Tag Archives: MAFANIKIO KWENYE BIASHARA

Tatizo la kuajiri wafanyakazi wasio na sifa kwenye biashara yako.

By | July 13, 2015

Mapinduzi ya viwanda yaliyotokea takribani karne mbili zilizopita yalileta mabadiliko makubwa sana kwenye ufanyaji wa kazi. Kabla ya hapo hakukuwa na ajira rasmi na hivyo watu wengi walizalisha kwa kiwango kidogo na kubadilishana. Viwanda vilipokuja viliweza kuzalisha kwa kiwango kikubwa sana na hivyo kuhitaji wafanyakazi wengi. Na kwa kuwa wafanyakazi (more…)

BIASHARA LEO; Hiki Ndio Kitu Pekee Kitakachoifanya Biashara Yako Ndogo Iweze Kumudu Ushindani.

By | July 1, 2015

Kama unaendesha biashara ndogo, au unaendesha biashara mpya ambayo tayari kuna watu wengine ambao wanaifanya biashara hii kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe, basi una njia nyembembe sana ya kuweza kufanikiwa. Ukweli ni kwamba hawa waliopo kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko (more…)

BIASHARA LEO; Mpango Wa Biashara Sio Biashara.

By | June 30, 2015

Nina mpango mzuri sana wa biashara, biashara hii itakuwa na wateja wengi na itatengeneza faida kubwa. Asante kwa mpango huo mzuri, lakini elewa kwamba mpango wa biashara sio biashara. Unaweza kuandika vizuri sana kwenye karatasi zako mteja wako ni nani, yupo wapi na utawezaje kumfikia, lakini hii sio biashara. Sisemi (more…)

Umuhimu wa mafunzo kwa wafanyakazi wa biashara yako.

By | June 29, 2015

Kama unafanya biashara kubwa maana yake una watu wengi ambao wanakusaidia kwenye biashara hiyo. Biashara yako haiwezi kukua na kuendelea kama huna watu wazuri ambao wanafanya kazi kwenye biashara hiyo. Na hata kama una biashara ndogo malengo yako ni kukua zaidi ya hapo ulipo sasa. Ili kukua utahitaji kuwa na (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Chaguo Mbadala.

By | June 27, 2015

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipoteza wateja kwa kushindwa kufanya kitu rahisi sana, kutoa chaguo mbadala kwa wateja wako. Kwa mfano mteja amekuja anataka kitu fulani ambacho wewe huna, badala ya kumwambia tu mimi sina hicho na aondoke, unaweza kumwambia sina hicho unachotaka ila kuna hiki kingine ambacho kinafanya kazi sawa na (more…)

BIASHARA LEO; Epuka Siri Kwenye Biashara Yako, Hasa Wakati Wa Matatizo.

By | June 26, 2015

Wamiliki wengi wa biashara huwa wanapenda kuweka matatizo ya biashara zao kuwa siri yao wenyewe. Hata watu ambao wanahusika na biashara hiyo kwa karibu sana hawapati nafasi ya kujua kama biashara ipo kwenye matatizo. Watu kama wafanyakazi wa biashara hiyo wanakuwa hawajui kama biashara ipo kwenye matatizo na hivyo kuendelea (more…)

BIASHARA LEO; Sababu Za Kijinga Zinazokupotezea Wateja Kwenye Biashara Yako.

By | June 25, 2015

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamika biashara ni ngumu, biashara hazina wateja, biashara zina ushindani mkali na mengine mengi. Lakini kila ukichunguza biashara nyingi unaona makosa mengi ya kijinga ambayo wafanyabiashara wamekuwa wanafanya na yanawafukuza wateja. Yaani naweza kusema kwamba kama biashara inakufa, asilimia 90 ya sababu za kufa kwa biashara hiyo (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Viwili Muhimu Kujua Kuhusu Wateja Wa Biashara Yako.

By | June 24, 2015

Kwanza kabisa kama ambavyo nimekuwa nasisitiza, usiwe kwenye biashara ambayo hujui mteja wako ni nani. Tafadhali sana, chukua muda wa kumjua mteja wako au achana na biashara hiyo. Humsaidii yeyote kwa kutojua mteja wa biashara yako, na biashara itakuwa ngumu sana kwako kama hujui mteja wako ni nani. Sasa kikubwa (more…)

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia kwenye ubia wa kibiashara.

By | June 22, 2015

Moja ya njia rahisi za kuingia kwenye biashara au kukuza biashara yako ni kuingia kwenye ubia na mtu mwingine. Watu wengi wametumia njia hii, ila ni wachache sana ambao wameweza kufanikiwa kuendesha biashara zao vizuri kwa njia hii ya ubia. Watu wengi wanaoingia kwenye ubia wamekuwa wakiishia kugombana na kushindwa (more…)

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuingia kwenye ubia wa kibiashara.

By | June 22, 2015

Moja ya njia rahisi za kuingia kwenye biashara au kukuza biashara yako ni kuingia kwenye ubia na mtu mwingine. Watu wengi wametumia njia hii, ila ni wachache sana ambao wameweza kufanikiwa kuendesha biashara zao vizuri kwa njia hii ya ubia. Watu wengi wanaoingia kwenye ubia wamekuwa wakiishia kugombana na kushindwa (more…)