanafunzi mwingine wanamlazimisha achague wa kupigana naye na akikataa wanampiga wote. Siku moja kundi hili walikutana na mwanafunzi mmoja aliyeonekana kuwa mnyonge sana. Wakamwambia achague wa kupigana naye. Yule mwanafunzi akachora mstari (more…)

UKURASA WA 197; Una Sababu Moja Tu, Nyingine Zote Ni Kuchagua.

By | July 16, 2015

Umekuwa ukisikia mara nyingi kwamba kosa sio kutenda kosa, bali kosa ni kurudia kosa. Hii ikiwa na maana kwamba unapofanya jambo kwa mara ya kwanza na ukapata majibu ambayo hukutegemea kupata, tunaweza kukusamehe. Ila tunatarajia kwamba uwe umejifunza kwamba njia uliyotumia mwanzo haileti majibu unaotaka. Sasa kama wewe utarudia tena (more…)

UKURASA WA 196; Kama Huwezi Kujibu Swali Hili Hujui Maisha Yako Yanakoelekea.

By | July 15, 2015

Siku zote huwa nasema kwamba kuna ‘emergency’ chache sana kwenye maisha. Ile hali kwamba jambo limetokea na watu wanashangaa limetokeaje ni kuamua tu kutumia unafiki wetu wenyewe. Ni sawa na shimo ambalo lipo njiani kwa muda mrefu lakini watu wanaliangalia tu, siku moja linasababisha vifo watu wanasema ni ajali. Hapana (more…)

UKURASA WA 195; Dunia Inapenda Washindi, Usiumizwe Na Hilo.

By | July 14, 2015

Wakati unaweka juhudi za ziada zaidi ya wengine hakuna atakayekutukuza, na wengine wengi watakukatisha tamaa. Wakati wewe unafanya kazi wakati wengine wamepumzika, wanastareheka hakuna atakayekuwa anakumulika, na wanaojua watakuwa wanakubeza na kukuona hujui unachofanya. Kama utaendelea kung’ang’ana na kuweka juhudi licha ya watu kukususa na wengine kukukatisha tamaa, unajua ni (more…)

UKURASA WA 194; Utaanza kuona fursa nzuri pale utakapofanya hivi.

By | July 13, 2015

Hivi ulishawahi kununua nguo ambayo uliona ni nzuri na ya kipekee ila kila ulipopita mtaani ukaanza kuona karibu kila mtu anayo? Au labda unafikiria kununua kitu fulani mfano gari au vifaa, mara ghafla ukiwasha tv unaona kitu kile, ukipita mtaani unaona kitu kile? Au umewahi kufikiria kufanya biashara fulani mara (more…)

UKURASA WA 193; Ushabiki Unavyokuzuia Kufikia Mafanikio.

By | July 12, 2015

Ushabiki umekuwa kikwazo kwa watu wengi sana kuweza kufikia mafanikio makubwa. Watu wamekuwa wakijikuta wanalazimika kuacha mambo yao ya msingi kwa sababu hataki kupitwa na kitu ambacho anashabikia. Kuna watu ambao ni mashabiki wa mpira kiasi kamba hawezi kuacha kuangalia timu yake inacheza hata kama kutakuwa na kitu gani anachofanya. (more…)

UKURASA WA 192; Tatizo La Kuweka Kipimo Cha Furaha, Na Kwa Nini Hukifikii.

By | July 11, 2015

Kuna watu ambao huwa wanaweka furaha kwenye kipimo. Mtu anafikiri nikishapa kitu fulani basi nitakuwa na furaha sana. Kwa hiyo huwa inaanza hivi; Uko mtoto mdogo unatamani sana kwenda shule unasema nikianza darasa la kwanza nitafurahi sana. Unaanza na unagundua hakuna kitu cha tofauti sana. Unaendelea na shule kwa miaka (more…)

UKURASA WA 191; unalipwa kwa sababu unaonekana au kwa sababu unatoa thamani?

By | July 10, 2015

Swali muhimu sana hilo kujiuliza kama hujawahi kufanya hivyo. Ngoja nikuulize tena vizuri ili twende sawa, Je unalipwa mshahara kwa sababu unaonekana kazi au kwa sababu una thamani unayotoa kwenye kazi yako? Je mteja wa biashara yako ananunua kutoka kwako kwa sababu amekuona na wewe unafanya biashara au kwa sababu (more…)

UKURASA WA 190; Huwezi Au Hutaki? Kabla Hujaniambia Huwezi, Hakikisha Huponi.

By | July 9, 2015

Mpaka sasa umeshajifunza mambo mengi sana kuhusu mbinu za kuboresha kazi yako, biashara yako na hata maisha yako kwa ujumla. Lakini mbona bado huchukui hatua yoyote ili kuweza kunufaika na yale ambayo unajifunza? Mpaka sasa unajua kabisa ya kwamba kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya utaendelea kupata matokeo ambayo (more…)

UKURASA WA 189; Matatizo Yote Ya Mahusiano Yanaanzia Hapa… Sehemu Ya Pili(2)

By | July 8, 2015

Jana nilikushirikisha sababu kubwa ya matatizo kwenye mahusiano yetu sisi na watu wengine. Na kama ukiweza kuondokana na chanzo kile basi utapunguza sehemu kubwa sana ya matatizo kwenye mahusiano yako iwe ya kikazi, kibiashara, kindugu au kimapenzi. Kama hukupata nafasi ya kusoma kile tulichojadili jana basi kisome hapa; Matatizo Yote (more…)